Mchumba wangu ananishirikisha katika kila kitu cha maendeleo anachofanya

Akili huna wewe chamsingi akaanae chini waongee wataelewana ila unavyosema waachane huo sio ushaur na unaweza kupata mtukicheche wakati mtu sahihi anae
Kiukweli umemtukana bure jamaa Angalia kiasi cha Likes alizopata ndo unataelewa maana yake imegota wapi pole sana
 
Mshaurini huyu jamani...

MCHUMBA WANGU ANANISHIRIKISHA KATIKA KILA KITU CHA MAENDELEO ANACHOFANYA!

Mimi ni binti wa miaka 28, sijaolewa ila nina mchumba ambaye yeye ana miaka 30, nampenda sana na yeye anaonyesha kunipenda kwakuwa kashanitambulisha mpaka kwao na kwetu pia nimeshamtambulisha. Tatizo ni kuwa mpenzi wangu huwa ni muwazi sana, ananishirikisha katika kila kitu chake cha maendeleo anachokifanya na mara nyingi anakuwa anataka mawazo yangu, akitaka kununua kiwanja, kujenga, akitaka kitu chochote hata kama ni mapazia anataka tufanye pamoja.

Mimi nafanya kazi na yeye pia anafanya kazi, haniombi pesa na wala hajawahi lakini tatizo ni kuwa kwakuwa ananishirikisha katika mambo yake basi nashindwa kumuomba pesa kubwa kubwa kwaajili ya kufanya mambo yangu kwani kila hela yake najua imeenda wapi? Kwa mfano labda nataka laki mbili, ninataka kununua kitu changu labda kutoka na marafiki, nikimuambia pesa ananiambia hana si tumenunulia kitu flani, ukiangalia kweli alinunua hicho kitui na alinishirikisha hivyo naona aibu hata kumkasirikia kwani kinakuwa cha maendeleo na najua pesa yake yote.

Naumia sana kwani mimi kama msichana nahitaji kudekezwa na kufanyiwa suprize za zawadi kama marafiki zangu ambao wanaweza kufanyiwa birthday na wapenzi wao, kutolewa out, kununuliwa nguo na zawadi. Mimi nikihitaji kitu inabidi nimuambie mapema kabla ya mshahara ili aniweke kwenye bajeti na sanasana atakupa elfu hamsini hata laki hakupi kwani anakuwa anafanya vitu vingi vya maendeleo ambavyo ananiomba ushauri na ukiangalia anakuwa kweli hana kwani hata yeye hafanyi hizo starehe.

Kinachoniuma zaidi ni kuwa hawezi kufanya maamuzi yake mwenyewe kama mwanaume ni lazima aniambie na mara nyingi hupenda kufuata ushauri wangu na si wake. Kunipenda kweli ananipenda lakini nina wasiwasi je tukioana itakuaje kwani mara nyingi anasema tukioana itakua vizuri kama tukishirikiana kwenye mambo ya familia eti mshahara wangu nao tufanyie mambo ya maendeleo wakati yeye kama mwanaume anatakiwa kufanya kila kitu, niko njia panda nawaza je huyu ni mtu sahihi kwangu au nifanyeje?
Kabla haujafikiria kama huyu ni mume sahihi ilikuwa muhimu zaidi kujiuliza kama wewe NI mke sahihi???

Sent from my Z9 using JamiiForums mobile app
 
Hapa kuna mawili, huenda jamaa ndo lifestyle yake kwamba ameamua kufocus kwenye mambo ya msingi au labda ameamua kujificha kwenye hicho kivuli cha tunafanya maendeleo ili kuzuia mizinga.

Lakini na we binti kama jamaa haugusi mshahara wako kwanini usitumie hela yako kujitoa out mfurahie maisha?

We mwenyewe hela yako ni yako pekeako na unaionea uchungu halafu unaitaka hela ya jamaa na unajua anachoifanyia
 
Dada achana na huyo hajui nn mwanamke anataka.
kujenga ajenge ila mahitaji yako atimize.

Piga chini
 
Nasikitika bado hujitambui, mume anashughulikia kesho yenu wewe unawaza kula na kunya tu.
 
Hapo wadada ndo mnapofeli kumchagua mchumba sahihi, unapenda malimbukeni wakuchezee, wakupe suprise, wakutoe out na mengine. Hivi kwa umri wako bado unawaza suprise, umepata mtu anayeona mbele anakushirikisha kwa kila kitu wewe unaona sio sahihi duuuu, zingatia umri wako pia.

Kwa ushauri wangu huyu ni mwanaume sahihi kwako anayependa kukusiliza kwa ushauri na akatekeleza ila wewe sioni kama ni mke sahihi sana kama bado unadought action zake.
28yrs unajua hata kifua konasujudi lakini bafo anawaza ujinga ujinga tu
 
Hapo hakuna mwanamke vipo viatu tu na magauni
 
Halafu utakuta wanawake wenzie wanamjaza ujinga
Huyo rafiki yako ni bomu linalosubiri liingizwe kwenye ndoa likalipukie huko!

Sasa Kama ana kazi si atumie pesa zake kwa matumizi yake kwani lazima atumie hzo za jamaa zinazofanya Mambo ya kudumu...
Huyo binti anashida sehemu mtu anakushirikisha vitu vya maendeleo hupendi[emoji849][emoji849][emoji849]!!!!!!

Kuna viumbe sijui ua vinataka nn ili kuridhika....... AJABUUUU!
Mwanamke wa aina hii hata kumsalimia hafai
 
Ukiona unaanza kumwelewa mwanamke ujue siku zako za kufa zinakaribia
 
Mshaurini huyu jamani...

MCHUMBA WANGU ANANISHIRIKISHA KATIKA KILA KITU CHA MAENDELEO ANACHOFANYA!

Mimi ni binti wa miaka 28, sijaolewa ila nina mchumba ambaye yeye ana miaka 30, nampenda sana na yeye anaonyesha kunipenda kwakuwa kashanitambulisha mpaka kwao na kwetu pia nimeshamtambulisha. Tatizo ni kuwa mpenzi wangu huwa ni muwazi sana, ananishirikisha katika kila kitu chake cha maendeleo anachokifanya na mara nyingi anakuwa anataka mawazo yangu, akitaka kununua kiwanja, kujenga, akitaka kitu chochote hata kama ni mapazia anataka tufanye pamoja.

Mimi nafanya kazi na yeye pia anafanya kazi, haniombi pesa na wala hajawahi lakini tatizo ni kuwa kwakuwa ananishirikisha katika mambo yake basi nashindwa kumuomba pesa kubwa kubwa kwaajili ya kufanya mambo yangu kwani kila hela yake najua imeenda wapi? Kwa mfano labda nataka laki mbili, ninataka kununua kitu changu labda kutoka na marafiki, nikimuambia pesa ananiambia hana si tumenunulia kitu flani, ukiangalia kweli alinunua hicho kitui na alinishirikisha hivyo naona aibu hata kumkasirikia kwani kinakuwa cha maendeleo na najua pesa yake yote.

Naumia sana kwani mimi kama msichana nahitaji kudekezwa na kufanyiwa suprize za zawadi kama marafiki zangu ambao wanaweza kufanyiwa birthday na wapenzi wao, kutolewa out, kununuliwa nguo na zawadi. Mimi nikihitaji kitu inabidi nimuambie mapema kabla ya mshahara ili aniweke kwenye bajeti na sanasana atakupa elfu hamsini hata laki hakupi kwani anakuwa anafanya vitu vingi vya maendeleo ambavyo ananiomba ushauri na ukiangalia anakuwa kweli hana kwani hata yeye hafanyi hizo starehe.

Kinachoniuma zaidi ni kuwa hawezi kufanya maamuzi yake mwenyewe kama mwanaume ni lazima aniambie na mara nyingi hupenda kufuata ushauri wangu na si wake. Kunipenda kweli ananipenda lakini nina wasiwasi je tukioana itakuaje kwani mara nyingi anasema tukioana itakua vizuri kama tukishirikiana kwenye mambo ya familia eti mshahara wangu nao tufanyie mambo ya maendeleo wakati yeye kama mwanaume anatakiwa kufanya kila kitu, niko njia panda nawaza je huyu ni mtu sahihi kwangu au nifanyeje?
Ukiona umeanza kumuelewa mwanamke jua unakaribia kufa...

By JF Member.
 
Mimi ningekuwa na mawasiliano na huyo mchumba wako ningemshauri akupige chini kwani wewe ni bomu litakalompasukia huko mbele ya safari, wewe stahili yako ni kupigwa miti na kuachwa hadi utakapotia akili.
 
Back
Top Bottom