Mkuu nashukuru kwa kunielewa,mimi nilibahatika kufanya kazi benki kidogo ila sikukaa front dest/kirishani najua sana operations za benki behind zinafanyikaje..Kable ya hapo nikiwa chuoni/mtaani niliamini kabisa benki wanaiba pesa kama watu wengi wanavyoamini hapa,ila baada ya kupata uzoefu kidogo nimegundua hakuna hata senti ya mteja ianweza potea benki kwa makusudi,labda iwe ni fraud na ikiwa hivyo mteja hatoathirika.
Kuna changamoto za ndani ya benki ambazo wateja wengi hawazijui(Kiuhalisia hawapaswi kujua sababu haiwahusu),lakini kusema tu generally kwamba benki ni wezi wanaiba sio sawa hata kidogo,.
Bank Teller hawezi kuiba pesa kiasi ambacho anajua kabisa mshahara wake hauwezi kulipa iwapo mteja akija kudai,ndio maana unakuta wale sio waaminifu wanaiba elfu 10,20,30 au akizidi sana 50.Teller hawezi iba eti laki1,2,2,5 au 1M.Sabau anajua hiyo amount ni kubwa ni lazima ajulikane na pia lazima mteja aje kudai,na itapelekea hadi yeye kufukuzwa kazi.Kinachotokea ni makosa ya kibinaadamu tu,ila mteja sababu hajui anasema benki ni wezi (Ofcouse ni haki yao kulalamika sababu poesa ni zao).
Pia wanashundwa kujua kwamba hayo makosa yanatokea kote kote,..Kuna mteja alishwahi zidishiwa pesa akawekewa 5M badala ya laki 5,sababu alipata msg alienda branch nyingine faster akatoa 3M,yule teller alifukuzwa kazi kwa uzembe,haya makosa yanatokea pande zote ila wateja sababu ni wengi basi wakilalamika inaonekana benki ni wezi kumbe ni makosa ya kibinadamu tu.