Mchungaji Anthony Lusekelo, aionya Serikali ya Rais Samia juu ya amani ya Tanzania

Mchungaji Anthony Lusekelo, aionya Serikali ya Rais Samia juu ya amani ya Tanzania

Mzee wa Libapa Likubwa ?.Enheee ! Libapa Likubwa,una maana gani.Au lile lichupa Likubwa la konyagi ! Ngoja Huyo Mzee wa U*p*ko, a.k.a.Likonyagi Likubwa aione hii clip yako,ndo utaipata Fresh
 
nikuridishe kwenye point. JPM alijenga imani ya wananchi kwa serikali yao.hata kama kuna wachache waliokuwa wanaumia na uongozi wake lakini hukusikia watanzania wakiwa na hofu na uongozi wake .refer alivyoshugulika na swala la covid , watanzania walikua nae bega kwa bega katika maamuzi yake juu ya swala la covid ,haya ndugu yangu nikuulize hali ipoje kwa watanzania juu ya namna SSH ananyoshughulika na swala la covid ,ana support ya watanzania . jibu ni NO. watu bado wanapiga nyungu swala la chanjo hawataki kusikia. same kwenye swala la tozo . kupotea kwa kina ben saa nane usifikiri kuwa ni watanzania wote waliumia ,kuminywa kwa uhuru wa siasa usifikiri watanzania walikua wana time na siasa zao . watanzania walikua na imani na raisi wao. tofauti na sasaa
Baadhi ya watu wataweza kukubali hoja yako. Hata hivyo tuulize swali moja. Uchaguzi mkuu 2020 uliendeshwaji na matokeo gani. Kwa nini ilikuwa hivyo.
 
Samia, Majalwa na wenzake, wanaweza kuukosa ufahamu, wakiamini kuwa wanaweza kufuta Kanisa fulani lakini hawatambui kuwa wakristo ni wakristo, madhehebu siyo ukristo. Madhehebu ni njia tu kuufikia ukristo.

Dhuluma dhidi ya mkristo mmoja ni dhuluma dhidi ya wakristo wote.
 
Samia, Majalwa na wenzake, wanaweza kuukosa ufahamu, wakiamini kuwa wanaweza kufuta Kanisa fulani lakini hawatambui kuwa wakristo ni wakristo, madhehebu siyo ukristo. Madhehebu ni njia tu kuufikia ukristo.

Dhuluma dhidi ya mkristo mmoja ni dhuluma dhidi ya wakristo wote.
Na mzee wa kutoa macho kama mjusi naye anashindwa kumshauri amebaki kurusha mate tu
 
Baadhi ya watu wataweza kukubali hoja yako. Hata hivyo tuulize swali moja. Uchaguzi mkuu 2020 uliendeshwaji na matokeo gani. Kwa nini ilikuwa hivyo.
Hapakuwa na uchaguzi bali uporaji
 
Mzee wa Libapa Likubwa ?.Enheee ! Libapa Likubwa,una maana gani.Au lile lichupa Likubwa la konyagi ! Ngoja Huyo Mzee wa U*p*ko, a.k.a.Likonyagi Likubwa aione hii clip yako,ndo utaipata Fresh
Fresh ipi na kwanini
 
Ni mnafiki kama wanafiki wengine tu huyu mzee. Mara ngp serikali imefanya mambo ndivyo sivyo kwa wananchi wake amekaa kimya? Yaani leo taasisi za kidini zimeguswa ndiyo anafungua hilo domo lake? Alikuwa wapi miaka na miaka wengine walipoonewa?
Hata wew huwezi kupigana iwapo hutaona sababu za kupigana mkuu
 
Duh huyu mwamba bado yupo? Aisee kuna kipindi ARV zilimkataa alipaukaaaaaaaaaaaaa nywele zilikua kama kalambwa na mbwa koko, yaani haeleweki kalikiti si kalikiti wave si wave yaani , na tumacho tuliingia ndaniiii alibakia kichwa tu, nadhani ameshauriwa vizuri asiache dawa zake maskiiiini.
 
Ni either huna uelewa wa mambo au umeamua kushupaza shingo kwa kivuli cha udini.Nikupe mifano michache-Askofu Niwemugizi wa Ngara alinyang'anywa pasipoti baada ya kuongelea masuala ya katiba mpya;Askofu Juda Thadeus Ruwaichi alipambana sana na magufuli kuhusiana na msimamo wa serikali kuhusiana na CORONA,Askofu Shoo KKKT aliongelea sana madhila viongozi wa upinzani wanayofanyiwa nchini kwamba siyo sawa,TEC waliwahi kutoa Ujumbe wa pasaka kuhusiana na baadhi ya matukio mabaya yaliyokuwa yanafanyika nchini kiasi cha kuichukiza serikali ambayo ilipanga mkakati wa kuyafuta makanisa na baadaye kupiga U-turn.Swali la msingi-Mashehe wa Kiislamu zaid ya 150 nchi nzima waliwekwa Jela na Viongozi wa kikristo?? Kwa hiyo hata kama kitu kilichozungumzwa na Lusekelo (ambaye wewe unasema ni mchafu) ni sahihi,Je,tukipinge tu kwa sababu ni Lusekelo kasema au tupime usahihi wa jambo lenyewe?
Muulize kuwa nchi hii nani ni mtakatifu na mwenye haki ya kukemea?
Uchafu wake tumwachie yeye sisi tujali hoja muhimu aliyoitoa
 
Katika hali ya kushangaza, siku zote mzee wa Upako huwa upande wa serikali.
Lakini leo ameamua kuvunja ukimya na kuinyoshea serikali kidole tena kwa ukali kuwa ijihadhari isije kuharibu amani ya Tanzania.

Wakati akitoa angalizo hilo, amewataja kwa majina akianza na Kassim Majaliwa waziri mkuu, Rais Samia na Mpango.

Amewakumbusha kuwa sio vyama vya upinzani pekee huleta machafuko bali hata Serikali huwa ni chanzo cha machafuko.

Ameonya kuwa uonevu ukizidi hata askari taratibu huungana na raia kinyume cha watawala kwani hata wanao onewa ni jamaa zao na maaskari.

Zaidi ameionya serikali kujiepusha na kuingilia mambo ya kidini kwani hata wakizifuta imani za dini ziko mioyoni mwa watu na sio kwenye usajili wa kiserikali.

Amekumbusha kuwa miaka ya 80 serikali ilijaribu kufuta usajili wa makanisa hata kuwafunga wengine lakini ilishindwa na tena wakristo waliungana.

Amesema watu wa imani moja huungana wakati wa kuonewa hivyo wajihadhari na jambo hilo.

Amesema kwasasa serikali ina matatizo makubwa kisiasa, corona nk kwa hiyo isiongezee mzigo wa kidini haitabaki salama.
Zaidi msikilize hapo chini kwenye link.

View attachment 1897536
Safi sana hiyo naungamkono
Nakuunga mkono
 
Hawa wahuni wanaojiita viongozi wa dini JPM aliwadekeza sana, huyu alimjengea hadi barabara ya lami waumini wake wapite, kila mara alikuwa anawaalika ikulu na kuwapa upendeleo wa juu, na hiyo yote ni kutokana na uoga wake na kutojiamini, akipenda kusifiwa na kila mtu!! Wale wa upande mwingine ilikuwa ni kuwalisha ubwabwa na kuwahonga misikiti, miezi hii mitano wamepotezewa tayari wameanza mayowe! Ni wengi wataibuka, vikiwemo vyombo vya habari kama Clouds ambavyo vimekuwa yatima kwa sasa ambavyo mbeleko walilolitegemea lipo Chato milele. Kila utawala na namna yake ya kutawala. Itatuchukua siyo chini ya miaka 3 sumu na propaganda alizosambaza JPM nchi kuisha
Utakuwa ni mpumbavu sana kama hujaona point za Lusekelo,!
 
Jaman jaman hii nchi haina watu wajinga kama serikal inavyodhani.Haina watu wajiga kabisaa.Uvumilivu hekima na matumain ya watu kuwa things will be better ahead visitafsiriwe kama upumbavu au watu hawaoni.MZEE LUSEKELO KAONGEA VITU VYA MSINGI SANA.sio lazima serikal isikie lakin haitakosa cha kujifunza kwa kusikia maoni kama haya toka kwa watanzania sisi tunaochukuliwa kama wajinga flan.
 
Mzee Lusekelo naona busara zake zinapungua kwa kasi sana!!
namshauri awe anafikiria kwanza kabla ya kuzungumza, maana yeye ni kiongozi wa waumini, hivyo asije akadharauliwa.

Kinacho fanywa na Serikali hii sio jambo jipya .
Serikali hawezi kuchokonoa taasisi za dini bali serikali inao wajibu wa kulinda Amani na utulivu wa kila raia bila kujali dini.
ni kweli kila raia anao uhuru wa kuabudu lkn uruhu huo lazima uwe na utaratibu na mipaka, Serikali ndio yenye jukumu la kusimamia utaratibu huo.
Serikali haiwezi kuachia makanisa na misikiti ianzishwe kiholela tu bila kufuata utaratibu wa kusajiliwa n.k. inawezekana kuanzishwa vikundi vya kigaidi, waumini kupotoshwa na kuangamizwa n.k, ndio maana serikali imeweka utaratibu wa kusajili Misikiti na Makanisa ili kuzuia makundi maovu na wabaya kutumia mwanya wa kujificha ktk vyombo vya kidini.

Endapo hakutokuwa na utaratibu kama anavyo taka Lusekelo kutasababisha vurugu.
Lusekelo asiifundishe Serikali namna ya kusimamia Amani ya nchi, kwenye jambo hili namshauri akae afikirie au azungumze na Waziri wa mambo ya ndani Simbachaweni.


Waziri Simbachaweni amekuwa kimya sana kwenye mambo ya msingi, tuna muomba awe anajitokeza kwa wakati kujibu upotoshaji unapo jitokeza.
wizara ya mambo ya ndani ndio wizara iliyo pewa dhamana ya kusimamia Amani ya nchi hiii, hivyo tusiwaachie watu wanapotosha ukweli either kwa maksudi au kwa kutoelewa au kwa malengo binafsi.
tusinywee kwenye masuala ya Amani ya nchi, tujitokeze kwenye vyombo vya habari tutoe ufafanuzi, tusiachilie upotoshaji uchukue nafasi.
Mawaziri wetu mmepewa dhamana ya kutuongoza na kusimamia, acheni kukaa kimya kama mmeshindwa kazi ni bora mkaomba kustaafu kuliko kuamua kula ganzi.
Ni kweli sio jambo jipya, pia amewakumbusha kuwa haya yalifanyika miaka ya 80 na serikali ilishindwa
 
Back
Top Bottom