Mchungaji asimamishwa kazi tuhuma za kumtorosha mke wa muumini wake

Mchungaji asimamishwa kazi tuhuma za kumtorosha mke wa muumini wake

Mkuu suala ni kuwa anatimiza ahadi ya kuwa na mke mmoja wa kufa na kuzikana. Akimuacha inatakiwa aishi bila mke maisha yake yote kwakuwa akioa atakuwa anazini.
Paroko anajilia vyake Hana habari
 
Namshauri bwana Simon Ngalawa aachane kabisa na mwanamke huyo for the sake of his mental health.

Mwanamke kakuacha, kaenda tembea na mchungaji, unamkomalia wa nini? Tafuta mwingine bwana Ngalawa wanawake wapo wengi.

Najua unampenda ila know your worth and be a man, achana nae utapata mwingine pia jitahidi sana upambane upate hela maana it seems mama amefata sadaka zetu waumini.
Hivi Katibu alikua anamzidi hela Masanja?
 
Ndoa hamna hapo.

Mwanamke mzinzi kakutana na mchungaji mzinzi
 
Mkuu suala ni kuwa anatimiza ahadi ya kuwa na mke mmoja wa kufa na kuzikana. Akimuacha inatakiwa aishi bila mke maisha yake yote kwakuwa akioa atakuwa anazini.
Hapana, Katika Mathayo 5:32 imeandikwa; Lakini mimi(Yesu) nimewaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwasababu ya uzinzi, anamfanya azini, na mwanaume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka anazini. Mithali 6:32; Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.

Pamoja na kwamba mimi siyo mtaalam wa Theolojia, nilivyoelewa ni kuwa inaruhusiwa kumpa mwanamke talaka kama una uhakika amezini, isipokuwa kama umempa mkeo talaka kinyume na kuwa amefanya uzinzi unamfanya azini hapo wewe ndiyo umekosea mbele za Mungu. Na mwanamke aliyepewa talaka kwasababu ya uzinzi, yeyote atakayekuja kumwoa huyo mwanamke mtalikiwa ajue anazini maisha yake yote. Kwa maana nyingine hairuhusiwi na hurusiwi kama ni mkristo wa kweli kuja kuoa mwanamke aliyepewa talaka kihalali kwasababu ya uzinzi alioufanya. Huyo hatakiwi kuolewa tena.
 
Namshauri bwana Simon Ngalawa aachane kabisa na mwanamke huyo for the sake of his mental health...
inawezekana anachotaka ni ukiri wa mke mbele ya viongozi wa kanisa ili apate ushahidi wa wazi kwa ajili ya talaka. Unajua ndoa za kikristo mpaka uandikiwe talaka ni shida sana, wanataka hata ushahidi wa kanisa nyakati zingine unahitajika.
 
Back
Top Bottom