Mchungaji asimamishwa kazi tuhuma za kumtorosha mke wa muumini wake

Mchungaji asimamishwa kazi tuhuma za kumtorosha mke wa muumini wake

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
MCHUNGAJI wa Kanisa la Anglikana Yombo Kiwalani jijini Dar es Salaam Edwin Taji, amesimamishwa kutoa huduma ya kichungaji baada ya kudaiwa kumtorosha mke wa muumini wake na kumpangishia nyumba maeneo ya Pugu Kajiungeni.

Madai hayo yametolewa na muumini wa kanisa hilo ambaye ni Mume wa mwanamke huyo Simon Ngalawa mkazi wa Yombo akilalamika kuwa mkewe Ester Makunya kujihusisha kimapenzi na mchungaji Taji.

Ngalawa anadai baada ya kusikia tetesi hizo kutoka kwa waumini na ndugu zake, alibaini kuwa mkewe alianza kuwa na fedha wakati hana kazi wala biashara yoyote, na baada ya kupitia kipindi kigumu cha maisha kwa miaka mitatu ndipo alipoondoka nyumbani na kwenda kuishi Kiwalani ambako inadaiwa alipangishiwa nyumba na kufunguliwa duka na mchungaji huyo.

Amesema licha ya kuitisha vikao vya familia, kwenda ustawi wa jamii na Dawati la jinsia lakini ilishindikana mkewe kurudi nyumbani ndipo alipoamua kukutana na viongozi wa juu wa kanisa hilo ili kumshtaki Mchungaji huyo.

Taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo zinaeleza kuwa Mchungaji Taji amesimamishwa kuhudumu wiki mbili zilizopita huku shauri lake likiendelea kujadiliwa na wakuu wa kanisa hilo.

Chanzo: IPP
 
Namshauri bwana Simon Ngalawa aachane kabisa na mwanamke huyo for the sake of his mental health.

Mwanamke kakuacha, kaenda tembea na mchungaji, unamkomalia wa nini? Tafuta mwingine bwana Ngalawa wanawake wapo wengi.

Najua unampenda ila know your worth and be a man, achana nae utapata mwingine pia jitahidi sana upambane upate hela maana it seems mama amefata sadaka zetu waumini.
 
Watu kutaka gudlyf liwe km zawadi ndio Kuna wagharimu. Sadaka zetu wanahonga wadogo zetu wana-walawiti.
Wake zetu wanawatafuna.🤔
#arudi kubambika
FB_IMG_16646613623086734.jpg
 
**Mume Marioo kajaa wivu mke kulelewa peke yake. Hizo nguvu za kwenda kushtak kwa Viongozi wa padre ni gubu, alitaka na yeye afunguliwe Duka kama mke.

NB: kwenye uislam ndo maana Kuna kuoa wake wanne.**

346730951a2f43a3a303e2c325f936ab.jpg
 
Namshauri bwana Simon Ngalawa aachane kabisa na mwanamke huyo for the sake of his mental health...
Mkuu suala ni kuwa anatimiza ahadi ya kuwa na mke mmoja wa kufa na kuzikana. Akimuacha inatakiwa aishi bila mke maisha yake yote kwakuwa akioa atakuwa anazini.
 
Back
Top Bottom