Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
ACT Wazalendo hatutaki maneno bila vitendo, kwa kuwa mvua hizi zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa wananchi, tunaitaka Serikali ichukue hatua zifuatazo:
1. Iunde Timu Maalumu ya Kitaifa ya Kukabiliana na Majanga itakayohusisha TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu na TMA, kwa ajili ya kuratibu na kufuatilia maandalizi ya wizara, mikoa, wilaya na mamlaka za serikali za mitaa.
2. Iongeze fedha kwa NFRA ili kununua na kuhifadhi chakula cha kutosha kwa ajili ya kukabiliana na dharura na kusaidia maeneo yatakayoathirika, huku ikipunguza matumizi yasiyo ya lazima na ya anasa ili kuelekeza rasilimali kwenye maandalizi ya janga.
3. Mikoa na wilaya zitambue na kutangaza maeneo hatarishi, ziandae maeneo salama ya kuwahamishia wananchi, na kutoa elimu ya tahadhari kwa wananchi, wakulima, wafugaji na wavuvi kwa kushirikiana na vyombo vya habari na asasi za kiraia.
4. Iharakishe ujenzi na ukarabati wa miundombinu muhimu, ikiwemo madaraja, makaravati na barabara, pamoja na kusafisha na kupanua mitaro na njia za maji ili kuzuia mafuriko. Miradi iliyo hatarini ikamilishwe haraka au ifikie kiwango salama kabla ya mvua kuanza.
5. Ichukue hatua maalumu kwenye maeneo ya migodi: shughuli za uchimbaji zisitishe kwa muda katika maeneo hatarishi, wamiliki wa migodi waimarishe kingo na watengeneze njia salama za maji ili kuzuia mafuriko na ajali.
6. Serikali ifanye maandalizi ya kimatibabu (afya) na kiuokoaji kwa kuongeza wataalamu, dawa na vifaa tiba, iandae kambi za dharura, na kuimarisha uwezo wa uokoaji kwa kutumia helikopta, boti, jaketi za kujiokoa na zana nyingine, kwa kushirikisha vyombo vya ulinzi na usalama.
7. Viongozi wa ngazi zote wawe kazini kikamilifu, hasa katika maeneo hatarishi, badala ya kusubiri majanga yatokee. Serikali pia itoe taarifa na elimu endelevu kwa umma kuhusu tahadhari na hatua za kuchukua kabla na wakati wa mvua.