Mchungaji wa Kanisa la Huduma ya Kristo lililopo Mtaa wa FFU, Kata ya Murieti, Steven Jacob Gumbo (35) ambaye iliripotiwa ametekwa na 'Watu Wasiojulikana' Mei 16, 2025 amezungumza na Wanahabri na kueleza kuwa Watu waliomchukua walijitambulisha kuwa ni Askari Polisi na wanamhitaji kwa ajili ya mahojiano
Amesema Watu hao walimchukua kwa nguvu huku wakimpiga, akapelekwa sehemu ambayo hakuifahamu na kuingizwa kwenye chumba kisha kuanza kumshambulia.
Ameongeza "Naomba nisiongee mengi, sababu ya kutekwa ni ishu za Mtandao. Walichukua maelezo, wakanipeleka porini West Kilimanjaro, wakachukua simu yangu na kunitaka nifute video zangu zote, wakazungumza vitu ambavyo siwezi kuvisema kwa sasa kisha wakanitelekeza hapo."