KERO Mchezaji wa Simba anatumia jina langu, ananiambia nikashtaki popote

KERO Mchezaji wa Simba anatumia jina langu, ananiambia nikashtaki popote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Aliyekushauri kakushauri vibaya sana kulileta huku.Kwa kuwa umesema nyinyi ni marafiki wa kifamilia,rudi nyuma mtatue kifamilia.Hii ni aibu tu.Vyeti vyako kama unavyo we pambana navyo.Tukiwa chuo hapo Dodoma kuna siku nilikatisha makaburini kule kizota,tukaona kaburi lina jina la Rafiki yetu mmoja,jina full majina matatu.Tukamshtua tukacheka basi yakaisha.Majina duniani kufanana ni kawaida.Asingekuwa maarufu hapo Kariakoo wala usingejali.Hoja ni kuacha kutumia jina ama kukutoa chochote kitu?
Mkuu hapo huyo mchezaji ameshaharibiwa baadhi ya vitu, hebu chukulia tu Yanga wakianza kutafuta majina halisi ya huyo Duchu na wakaitafuta Ile timu waliyomfungia jina asicheze huoni hapo Kuna kesi ya vyeti feki na udanganyifu katika kazi?? Japo wote wawili watapata adhabu hii haikwepeki
 
Inabidi simba ipokonywe points kwa kumchezesha mchezaji aliyefungiwa.
 
Ligi ya Tz mchezaji anaweza cheza hata akiwa na umri wa 40. Uongo ni mwingi sana Kwa wachezaji ktk umri.
Sio tu TZ mkuu kiufupi ni wachezaji wa kiafrika tunadanganya sana umri Yani kama ukianza kizichunguza hizi timu za UNDER ngapi ngapi sijui Yani utakuta Kuna vijeba vina umri wa Zimbwe na shomari lakini utakuta unaambia ni under17
 
Unapata athari zipi mtu mwingine kutumia jina lako?

Mpaka umepata TIN maana yake NIDA unayo na inakubalika. Umekosa kazi kisa jina lako linafanana na la mtu mwingine?
Umekosa hati ya kusafiria?
Umeshtakiwa kwa kosa la huyo mchezaji bila wewe kulifanya?

Kipi unaathirika nacho hasa.
Mkuu unatetea udanganyifu??? Yani jina la Mbeya City na jina la Simba Fc yawe tofauti alafu unatetea aiseeeee sisi kama yanga tayari huyu mdau Leo anakutana na wakili wa Yanga hii kesi inaanza Leo Leo kabla mahakama hazijafungwa maana Leo ijumaa😀😀
 
😂😂😂....
 
We jamaa ndo utakuwa na shida, kama una akili ungelifuta huu uzi kabisa. Utaishia ndani. Alaf jamaa atapigwa pemalti tu ataachwa.

Wewe ulikosa pakubwa kuruhusu afanye kulitumia in the first place. Na kutangaza hivi ndo umejinyonga mwenyewe
 
Hapa inshu sio majina...
Ila n dharau!!

Mwanaume anaweza pigana kisa 200, hata kama bank Kuna milion 50.
Kuna muda mtu anaamua kupigana sio kwasabb ya kupata au kukosa ila kwasabb ya heshima yake imetikiswa!!
Hii huja automatic bila kufikiria hatari iliyoko mbele
 
Back
Top Bottom