Mchungaji asimamishwa kazi tuhuma za kumtorosha mke wa muumini wake

Mchungaji asimamishwa kazi tuhuma za kumtorosha mke wa muumini wake

Mkuu ndo maana nakwambia rudi bongo uone sio kuandika vitu vya kusimuliwa na kukurupuka kujitetea umekulia huku. Nguo unazoziongelea zipo kwenye masherehe. Nenda Instagram angalia post za slayqueens wakitoka kanisani ni nguo ndefu za heshima.. Wewe ndie unayeleta mijadala ya ajabu ajabu ili mradi tu upate ligi ya udini
Unaona sasa mkiguswa mnakimbilia kwenye chuki za kidini
Hapo unazidi kuwasha moto tu na ndio mnapenda mijadala ya hivyo ya kuvutana na matusi juu

Nimekulia huko na nimeyaona sana kina mama nguo wanazovaa kumfurahisha mchungaji

Kweli yapo makanisa yaliyoamua kuwakataza waumini kuvaa vibaya na wajisitiri na matangazo nimeyaona nje

Lakini kubali kuwa yapo mengine mpaka leo bado wanaingia mapaja wazi sio uongo wala chuki niwe Muislam au mkiristo ukweli ni lazima usemwe wala sio chuki kama ulikolipeleka wewe
 
Hawa wachungaji sijui manabii na maprophets haaahaaaàaa nilishawanawa kitambo.....uhuni mtupu
 
Mkuu ndo maana nakwambia rudi bongo uone sio kuandika vitu vya kusimuliwa na kukurupuka kujitetea umekulia huku. Nguo unazoziongelea zipo kwenye masherehe. Nenda Instagram angalia post za slayqueens wakitoka kanisani ni nguo ndefu za heshima.. Wewe ndie unayeleta mijadala ya ajabu ajabu ili mradi tu upate ligi ya udini
Sawa mkuu yaishe
Sitaki ligi ya hii ila humu kila mmoja ana haki ya kutoa mawazo yake
Kuna watu wamo wanatetea majizi nao pia ni haki yao kutoa maoni

Wapo wanaopinga mabaya na wapo wanaotetea pia
Mimi nimeandika maoni yangu na wewe umetetea unayojua sawa
 
Wanawake Kwa wachungaji sijui wamewaroga na nini
Wala hawana uchawi wowote,
Zaidi ya kuchukua baadhi ya maandiko kwenye biblia na kugeuzageuza maana na kutumia mistari kama silaha ya kutongozea wanawake.

Wahuni sn hao,,
 
MCHUNGAJI wa Kanisa la Anglikana Yombo Kiwalani jijini Dar es Salaam Edwin Taji, amesimamishwa kutoa huduma ya kichungaji baada ya kudaiwa kumtorosha mke wa muumini wake na kumpangishia nyumba maeneo ya Pugu Kajiungeni.

Madai hayo yametolewa na muumini wa kanisa hilo ambaye ni Mume wa mwanamke huyo Simon Ngalawa mkazi wa Yombo akilalamika kuwa mkewe Ester Makunya kujihusisha kimapenzi na mchungaji Taji.

Ngalawa anadai baada ya kusikia tetesi hizo kutoka kwa waumini na ndugu zake, alibaini kuwa mkewe alianza kuwa na fedha wakati hana kazi wala biashara yoyote, na baada ya kupitia kipindi kigumu cha maisha kwa miaka mitatu ndipo alipoondoka nyumbani na kwenda kuishi Kiwalani ambako inadaiwa alipangishiwa nyumba na kufunguliwa duka na mchungaji huyo.

Amesema licha ya kuitisha vikao vya familia, kwenda ustawi wa jamii na Dawati la jinsia lakini ilishindikana mkewe kurudi nyumbani ndipo alipoamua kukutana na viongozi wa juu wa kanisa hilo ili kumshtaki Mchungaji huyo.

Taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo zinaeleza kuwa Mchungaji Taji amesimamishwa kuhudumu wiki mbili zilizopita huku shauri lake likiendelea kujadiliwa na wakuu wa kanisa hilo.

Chanzo: IPP
Masanja kapata mtetezi wake kwenye tasnia yao.
 
Ni wazi mke hataki ndoa hivyo ni vema Mume akaacha kulazimisha mahusiano.

Mume kwa mujibu wa Biblia anaruhusiwa kuoa mwanamke mwingine ( maadamu kosa la uzinzi wa mke limethibitika)
 
Back
Top Bottom