Mchungaji apigwa na wananchi wa Kigoma kwa kuzuia waganga wa kienyeji "Kamchape" wasiingie eneo la kanisa kutafuta uchawi

Mchungaji apigwa na wananchi wa Kigoma kwa kuzuia waganga wa kienyeji "Kamchape" wasiingie eneo la kanisa kutafuta uchawi

Huko ni kuingiliana uhuru wa kuabudu.

Au mpaka kwenye misikiti nako wanafanya hivyo.

Sijui kwanini ndugu zetu waislamu wakiwa na kiongozi mkubwa serikalini ndio wanazidisha vituko vya kuchafua dini za wengine.
 
mchungaji avamiwa na wananchi na kupigwa vikali baada ya kugoma kukubali watu wenye imani potofu kuingia kwenye viwanja vya kanisa kutoa uchawi.

waganga hao wa kienyeji wanakusanya 5,000/ kwa kila nyumba, kama malipo ya kuwatoa wachawi wote. Mchungaji aligoma kuwapa hela na aligoma kuwaruhusu kuingia kwenye maeneo ya kanisa.

Najiuliza kwanini watu Wa tanzania tunanaamini sana kwenye uchawi, Elimu itolewe ili Watanzania Tuache Imani za ushirikina. Imagine kwenye zama hizi za teknolojia bado kila nyumba inalipishwa 5000 na waganga wa kienyeji ili watoe wachawi

View attachment 2932691
Usiseme watanzania sema hayo majinga ya Kigoma. Kwanza Kigoma wengi siyo raia. Hayo majitu yako nyuma kabla ya uhuru wa Tanganyika
 
Sometime wale jamaa zetu wa upande wa pili wanakuaga sahihi. Dharau zinazidi. Unahisi nini kingetoa kama wangelazimisha kuingia msikitini kama sio kupelekewa moto hadi akili ziwakae vizuri?
 
Funguka acha kukariri, Kila Jamii ina mungu wake, wachina Wana mungu wao, wahindi, waarabu, wazungu etc wana wa kwao pia, hata waafrica kabla ya ukoloni tulikuwa tuna mungu wetu, sasa Leo mmeletewa mungu na hao wazungu na waarabu mnaona hakuna mwingine, inabidi kutuma akili sana haya mambo ya Imani la sivyo utaonekana chizi tuu, Jamii nyingi sana zimeanza kushtukia huu usanii na hata hao wazungu waliowaletea huyo mungu wameanza kushtukia na kuachana na hayo mambo ya kufikirika na hadithi za watu wa kale
Wewe ndio ufunguke. Tofautisha Mungu na miungu. Ukijua tofauti ya hayo majina mawili hutahangaika .
 
Vyote viwili kuviamini ni uvivu wa kufikiri

Imani ya Uchawi imeletwa na dini

Dini na uchawi ni sawa na simba na yanga zinategemeana na zinaendana
Ila watu Kwa kuropoka eti dini na uchawi vinategemeana. Yani akina mwamposa wamewafanya muamini ujinga Sana.
 
"Nikapiga simu polisi ...polisi hawaji
Piga simu polisi hawaji
Nikampigia simu baba askofu alikuwa Dodoma
Ndipo naye akapiga simu polisi baadaye wakaja"

hahaha nakuelewa kumaanisha nini 😁
 
mchungaji avamiwa na wananchi na kupigwa vikali baada ya kugoma kukubali watu wenye imani potofu kuingia kwenye viwanja vya kanisa kutoa uchawi.

waganga hao wa kienyeji wanakusanya 5,000/ kwa kila nyumba, kama malipo ya kuwatoa wachawi wote. Mchungaji aligoma kuwapa hela na aligoma kuwaruhusu kuingia kwenye maeneo ya kanisa.
Napiga simu Polisi waje, hawaji. Napiga simu Polisi waje, hawaji.

Mchungaji, nakushauri siku nyingine ukitaka Polisi waje kwa spidi ya ndege waambie Chadema wamekusanyika kanisani kufanya mkutano bila kibali!
 
Back
Top Bottom