Kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za FIFA Serikali hazipaswi kuingilia mambo ya soka au kuyaendesha mashirikisho ya mpira wa miguu ya nchi husika.
Hiyo ina maana kwamba hapa kwetu Tanzania, Serikali hairuhusiwi kuingilia maamuzi ya TFF.
TFF walipaswa kuikatalia Serikali iliposema mchezo wa Yanga na Simba usogezwe mbele kwa masaa 2 maana kanuni na taratibu haziruhusu.
Kutokana na hili sakata, Yanga wanapaswa kupewa point 3 na magoli 3 sababu wao wapo sahihi kikanuni. Nitawashangaa sana Yanga kama watakubali kurudia mechi hiyo. Nawashauri Yanga, ikiwa TFF itakataa kuwasikiliza kuhusu kupewa point 3 basi waiandikie FIFA barua ya malalamiko halafu tuone moto wake.
Yanga msikubali kuchezeshwa hii ngoma ya TFF na Serikali, komaeni mpewe points zenu 3 na magoli 3 sababu wenye makosa siyo ninyi, ni hao TFF na Serikali. Ninyi mlifuata kanuni na taratibu kama zinavyosema.
Kateni rufaa, andikeni barua FIFA watu waadabishwe, heshima irudi. Hao TFF wamejisahau sana hao akina Wallace Karia na wenzake.
Yanga chomeni utambi FIFA, hii ni nafasi yenu adimu ya kurudisha heshima ya soka la bongo.