KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,185
- 37,239
Habari waungwana wa humu.
Bila shaka hakuna aliye mgeni wa kadhia hii kwenye maisha yetu ya kila siku kwenye jamii zetu..
Kama kawaida ya watu duni umoja wetu ndio nguvu yetu ya kufanikisha yale yanayoonekana yako nje ya kimo chetu kiuchumi.
Mshikamano ni jambo la msingi sana lakini inakuwa kheri zaidi ukielekezewa kwenye mambo ya msingi kwenye jamii yetu kwa ujumla wake kama vile afya, elimu, misiba na majanga mengine ya kiasili.
Suala la ndoa au kufanya harusi ni suala binafsi..ambalo watu wa nje ya wale watu wako wa karibu inabakia kuwa ni khiyari kwao na sio kama shuruti
Kwenye jamii yetu kumezuka hali ya kudai na kulazimishana michango ya harusi utadhani ni deni mtu anakudai.
Wao wanakaa kwenye kamati zao na kuandaa bajeti zao ambazo wanajua kabisa haziendani na misuli yao kiuchumi.....alafu wanaamua kulingana na bajeti hii kila mtu atoe kiasi fulani cha fedha.
Ndugu zanguni hii si sawa...si vyema kupanga bajeti zenu za anasa kwenye mifuko ya watu wengine....Hali ya maisha ni ngumu.
Tunajua na kutambua kuwa ndoa ni jambo kheri lakini bado kwa asilimia kubwa linabakia kwenye uwezo wa muoaji kwanza na khiyari ya michango ya watu wengine
Kwanini usifanye jambo lako kwa wepesi kwa kadri ya uwezo wako kiuchumi....kwanini uhangaishe au kusumbua kwenye jambo ulilolipanga mwenyewe.....
Ukishampa mtu taarifa basi muache afanye khiyari mwenyewe na so kumfuatilia kama wale watu wa OYA..
MCHANGO WA HARUSI SIO DENI.......