Mchezo mchafu unaofanywa na benki kuwapora wateja pesa zao

Jambo kama Hilo limenitokea NMB hivi majuzi

Mwezi wa nne mwaka huu niliangalia salio nikakuta Nina akiba Kama ya 200k, na ushee

Mwezi huu wa tano mwanzoni kabisa nilienda kuchomoa mpunga kutoa 190k ikagoma salio halitoshi, nikajaribu 180k nikaambiwa pia salio halitoshi, nikajaribu 175k pia nikaambiwa salio halitoshi, daaa ndio nikajaribu 170k ndio ikafanikiwa kutoka


Sasa nikajiuliza iweje uwe na salio la 200k halafu hutoe 175k muamala usifanikiwe?


Ina maana kuna kiasi kingine Cha fedha kimepungua kwenye salio la mwanzo bila Mimi mteja kutambua

Tuweni makini kuna mfumo wa upigaji kwenye haya mabenki.
 
Ifike mahali bank za hivyo zitajwe waziwazi. Mfano mimi kwenye bank ya CRDB tarehe 23 April nilifanya muamala mara mbili lakini nilikuta makato ya pesa zaidi ya mara 10. CRDB kwa sasa imekuwa ni bank ya hovyo kabisa.
CRDB ya sasa ni Hovyo kuliko Hovyo yenyewe, wana ujinga mwingi sanaa!
 
Mkuu haka kamchezo wafanyakazi wenu wanakafanya sana, binafsi nimeshawahi toa hela kwenye ATM NMB hela haikutoka nikasubiri masaa 24 haikurudi nikajanza form tena pale muhimbili branch hela ikarudishwa imekatwa vibaya sasa nikajiuliza hela niliyotoa haijatoka hata kuirudisha kwenye account inakatwa tene, pili nilinunua umeme sikupata token nikajaza form nirudishiwe hela yangu hadi kesho hela haojarudi.
Kuna mauchafu mengi sana humo kwenye mabenki yakutokuwa waaminifu kwa wateja wao
 
Na Ndio maana wahindi hawaweki pesa kwy bank za wabongo. Wanaweka Exim Bank
 
Tuwe tunazianika majina hizi bank sio tunazungumzia kwa usiri kamavile jiwe yupo.
 
Nimeitelekeza akaunt yangu ya Stanchat. Wana makato haoo balaa. Nadhan ni malimbikizo ya hela ya kutunzia akaunt
Dah... Sasa mimi kuitelekeza ni ngumu maana naitumia kwa ajili ya mambo yangu ya kimtandao
 
Bank kunatokea human errors ndio maana kukawa kuna kurivezi kwenye system kwa sababu inajulikana wanaofanya kazi ni binaadam wanaweza wakakosea.

Kuna matukio ya wateja kupiga hela za bank pia. Mtu anataka kuweka elfu 50 bahati mbaya cashier anaweka laki 5 mteja akipata sms dakika hiohio anaenda kuzitoa. Ni wachache sana wanarudi Bank kusema mmekosea mmeniwekea pesa zaidi.

Ila kuna staff ni wadanganyifu wa makusudi.

Ukiwa hujui system ya bank na vp wakati mwengine staff pia kuna makosa wanafanya basi utaona kama unaibiwa. Uzuri system inaonesha kila kitu So Sio rahisi pesa yako ikapotea bank
 
Sister wangu alifiwa na mumewe mwaka alikua mhasibu kwenye wizara flan,same alipopata usimamizi wa mirathi alikutana na hali kama hiyo,stanbic hakukua na pesa,crdb kuna deni ambalo mkewe alitambui,nmb kuna laki 4!nchi ngumu sana hii!
Bank kuna dual control system. Sio rahisi staff mmoja akafanya wizi pekeyake mara nyingi laziim kuwe na ushirikiano na staff wengine which is ni ngumu.

Ukikuta kiasi cha pesa kwenye akaunti ya bank aloiacha marehemu basi ndio hio hio. Kwani bank statements si zipo mnakwama wapi kufuatilia?
 
Hili la Marehemu kupigwa hela zao linaweza kuwa kweli,nakumbuka Marehemu kaka yangu alipofariki,familia ilifuatilia process zote na zilivyo ndefu sasa mara mahakamani mara wapi sijui,wanakuja kwenda bank holaa,hakuna kitu kabisa,account zake hazikuwahi kuishiwa kabisa hapo kabla!!kwa huu uzi naanza kuhisi pengine kuna wajanja walichungulia fursa.
 
Inaonesha elimu yahitajika sana. Banki si rahisi kukuibia maana statement huwa zipo
 
Huyu Mashuke ni sawa sawa na Virgo?
August 23 hadi September 22?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata hiyo 2m huenda sio kweli.
Kama Bank statement inaandikwa kwa computer itakosewje?
 
Aisee.. Kuna account yangu bank ya standard chartered,
Juzi nmeweka 190,000 kwa njia ya m pesa cha jabu hiyo bank wakafyeka 22,000 nzima. Mpaka sasa hivi nawaza wamekata kwa jili ya nini sipati jibu.

Absa
Standrd chartered
Kama unataka maendeleo hapa unapotea maana


Mimi muanga wa makato hapo mwanzo wa mwezi ni makato na benki nyengine angalia hayo makato.sasa kwa hali hii utaweka pesa kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…