Mkuu @figaniga hii mada ni nzuri ILA kwa walionyimwa visa watatolea hasira zote hapa;(
Maisha ni popote unapoona kuna furaha kwako wewe,na unaweza kupahimili katika suala zima la utafutaji.
Kuhusu mchango kwa pato la taifa..hmmm don think kama kuna uzito kivile tena kwa hali ya kiuchumi na kashda za kisiasa Tanzania ilivo sasa mtu akigundua anachangia taifa atastop!!
Saivi bana ni kustrugle kivyako kwa manufaa yako na familia yako.
Ukiwa Nyumbani...Ukiwa Ulaya usipokuwa mvivu na mchaguzi wa kazi unatoka tuu..
Ulaya social security,sheria zinakulinda,huwezi mfanyisha mtu kazi bila kumlipa au hadi aandamane ndo alipwe. . Longolongo za kukatisha tamaa kama mishahara ya walimu hakuna! Kiafya unauhakika wa matibabu sahihi,tofauti na bongo unamalaria unapewa dawa za kifafa!!
Huduma muhimu za jamii kwa nchi za wenzetu,zipo kwa uhakika na zinatolewa kwa usalama..
Suala la mashauzi kwenye mitandao ,me naona ni mtu mwenyewe maana kuna wasio nje anaposts picha kimashauzi balaa na inaonekana kawaida ila mtu ukiwa ulaya ukapiga hata picha pembeni ya gas station unaonekana mashauzi!!
Mtu akiamua kujishusha mwenyewe hata ummezeshe chaki hawezi kuelewa. We utakavochukulia hali yako ndo itakavokufanya umjudge mwenzio.
Kuhusu Lugha ,ukikaa hata Moshi au Arusha muda mrefu lazima kuna utakacho copy bila kupenda,kama sio lafudhi,basi hata tabia.. So applied to Mtu alie nje,we mtu unafanya kazi 24/7 ki-inglish kwa miaka mingap sijuw ,kiswahil maybe ukutane na mbongo mwenzio kwenye shughuli ama kwa simu ama jf ama familia yako..yan muda mwingi wewe katika masaa24 masaa20 ni english sasa em tuambiane apo..utasema mtu anajishaua?
Popote ulipo,malezi uliyokulia,hofu yako kwa Mungu,hekima kwa wenzio na juhudi zako katika utafutaji ndo zitakufanya uwe wewe kama ulivyo na michango, mitazamo,misaada kwa familia yako na taifa kwa ujumla.