Mchepuko anachanganya mapenzi na pesa, nilichomfanyia nadhani kapata funzo

Sister kumbuka kila Mara nasema nna mpango wa kumuoa, Sema tatizo tabia zake kujirekebisha Ni Changamoto.

Nnakaa na mtu,
ugomvi kidg tu anatishia Kama vipi tuachane, mara wanaume wako wengi.

Kama Kuna siku nilimwachia elfu 5 na kila kit kilikuemo, kakasirika na kasema Kama Huna pesa za kunihudumia Sema wanaume wenzako wakusaidie.

Ile kauli iliniuma Sana mpk nikaja kuleta Uzi humu jf. Maana nikijiona Kama Niko na mtu Ila siku nikiwa siko vizur zinazuka kauli ngumu ngumu na za kukatisha tamaa.
 
Huyo binti ni aina ya watu wanaiishughulikia leo na wakisema kesho itajishughulikia yenyewe.
Nashauri DeepPond
Amuache binti wa watu aolewe tu.
Najua ataumia kuachika but akiolewa na akawa na life nzuri atashukuru.
Mimi binafsi nikiona ninampotezea muda binti huwa nasema wazi plz ukipata mtu olewa.
Niliwahi kumwambia mmoja hivyo tena kwa upendo ...lkn alinichukia sana hadi leo.
Sikujuta kwani nilifanya kitu sahihi hata kama aliumia but nafsi yangu ilikuwa huru na amani kwa kutomharibia mtu maisha yake kwa tamaa zangu
 
Kodi anamlipia ,kazi kamtafutia mengine nae ajipange
 
Kwa kauli hiyo ulikuwa muda sahihi wa kumwacha.
Tatizo lako ukikumbuka kidude chake unasahau kila kitu.
Plz amua achana na huyo binti
 
Pole sana changamoto kwenye mapenzi zipo. Ukiangalia pande zote mbili wote mna mapungufu yenu.
Sina experience sana na mambo ya michepuko ndio kwanza nasoma soma kwenye stori zako.

May be anabehave hivyo sababu anajua kabisa hapo hakuna ndoa ila inabidi uishi nae kama alivyo. Mwisho wa siku yeye ndio ataamua abadilike tabia umuoe, au aendelee kupoteza muda huku jua linazama.
 
Du...kweli ulikomaa!!
 
Mkuu,
Ujue kina vitu vinakatisha sn tamaa,
Sikufichi Kuna siku Hadi chozi lilinitoka
Nilikua hospital uncle wangu aliumwa,

MamaJ akiwa mkoani akaniomba nimtumie laki 1 apate nauli ya kurudi dar
Nikamwambia niko hospitali ntakutumia nkirud dukan, akasema sawa.

Kweli nmerud dukn kuchukua Ela, gafla nikapigiwa Simu Hali ya uncle ni mbaya nigeuze. Kufika panahitajika dawa haraka za elfu 70 na mfukoni nna laki TU.

Ikbd kusema nna 50, 20 mnikopeshe kweli wakakubali. Elfu 50 ilobaki nikaenda mtumia mamaJ kwa wakala apate nauli ya Basi.

Cha ajabu hakusema Kama pesa kapata,
Na ALIPOFIKA nikamuuliza vp mbn ukunifahamisha km pesa umepata.

Akajibu kua Kwanza pesa yenyewe nmetuma pungufu, afu nmetuma nje ya Muda. Kwahyo hakuona umuhimu wa kushukuru.

Nilivolalamika Sana kua nmeacha mgonjwa kwa ajili yake,
Akasema Kama naona nmetuma pesa nyng sn mpk nampigia kelele anaweza KUFANYA mpango anirudishie hiko ki elfu 50 changu.

Nliumia Sana mpk chozi lilinitoka,
Nikawaza what if wangegoma kutoa zile dawa na anko akafariki, nafsi ingenisuta vipi.

NI VINGI SANA VYA KUUMIZA MKUU[emoji26]
 
Kodi anamlipia ,kazi kamtafutia mengine nae ajipange
Ndio shida ya sisi wanawake vitu vidogo vinatutoa utu, kodi unaweza kuta ni 150k au 200k. Ambayo kwa kazi yake angejitafutia nyumba affordable akaishi na kulipa kodi mwenyewe.

Mwisho wa siku pia tusimlaumu DP sana sababu anadeserve mtu miaka nenda rudi unashindwa kujiongeza yeye ana kazi kila siku anapewa hela ya kula,mshahara wake anapeleka wapi??

Ndio maana hata DP anamchukulia poa, kumbuka kuna mchepuko ni fundi cherehani tuu ila kajiongeza mpaka huwa anasifiwa humu pamoja na kwamba hatoi mzigo sana ila kashasaidiwa mambo ya maana mengi.
 
Kodi pale anapokaa nalipa 120,000 kila mwezi
 
Kwa komenti ya dadangu Dejane
Nimegundua mwansmke ni mtu asiyeona mbali...samahanini kwa kauli hiyo.
Kulipiwa kodi ndio uone umefika?
Huyo dada alipaswa ajipange mapema na awe amekuwa na mtaji wa maana ukiangalia anapewa aftatu za meza na kodi ili ajikomboe kwenye utumwa huu wa ngono usiokuwa na future.
Zinakuja siku hataweza tena kukata viuno ili aachiwe kodi ya meza.


Wanawake wafungue macho waone mail nyingi mbeleni
 
Yah! Khs fundi cherehanj,Una kumbukumbu nzur sn.
Yule fundi cherehanj anafanya maendeleo mpk mwnyw najistukia kila nikienda kwake kaboresha.

Nalazimika kumsapoti asijiskie vby maana mwnyw naona aibu anavojitoa kufanya maendeleo na haniombi Wala kunisubiri.

Sasa mamaJ Hana wazo lolote la maendeleo,kila ikifika ijumaa TU anawaza leo Bata wapi.

Hapa kusingekua huu ugomvi
Leo ni ijumaa najua lazima angeshaniuliza habar za kitimoto na bia wapi usiku wa leo.
 
Mwanamke akiwa na character hizi mbili anakuwa mbaya na hatari zaidi ya nyoka.

Mosi, UKOSEFU WA SHUKRANI..yaani hata umetendee mema milioni ukifanya baya moja anahesabu kuwa huna jema ulilomfanyia zaidi ya lile baya moja.

Pili, KUKITHIRISHA LAANA (Matusi) na kauli mbovu . Mwanamke asiyejua kuuzuia ulimi wake mbele ya mwenza wake ni mbaya sana zaidi ya nyoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…