Mchungaji Anthony Lusekelo, aionya Serikali ya Rais Samia juu ya amani ya Tanzania

Nimemuelewa sana. Ana hoja nzito.
Samia aisikie sauti ya Mungu hiyo kupitia kwa Mzee wa Upako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata angeongea wakati anakata roho ujumbe huu unatosha
Tumeziba masikio🙉🙉,haiwezekani aanze kuikosoa serikali baada ya kuona serikali haimpi favour katika Mambo yake binafsi!
Mimi mwananchi wa kawaida siioni hiyo hatari anayoizungumzia mzee wa upako!

Mama SSH chapa kazi,wananchi tuko nyuma yako
 

1. Kwamba JPM na Corona? Unadhani JPM aliungwa mkono kwenye Corona na watanzania wote?



2. Msimamo wa JPM na Corona uliungwa mkono na wajinga na wanafiki. Hao ndiyo waliokuwa wapiga nyungu.



Watu wangapi akiwamo yeye walipoteza maisha kwenye ujinga wake huu na Corona?



3. Wangapi waliachana na ujinga wake hata kabla hajazikwa?

4. SSH hana support ya wajinga wale wale kwenye Corona kwa sababu ya kuwakumbatia watendaji wale wale hasa kwa wizara ya afya ili kuleta mtizamo tofauti. Hawaaminiki.



3. Kwamba watanzania hawakuumia na kupotea kwa Ben Sanane? Wangapi walijua tulikuwa na mtu anaitwa Ben na hata kuwa alipotea, kwenye media industry hii iliyokuwa suffocated kama iliyopo?
4. Kwani hujui kuwa watu wengi sana walifurahi mno kutokana na kifo cha JPM kiasi cha sherehe hata za kawaida tu kupigwa marufuku kuhofia kuadhimishwa kifo chake kwa kuserebuka?
5. Tofautisha nyie kina Sabaya na ndugu na jamaa wa akina Azory, Ben, Mawazo, Lissu na wote waliokumbana na ushetani usiovumilika wa JPM.



Nyie mliokuwa mkifanya naye ujambazi lazima mlie machozi ya damu. Si kawaacha yatima?



Hiiiiii bagosha!
 
Hii bagosha umekandamizia sana
 
Ana uhuru wa kusema na amesema sasa, sio lazima ukubaliane naye
 
Hamjifunzi tu kwa Mange, Chahali, Nyalandu, Gwajima, Kakobe, Lowassa na Kigogo?
Hamuwezi kutofautisha watu wenye misimamo ya kweli na wakosa fursa wenye gubu tu ?

Mzee wa upako atawashangaza baada ya mfupi tena.

Gurudumu lazima lizunguke kwenda mbele. Yeyote atakayesaidia kulizungusha kwenda mbele anakaribishwa. Yeyote atakayelizuia kwa wakati huo hata kama ni Mbowe atakuwa hafai.

Lowassa, Nyalandu, Mashinji, Nassari, Silinde nk walipokuwa wa muhimu tulifurahi kuwa nao kama ambavyo tulivyofurahi kutokuwa nao walipokuwa mizigo.

Mmoja asidhani kuwa ni wa muhimu siku zote na kwa kila hali.

Hapo ndipo walipo akina Mdee.

Mwana mpotevu alirudi kwa baba yake akapokelewa. Mwana mwema akachukia na kupotea jumla.

Vita hivi vinataka akili.

Mandela hakuwatosa kina Buthelezi. Kuna aliyekuwa msaliti kuliko hao?

Tupigane vita na akili kichwani. Tunahitaji watu. Magereza yatajazwa na watu na hapo ndipo uhuru kamili utakapokuja.
 
Hahaha mwamba umwkomaa naye kwelikweli
 
Ana uhuru wa kusema na amesema sasa, sio lazima ukubaliane
Mi sijamzuia kusema, kwani anaweza akasema na asisikike na aliowatarget kwasababu hawana muda wa kumsikiliza mtu aliyejikatia tamaa

Kipindi kile nchi inahitaji aseme yeye aliimba nyimbo za sifa kwa Magufuli,adhabu ya msaliti na mnafiki ni kifo Cha bila AMANI ya moyo wake.
 
Na vyama vya upinzani viache ugaidi na ukabila na upuuzi wa kushangilia vifo vya viongozi vinginevyo mtaishia kukesha kwenye mitandano kutema nyongo huku miaka ikiyoyoma
 
Wewe ndio una roho chafu. Ulikuwa mpiga dili ukabanwa sasa bado unatapatapa. Huna lolote wewe. Hakuna kama JPM huo ndio ukweli mchungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…