SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Nakumbuka mwanzoni mwa msimu huu nilipongeza usajili mzuri waliofanya Simba ila nikatoa angalizo moja kuwa wachezaji wa Simba wapigwe marufuku kuzoeana na wachezaji wa Yanga nje ya uwanja.
Naelewa hawa wachezaji wana maisha nje ya uwanja na naelewa pia wengine wana historia zinazoingiliana kwa hiyo mahusiano nje ya uwanja hayaepukiki, ila ni vizuri tukajua uhalisia wa mpira wetu na tuambiane ukweli.
Nakumbuka kushangaa Aubin Kramo kuendeleza ukaribu na kina Yao na Pacome kiasi kwamba alikuwa anaenda hadi airport kumpokea Pacome. Mwisho wa siku wote tunajua story yake.
Huyu Ahoua naye siku zake pale Simba zinahesabika. Nasikia naye anaendeleza ukaribu na wachezaji hao hao wa Yanga. Nadhani viongozi wa Simba hawakuona haja ya kumpa mwongozo ila athari zake tunaziona sasa. Kocha Fadlu naye akiendeleza kumkumbatia ataondoka yeye kwanza halafu huyo Ahoua atamfuata.
Ifike wakati tuambiane ukweli wanasimba. Kuwa na mchezaji kama huyu uwanjani ni kujikaba wenyewe. Ni kuwapa pressure mabeki wako kwa dakika 90 maana mnakuwa siyo tishio kule mbele. Mwisho wa siku kina Ateba wanaonekana butu kumbe hawalishwi nafasi zozote za maana.
NYONGEZA: Pamoja na kwamba tunasema kocha asiingiliwe ila naye ni binadamu. Anaweza kuleta chuki binafsi katika kazi ikamfanya aharibu timu kwa kuwapiga pini wachezaji au kuwabeba wasiostahili. Yuko wapi Karabaka mchezaji aliyethibitisha ana bahati ya kufunga? Mbona Awesu hapangwi katika mechi anazoonekana kabisa anaweza kusaidia?