TANZIA Mchekeshaji Jumanne Alela maarufu kama "Mzee Matata" wa Mizengwe afariki dunia

Poleni ndugu , jamaa na marafiki.

Mizengwe kipindi changu hicho no kukosa ITV Jumapili 21:05 - 21:30.
 
R.I.P Kwake japo alionekana ni Mdhaifu ( Mgonjwa ) Kitambo sana tu hata kwa Kumtizama Runingani.
 
Mara ya mwisho kuangalia mizengwe wiki kama 2 hivi waliyoigiza kuhusu mke kutaka kumpa mme talaka na mme kudai mgawanyo wa mali marehemu akiwa mwenyekiti wa mtaa hali yake ya kiafya haikuwa nzuri alikuwa kaisha na kuzeeka sana mpk nikawaza hili lililomtokea

Siku zake zimetimia Bwana awafariji familia
 
Naam, hata mimi niliiona hiyo, japo sikufikiria kufa ila nilijisemea mzee wangu amedhoofika sijui Masigara wanayovuta!!!
 
Pumzika kwa amani mzee wetu. Alikuwa na style ya kipekee haifanani na comedian yeyote tz, nakumbuka ile shoe shiner wa pita usemwe
 
Wachaga wanaofia Dar, ni kama asilimia mbili tu, huzikwa Dar, wengi husafirishwa kwenda kuzikwa kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…