Mchawi wa Yanga ni mfumo wa uongozi. Msolla na Mwakalebela waondoke kwanza

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
Habari wadau,

Nimeona yanga leo tumemfukuza kocha Kaze.

Hii haijatosha. Niliwahi kuandika kwenye uzi wa Enyimba success case study maneno haya.

Mimi ni mwanayanga ila naona kabisa simba atatwaa caf champions league mapema kuliko yanga yangu kwa staili yetu ya kuwapa vyeo kina Msolla.

Wazee kama Msolla kwa mfano ukweli kabisa mabadiliko hayataki ila anazuga anayataka kwa mbinu ya kuyachelewesha ili ale pesa za yanga mpaka anazeeka na kustaafu. Msolla sio mjinga kuchelewesha mabadiliko, anajua yakija haraka cheo chake kitafutwa na yeye atakosa ajira.

Enyimba wa igbo waliamua kumpa timu mzee Kalu na akaifanya timu iwe kigogo Africa.

Mamelodi pia waliamua kumpa timu mzee Motsepe.

Yanga GSM hawezi kuweka hela za kutosha sababu hajapewa timu kama Mo alivyopewa Simba.

Msolla na Mwakalebela wasepe timu apewe tajiri mmoja iwe kama yake rasmi.

Mazembe haijaanzishwa na Moise Katumbi ila wanachama walimpa timu mwekezaji Moise Katumbi mafanikio yakaja

Mamelodi haijaanzishwa na Motsepe ila wanachama walimpa timu mwekezaji Motsepe mafanikio yakaja

Enyimba haijaanzishwa na Kalu, ila wanachama walimpa timu mwekezaji Kalu mafanikio yakaja.

Simba wameshampa Mo mafanikio tunayaona wote.

YANGA NA SISI NI ZAMU YA KUMPA TIMU MWEKEZAJI, MSOLLA NA MWAKALEBELA VYEO VYAO VIFUTWE WASEPE
 
Timu inatakiwa kuendeshwa kama kampuni, kama biashara. Mfumo wanaotumia haufai kabisa, hasa kwa nchi zetu ambazo wanachama ni hohehahe.
 
Watakuja hapa watu kukosoa, tafadhali andaa majibu ya kutosha mkuu ikikubidi njoo na mifano kama hiyo kutoka Ulaya.
 
Baselona timu walimpa nani ili kutawala soka la ulaya?
 
Baselona timu walimpa nani ili kutawala soka la ulaya?

Wanachama wa ulaya tofauti na africa. Kila mwanachama akinunua jezi original tu ambayo bei zao za laki tatu. Timu inajaa mahela.

Mpira wa africa tofauti na ulaya. Sababu wanachama ni maskini hawawezi kumudu gharama za kuendesha klabu.
 
Wanachama wa ulaya tofauti na africa. Kila mwanachama akinunua jezi original tu ambayo bei zao za laki tatu.. timu inajaa mahela..

Mpira wa africa tofauti na ulaya. Sababu wanachama ni maskini hawawezi kumudu gharama za kuendesha klabu
Hafu hao hao wanachama hohehae Timu ikifanya vibaya wanataka mocha afukuzwe, tunaangalia mpira wa Ulaya lakini hatujifunzi wakati mwingine mnahitaji kuvumilia mjenge Timu, we mnasajiri Timu nzima kila msimu mnategemea mtafanikiwa vipi hapo?
 
Shida sio uongozi shida ni mzamini kqpora majukumu ya uongozi ulio chaguliwa na wanachama.
 
Kuna siku niliuliza humu.
Gsm ni nani pale yanga.
Mfadhili,msaidizi,au muwekezaji.watu hawakunielewa.
Inafikia hatua Gsm anakaa na mikataba ya wachezaji.
Analoongea Gsm ndo hilo hilo.
wakiambiwa wawape timu Gsm kama Simba walichofanya wanakimbilia kusema wao ni timu ya wananchi.
Timu yao haiwezi kumilikiwa na MTU mmoja.sasa unajiuliza Gsm anavyotoa hela zake unadhani anasaidia,ana fadhili au anawekeza?hela zake zitarudi vipi?
Mkuu, ndiyo yeye tu wanae mtegemea, sasa wakimfukuza watapata wapi mwingine? Kila mdhamini hataki kuweka pesa zake kwenye ako kadimbwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…