KERO Mchezaji wa Simba anatumia jina langu, ananiambia nikashtaki popote

KERO Mchezaji wa Simba anatumia jina langu, ananiambia nikashtaki popote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Naitwa David Frank Kameta, baada ya kupata wakati mgumu muda mrefu ikiwepo kusalitiwa na mtu ambaye nilimuamini, sasa naona ni bora Dunia ijue kinachoendelea. Hapa nazungumzia usaliti wa rafiki yangu Emmanuel Robert Kakoti jina lake maarufu wengi mnalijua, kwa sasa ni mchezaji maarufu katika klabu kubwa katika Ligi Kuu Bara.

Alichukua jina langu kwa makubaliano maalum kuwa atalitumia muda mfupi lakini amenigeuka na kuendelea kulitumia kwa miaka mingi, hataki kurejea katika jina lake halisi huku akinisababishia hasara nyingi na mzozo katika familia yangu.

Stori yetu ipo hivi…
Tuliishi pamoja Mbeya, tulisoma wote ingawa alikuwa mbele yangu darasani, mimi umri wangu ni miaka 32 (nilizaliwa 1994), yeye mwenzangu alianza kucheza mpira tukiwa wadogo, hayo hayakuwa mambo yangu.

Mwaka 2017 au 2018 (sikumbuki vizuri), Emmanuel akiwa timu ya Mbeya City alionyesha utovu wa nidhamu, uongozi ukamfungia usajili pamoja na kufungiwa kutumia majina yake yote halisi kwenye soka. Hiyo ilimfanya aonekane kama amefutwa kwenye Ulimwengu wa soka.

View attachment 3657241
Kikosi cha Mbeya City cha Msimu wa 2017/2018 ambacho Emmanuel Robert Kakoti alikuwepo (jina la nne kutoka juu).​

Kuna siku ilikuwa deadline ya usajili, Emmanuel aliniomba, "Mwanangu, usajili unafungwa leo na nimekosa nafasi, naomba nisaidie cheti chako cha kuzaliwa nitumie kwenda Mbeya Kwanza. Nikianza tu kucheza, nitabadilisha jina kwenye leseni na kurudisha jina langu halisi."

Sababu ya urafiki na huruma, nilimpa cheti changu, akafanikiwa kusajiliwa Mbeya Kwanza kwa jina langu la David Frank Kameta. Aliendelea na maisha yake ya soka katika timu ya Lipuli ya Iringa, lakini ilikuwa ni kinyume na ahadi yetu, hakubadilisha jina hilo. Nilimsisitiza kuwa anatakiwa kurejea katika jina lake halisi lakini aligoma.

Aliposajiliwa katika timu yake ya sasa ya Kariakoo, akaanza kunikwepa, akawa ananipa majibu ya mkato. Huku nyuma mimi nikaingia katika mgogoro wa kifamilia wakiniambia nimeuza jina.

View attachment 3657258
Document yangu ya TRA

View attachment 3657260
Cheti changu cha kuzaliwa​

Baada ya msiba wa mzee wangu, familia ilikaa kikao na kunisema sana, nilipompigia simu Emmanuel mbele ya familia hakupokea. Nilituma ujumbe kumtaka ache kutumia jina langu, alinijibu kwa dharau: "Fata sheria yoyote, mimi siachi kulitumia."

Nilipofuatilia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Pasipoti, nilikuta mfumo unaonyesha uwepo wa watu waliofungamana japokuwa yeye aliandika amezaliwa Mwaka 2000 au 2001.

Hali hiyo imeniletea athari kubwa sana kiakili na kisheria kwani jamii inaamini niliuza utambulisho wangu na kuna fursa kadhaa nimezikosa kwa sababu yake, nimeamua kuandika hapa baada ya kuona uungwana wangu umeniponza na mtu ananiletea dharau.


BWEGE MMOJA KILAZA NWENYE NJAA. SI AMESHAKUAMBIA FUATA SHERIA. FUATA SASA. UNALETA HUKU KULIA LIA KWANINI? HUNA AKILI ALIKUZIDI AKILI. ACHA AFAIDI WEWE KILAZA SANA. JINA LAKO KWA SASA UNAITWA NANI?
 
Tafuta wakili,?? Atakupa mwongoz upate haki yako! Acha kupost personal info zako mhimu kwa kila mtu kitakulamba.
Anapoteza muda,itakula kwakwe, yeye anasema amezaliwa2001 na jamaa kaweka 2000 ,pia majina kufanana kupo tu,akipeleka kesi mahakamani atapigwa tatu bila huyu mjinga.

Wivu na chuki vinamsumbua,anayecheza huko siyo jina na mtu,hata akipewa jina lake atalufanyia nini!?
 
Hapa it seems kulikuwa na mutual agreement ila inaonekana huyo mwamba kakiuka makubaliano so ndo inabidi jamaa ajaribu kumwaga mboga.
True ,ilitakiwa Duchu angekubaliana naye kwamba natumia vyeti vyako nakupa labda milio 20 ila nakupa 5 kwa awamu nne kisha tusijuane....ila ila ya kumtoa toa vilaki laki lazima wafike hapo.
 
Siyo mtaalamunsana wa maswala ya Sheria za soka, ila hii inaweza kumletea Duchu shida kwenye soka lake
Shida gn atapata duchu?,

Hao ni watu wawili tofauti.
Huyo kameta duchu ni mcheza soka timu ya simba.
Na huyo kameta mwingine ni fundi viatu..

Hapo shida sio majina bali ni professional je zinafanana au tofauti?
 
Kivipi iwe identity theft wakati walikubaliana?
Kwa mujibu wa mtoa post.
Kosa lipo wp?mleta mada njaa imemtoa mafichoni.
Kukubaliana hakuondoi identity theft.

Hutakiwi kukubaliana na mtu atumie jina lako.

Hata mkikubaliana wote mmefanya fraud hapo katika kesi ya identity theft.

Yani hiyo identity si mali yako kwamba unaweza kumuazima mtu kama suruali.

Hapo kuna kosa la jinai limetendeka. Kumpa mtu hizo documents atumie kama zake wakati si zake ni kesi kwa wote wawili.

Umeelewa?
 
Back
Top Bottom