Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Usijidanganye wewe, hakuna kitu rahisi kuanzisha kama kanisa, tena kwa mtu kama Mch Kimaro akiamua akakohoa tu kho, Kanisa tiyar.
Huo ugumu unaosema sijui unamaanisha ni ugumu wa kuliandikisha au wa waumini??!!!
Yeye akaanzishe Madrasa tu,keshasema anawaamini vijana wa kiislam hao Ndio wawe waumini wake
 
What is seminar... Zipo kwenye calendar za kanisa.
Kwani semina mpk ziwekewe kalenda?Semina inakua jinsi mtumishi anavyoongozwa na roho wa Mungu kuhusu uhitaji wa watu kwa wakati husika,sio mpk muweke kalenda zenu za kutumia akili.

Haya makanisa ndio mpk mtumishi anapangiwa leo hubiri hiki na sio hiki

Ukihubiri hiki utafukuzwa kanisani,upuuzi mtupu na utapeli
 
Hajalazimishwa. Walifanya kikao kwanza kwenye ofisi ya Msaidizi wa Askofu DMP. Wakakubaliana. Yeye ndio kajiona yupo juu kuja kuwalilia washirika na kuchochea wafausi. Yule afukuzwe moja kwa moja miasi.
😂😂😂Haya makanisa haya,watu wanajiundia vijitaasisi vya kuchota pesa za raia ni kama siasa tu yani,watu wanajiundia vi vyama wapige ruzuku,waishi
 
Kwani semina mpk ziwekewe kalenda?Semina inakua jinsi mtumishi anavyoongozwa na roho wa Mungu kuhusu uhitaji wa watu kwa wakati husika,sio mpk muweke kalenda zenu za kutumia akili.

Haya makanisa ndio mpk mtumishi anapangiwa leo hubiri hiki na sio hiki

Ukihubiri hiki utafukuzwa kanisani,upuuzi mtupu na utapeli
Ndo 4 4 2 yetu.. Kama unataka 4 3 3 NeNda kaanze ya kwako.
 
Ukishaona taasisi imejaa wachaga jua hakuna kinachoendelea zaidi ya upigaji
Naomba ku declare kabisa mimi nimekulia kkkt kuanzia sunday school, kipaimara mpak sas najielewa. Ukwel ni kwamba kanisa letu limejikita kuhubiri michango na utoaji kuliko kuponya na kuinua watu spiritually ndo mana kuna ma conflict of interest



Sio Kweli.

Acha kuwachukia wachaga.

Makanisa karibia yote ya kilokole yale ya mwendokasi na haya kongwe ya kawaida ya CCT na Roma yote siku hizi ni upigaji mtupu wa sadaka na michango chungu nzima [emoji108]

Kwa Hilo huko kote ni wachaga wanapiga?

Sio vizuri kuleta chuki za wazi za kikabila. Maana hazijengi zinabomoa upendo na mshikamano.

Kwa unataka kusema Kimaro anasakamwa sababu ya kuwa Mchaga?

Wekeni wazi tuhuma zake tuzijue na sio kumhukumu kwa jumla jumla Eti sio mtiii ! Kipimo cha utii ni kipi?
 
Achaneni na makanisa ya kitapeli haya, viongozi wanawaza fitina na kulogana tu,kukamua sadaka za waumini
Haya madhehebu ni ushenzi tu

Watu wamekaa wakajianzishia vijitaasisi vya kupiga hela
[emoji23][emoji23]
We nae mbona unakomaa na makanisa yakitapeli..kwanini usiendelee na kanisa lako kimyakimya Bila kutukana wenzako..au huyo mungu wenu anapenda Sana matusi..Mimi Sina dini kabisa..yaani naona mambo ya dini ni ujinga/upumbavu.. lakini siwezi kulazimisha mtu kama unavyofanya hapa
 
Mimi ni muislamu lakini nasema huyu Pastor Kimaro ni bonge la Pastor na waliomfanyia hizo figisu hawana roho wa Mungu ndani yao.

# Baba Kimaro kama unasoma UJUMBE huu please tunaomba tunaomba ufungue kanisa lako.

Siku 60 ni nyingi sana.

😭😭😭😭😭😭
Kanisa ni kama taasisi nyingine yeyote ina misingi na kanuni na taratibu na mara nyingi wanao jiona wamekuwa wazuri ki huduma husahau kama ile ni taasisi yenye taratibu zake ,

katiba ya KKKT iko vizuri sana hayupo ambaye anaweza kuwa zaidi ya kanisa na ukitaka kuwa basi unakatwa mapembe hata uwe askofu nani, ndio uzuri wa KKKT
 
Maombi yake siku anatangaza kupewa likizo na kuhamishwa yalikuwa ya kupandikiza uasi ndani ya kanisa. Ni hekima ya hao viongozi wake tu,anatakiwa avuliwe uchungaji.

Mtu anahamishwa na anaacha mchungaji mwenzake hapo kanisani lakini anafanya kama huyo mchungaji mwenzake sio kitu au sio mchungaji.

Kiburi cha umaarufu ni kibaya sana.
swali la kujiuliza, yeye alihamia pale akitokea Kariakoo Lutheran (KKKT), kama aliyemuachia kijiti naye angefanya anayofanya yeye angekuwa mchungaji wa kijitonyama? Kanisa alilikuta, wachungaji wengi wamehama miaka nenda rudi, na kama kila mchungaji atakuwa hataki kuondoa sehemu uliyomhamishia, patatosha? kwani hakuna uongozi? hakuna viongozi? hakuna wakubwa? yeye au wao na maaskofu na viongozi wengine wote wapo sawa au mmoja ni kiongozi wa mwenzake.

pale alichofanya, kwanza ameanzisha uasi kwenye kanisa, pili, amecreate kazi kubwa sana kwa mchungaji atakayempokea kijiti, waumini hawatamkubali, itakuwa shida. tunawaachia wao wenyewe walutheran tuone watafanyajea.
 
swali la kujiuliza, yeye alihamia pale akitokea Kariakoo Lutheran (KKKT), kama aliyemuachia kijiti naye angefanya anayofanya yeye angekuwa mchungaji wa kijitonyama? Kanisa alilikuta, wachungaji wengi wamehama miaka nenda rudi, na kama kila mchungaji atakuwa hataki kuondoa sehemu uliyomhamishia, patatosha? kwani hakuna uongozi? hakuna viongozi? hakuna wakubwa? yeye au wao na maaskofu na viongozi wengine wote wapo sawa au mmoja ni kiongozi wa mwenzake.

pale alichofanya, kwanza ameanzisha uasi kwenye kanisa, pili, amecreate kazi kubwa sana kwa mchungaji atakayempokea kijiti, waumini hawatamkubali, itakuwa shida. tunawaachia wao wenyewe walutheran tuone watafanyajea.
Mbwa mwitu walilivamia kanisa na wakaanza kutengeneza ufalme wao na kuacha ule wa Mungu.

Mbwa mwitu wana kiburi na wanaamini hawapaswi kuguswa na yeyote.
 
Namkubali

Siku hizi kuna makanisa ya maji, mafuta na chumvi hayana tofauti na uganga wa jadi
kwahiyo na kanisa lake yeye mwenyewe ni madalali, pamoja na boss wake Shoo ambaye anatoka naye Machame. unafikiru huu uamuzi wa kumng'oa, Dr. Shoo mchaga mwenzie wa machame ambaye ndiye mkuu wa kanisa hilo atakuwa amerukwa? lazime yeye ametoa go ahead. sidhani kama kkkt wamekurupuka.
 
View attachment 2486999
Picha: Mchungaji Eliona Kimaro

Semina iliyokuwa imeanza katika usharika wa KKKT Kijitonyama ikiongozwa na Rev Dr. Eliona Kimaro imelazimika kusimama kufuatia barua aliyopewa ya likizo ya siku 60 na kupelekea kushindwa kuendelea na semina hiyo.

Mchungaji Kimaro amesema anatumia fursa hiyo kuwaaga Washarika wake na kuanzia Januari 17 Mchungaji Anna ataendelea kuwa kiongozi wa Kanisa hilo.

Kwa mujibu wa barua, Mchungaji Kimaro atamaliza likizo yake ya lazima 17/03/2023 na barua inamuelekeza kuripoti makao makuu na sio usharika wa KKKT Kijitonyama ambapo atapangiwa sehemu nyingine.

View attachment 2487019

Video: Mchungaji Kimaro akiwaaga waumini
Amesema:
"Mimi ni Mchungaji wa Lutheran ninayeheshimu kiapo changu cha kichungaji na kuishi katika kiapo changu cha kichungaji na maadili pia ya kichungaji kwa neema ya Mungu. Kwa sababu hiyo imenilazimu kutii amri na kwenda kwenye hiyo likizo ya siku 60 na baadae kuripoti kwenye ofisi ya Askofu kama nilivyoelekezwa" Asante.

View attachment 2487041
Video: Mchungaji Kimaro akiombea Waumini baada ya kuaga

UPDATES
Baadhi ya Waumini wa KKKT wajitokeza kupinga uamuzi wa Mchungaji Kimaro kupewa likizo
Waumini Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama wamekubaliana kutoingia ndani ya Kanisa hilo hadi watakwporudishiwa Mchungaji wao Dk Eliona Kimaro aliyepewa likizo ya siku 60.

Uamuzi huo umefikiwa na waumini hao baada ya kukubaliana kufanya maandamano ya amani katika viwanja vya kanisa hilo hadi pale mchungaji wao atakaporudishwa au kupewa sababu za kupewa likizo hiyo.

Tazama baadhi ya video hapa chini:

View attachment 2487024

View attachment 2487032

View attachment 2487035

Video hizo hapo juu zinawaonesha Waumini wa KKKT Usharika wa Kijitonyama wakipinga mchungaji wa usharika huo Dk Eliona Kimaro kupewa likizo ya siku 60.


PIA SOMA:
1. https://www.jamiiforums.com/threads...amlijui-viongozi-wake-hawajakurupuka.2057299/

2. https://www.jamiiforums.com/threads/projects-za-mchungaji-kimaro-akiwa-kkkt-kijitonyama.2057447/

3. https://www.jamiiforums.com/threads...ma-na-kiongozi-wangu-askofu-malasusa.2057711/
Hakuna vitu vya kijinga duniani kama dini
 
Imeandikwa; “Mungu ni Roho nasi tumwabudo inatupasa kumwabudu katika Roho na Kweli.”
 
Back
Top Bottom