safi upo sahihi, mimi ndo nipo huku mirerani, hili walilificha ili wakauze nje, na wangepata hela nyingi zaidi ya lile ka kwanza, sema tu muingiliano uliotokea huko chini ndo siri ikafichuka na serikali kuingilia kati. Na pia muelewe laizer sio kama yeye ndo anapata hela kubwa kuliko wote ni hapana,, laizer yeye ni mwenye mgodi, ila kuna wahudumiaji mgodi na hao huwa wana percent kubwa zaidi ya lizer,, unaweza kuta kwenye ile bilioni saba yeye laizer akaambulia tatu tu, na nne ikaenda kwa wahudumiaji,, ila hili jiwe la sasa lina mgogoro na watu wanne, ni stori ndefu nikielezea hapa, na sivuri kiusalama.