Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

ASKOFU MWAMAKULA AZUNGUMZIA SUALA LA KUSIMAMISHWA KWA MCH. DKT. KIMARO

Taarifa za kupewa likizo na kusimamishwa kwa muda kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama Mch. Dkt. Eliona Kimaro zimeanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kuzua hisia nzito miongoni mwa waumini na wasio waumini wa KKKT. Kimaro ni miongoni mwa watu maarufu, hivyo suala hili haliwezi kuchukuliwa wepesi.

Hapa tumeweka tazamo wetu wa kitheologia ili kutoa mchango wetu katika hoja hii. Ni dhahiri kuwa misimamo binafsi ya Mch. Dkt. Kimaro imemtia katika misuguano mingi na uongozi wa KKKT kwa kipindi kirefu. Lakini, misimamo hiyo iliweza kuvumiliwa ndani ya KKKT na ndio maana alipewa kuongoza Usharika mkubwa katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Tumefuatilia kutoka kwa baadhi ya viongozi ndani ya Dayosisi ya Mashariki na kuelezwa kuwa matamshi ya Mch. Dkt. Kimaro aliyoyatoa hivi karibuni baada ya kutoka Marekani ndiyo yaliyopelekea uongozi wa Dayosisi kumuita na kumpa likizo ambayo imeibua hisia na mjadala mzito baada ya yeye Mch. Dkt. Kimaro kutoa hadharani jambo ambalo lilikuwa ni karipio la Kichungaji.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu bali vijana wa Kiislamu ndio waaminifu kuliko vijana wa Kikristo. Mch. Dkt. Kimaro amesikika pia akisema kuwa watu wote wanaosimama madhabahuni [Wainjilisti, Wachungaji na Maaskofu] ni matapeli na watu wote waliokaa kwenye viti [vya ibadani - Wazee wa Kanisa na waumini] ni matapeli pia. Mch. Dkt. Kimaro amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa takwimu [hajataja ni takwimu gani na taasisi iliyotoa takwimu hizo] zinaeleza hayo aliyosema.

Kitheologia tunapata tafsiri kuwa Mch. Dkt. Kimaro hana imani na maadili ya Kikristo, hana imani na mafundisho ya Kikristo na pia hana imani hata na watumishi wenzake wote wa Kikristo kutoka madhehebu yote nchini Tanzania. Tafsiri hapa ni kuwa Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa ana imani na maadili ya Kiislamu, mafundisho ya Kiislamu na hata Mashehe wa Kiislamu. Pia, Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa hana imani pia na hata vijana wake wa Kikristo ndani ya KKKT na nje ya KKKT ambao siku zote yeye mwenyewe amekuwa akiwafundisha katika ibada, mikesha, semina, morning glory, bali ana imani kubwa na vijana wa Kiislamu ndio maana akawaajiri hao katika miradi yake.

Mtumishi ye yote (Mwinjilisti, Mchungaji/Padre au Askofu) kutoka katika madhehebu yetu ya Katholiko (RC, Moravian, Lutheran, Anglikana na Orthodox) akitoa kauli kama hizo, ni lazima aitwe na uongozi wake, ahojiwe na hata ikibidi achunguzwe. Hicho ndicho kilichotokea kwake Mch. Dkt. Kimaro kuitwa na uongozi wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, kuhojiwa na kuchunguzwa. Kauli zake alizotoa zimepingana na imani, mafundisho na maadili ya Kikristo! Kauli ya Mch. Dkt. Kimaro hayakushambulia Ulutheri tu, bali kwa kujua au hata kutokujua, kauli yake ilishambuliwa Ukristo wote kwa ujumla katika nchi hii.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu tunatoa wito kwa waumini wote wa Kikristo nchini kuwa watulivu wakati KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani inashughulikia jambo la Mch. Dkt. Kimaro. Sisi tumelazimika kuandika baada ya kuona kuwa jambo hili limeanza kusambaa mitandaoni na kubeba hisia zaidi kuliko uhalisia na pengine kubeba upotofu mwingi zaidi kuliko ukweli.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
Kama sababu ni kusema vijana wa kiislamu wamekuwa waaminifu basi KKKT hao viongozi na huyu Mwamakula sijui watakuw hawajielewi kabisa
 
Mimi Nimezaliwa katika familia ya kiluteri na kupata hadi kipaimara ila mambo haya ya migogoro upande wa viongozi yalinikera ukifuatilia chanzo pesa halafu michango karibia mitano lol niliamua niwe tu nasali kwa ukawaida kwa mashahidi wa yehova watu walio na upendo wa hali ya juu wakiyaishi maisha ya viwango ya kikristo kwa matendo.

Kwanza KKKT inashangaza eti mtu anaweza akaacha kanisa lake la KKKT mtaani ila akawa anaenda kusali usharika wa Kimara eti kisa mchungaji wa Kimara ni maarufu anamvutia swali Je, akifa huyo mchungaji utaendelea kwenda huo usharika wa Kimara?
Mie ndiyo nasema Kanisa liheshimiwe jamani , yaani mtumishi asiwe juu ya KANISA!!!!! DAAAH HIZI PESA !!!!!!!!!!!
 
Duh
Mnamuondoa Eliyona mnamleta Anna?
1 Timotheo 2:12
[12]Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
But I suffer not a woman to teach, nor to usurp authority over the man, but to be in silence.
Ikiwa ya kwamba mnalisaliti neno ambalo kwalo mnajihalalisha kusimamia wengine mtashindwa nini kulana wenyewe kwa wenyewe?

Kkkt kwa kiasi kikubwa inaendeshwa kama chama cha siasa.

Fitina nyingi, uchawa mwingi na hata ushirikina mwingi hasa kwenye uchaguzi.

Hiyo Dayosisi ya mashariki na Pwana ina vita vya mda mrefu kati yake na watu wa ukanda wa kaskazini uliochagiza hata askofu wake Malasusa kuungana na Magu katika mkakati wa kuwademolish hawa watu.
Kuna mch mmoja huko kutoka kanda ya kaskazini aliyekuwa mkuu wa jimbo kwa wivu aliondolewa na kupelekwa huko Mwanarumango.

Sasa wakati Kimaro akitendewa haya yule Maksai wa Kimara Korogwe atie maji na baadae aliyekuwa Ubungo Plaza kabla ya kuhamishiwa Mbezi luis ajiandae kwa panga la Alex G.
Jamani mchungaji wetu nkya ubungo plaza tunammiss sana toka tupo wadogo mpaka sasa watu wazima wakaja kumuhamisha kumpeleka mbezi luis kanisa tumejenga naye na michango yetu

Kkkt ubungo plaza tujuane
 
Mimi nilikuwa sijui kinachoendelea hapo Kijitonyama ila ulivyoanza kuelezea tu kichwa changu kikaenda kwa Mchungaji Masai wa Kimara.

Nimesali pale Kimara mara moja moja nikimtembelea jamaa yangu, ni kweli ibada za pale sio za KKKT. Kuna siku ilibidi wenzangu waende pale mimi nikapitiliza nikaenda kusali Ubungo, niliwaambia mimi nimezoea ibada zetu za kilutheri hapo siwezi.
YEAH LAZIMA MWONGOZO WA KANISA UFUATWE SIYO MCHUNGAJI ANAKURUPUKA NA VIBES ZA ZAKE KAMA KANISA LAKE!!! HAPANA aisee hata kama ana upako basi vigezo na masharti yazingatiwe.
 
According to History, Makabila yenye Walutheri Wengi ni Wachaga(Marangu, Mwika, Pare, Same, Usangi, Ugheno Machame, Masama, Siha, na Old Moshi).

Arusha Mjini, Meru, Babati, Loliondo Karatu, Manyara, Kiteto. Singida, Baadhi ya Wanyiramba na Wanyaturu, Kagera :- Wahaya, Mbeya Tukuyu na Kyela, Iringa Mjini, Njombe Wabena na Wakinga, Tanga Wasambaa wa Lushoto. Maneromango Wazaramo wachache.

Kwa hiyo utaona Walutheri Wengi ni Wachaga, Wahaya, Wabena, Wanyakyusa, Wapare, Wanyiramba, Wameru, Wamasai , Wasambaa na Wakinga. Hayo ndio Makabila ya Tanzania yenye Walutheri Wengi.

Je ulitaka Kabila la wasio Walutheri washirikishwe wasipoabudu?
Kwenye wasambaaa wala haujakosea mkuu
 
Haswaaa na alipewa mtaji na Kimaro hapo hapo kanisani na alikua muimba kwaya
bhasi ilikuwa ni biashara ya jamaa... anyway huyu jamaa itakuwa ana miradi mingi aliyowapa vijana wa kanisaa wakumdhurumuuu 😀 😀 😀 hasira yake imewakaa juu ya dini ya kikristo maana pesa kwanzaa akajisahau na yeye ni mkristo. Anyway hata hayo mambo ya kusema dini ya kweli ni katoliki sababu ukute kafatiliwa juu ya ubadhirifu wa pesa maana sharika kubwa zenye mapato huwa kuna wizi sana mwisho wa siku hakuna MCHUNGAJI ANAWEZA SHINDANA NA KANISA HATA MALASUSA MWENYEWE HAWEZI.
 
Jamani mchungaji wetu nkya ubungo plaza tunammiss sana toka tupo wadogo mpaka sasa watu wazima wakaja kumuhamisha kumpeleka mbezi luis kanisa tumejenga naye na michango yetu

Kkkt ubungo plaza tujuane
yeah Mchungaji Nkya ni GENTLEMAN!!!!!! Mshauri mzuri, myenyekevu, hana tamaa, anasikiliza, anajitoa bila kuangalia uwezo wa mtu kwa hali na mali, waislamu na watu wa madhebu mengine anaenda nao vizuri, muwazi sana especially kwa vijana na mengi kama hayo. vijana wengi tu pale wamenufaika na ushauri wake ukiwemo i hope,
Binasfi mie ni mkatoliki lakini amenisaidia sana kunipa mwongozo.

MUNGU AZIDI KUMUOMGOZA KATIKA KILA ATUA YA UTUMISHI WAKE
 
Malasusa ana makando kando sana sio mtu wa kumwamini Mnyakyusa yule hili kanisa limekua kijiwe cha wapigaji na kupeana ajira za kindugu tu...ebu fikiria kuna sadaka ya mfuko wa elimu na haina maelekezo.

Mimi nimeamua kuwavungia tu siwezi kwenda tena huko kanisani
 
ASKOFU MWAMAKULA AZUNGUMZIA SUALA LA KUSIMAMISHWA KWA MCH. DKT. KIMARO

Taarifa za kupewa likizo na kusimamishwa kwa muda kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama Mch. Dkt. Eliona Kimaro zimeanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kuzua hisia nzito miongoni mwa waumini na wasio waumini wa KKKT. Kimaro ni miongoni mwa watu maarufu, hivyo suala hili haliwezi kuchukuliwa wepesi.

Hapa tumeweka tazamo wetu wa kitheologia ili kutoa mchango wetu katika hoja hii. Ni dhahiri kuwa misimamo binafsi ya Mch. Dkt. Kimaro imemtia katika misuguano mingi na uongozi wa KKKT kwa kipindi kirefu. Lakini, misimamo hiyo iliweza kuvumiliwa ndani ya KKKT na ndio maana alipewa kuongoza Usharika mkubwa katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Tumefuatilia kutoka kwa baadhi ya viongozi ndani ya Dayosisi ya Mashariki na kuelezwa kuwa matamshi ya Mch. Dkt. Kimaro aliyoyatoa hivi karibuni baada ya kutoka Marekani ndiyo yaliyopelekea uongozi wa Dayosisi kumuita na kumpa likizo ambayo imeibua hisia na mjadala mzito baada ya yeye Mch. Dkt. Kimaro kutoa hadharani jambo ambalo lilikuwa ni karipio la Kichungaji.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu bali vijana wa Kiislamu ndio waaminifu kuliko vijana wa Kikristo. Mch. Dkt. Kimaro amesikika pia akisema kuwa watu wote wanaosimama madhabahuni [Wainjilisti, Wachungaji na Maaskofu] ni matapeli na watu wote waliokaa kwenye viti [vya ibadani - Wazee wa Kanisa na waumini] ni matapeli pia. Mch. Dkt. Kimaro amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa takwimu [hajataja ni takwimu gani na taasisi iliyotoa takwimu hizo] zinaeleza hayo aliyosema.

Kitheologia tunapata tafsiri kuwa Mch. Dkt. Kimaro hana imani na maadili ya Kikristo, hana imani na mafundisho ya Kikristo na pia hana imani hata na watumishi wenzake wote wa Kikristo kutoka madhehebu yote nchini Tanzania. Tafsiri hapa ni kuwa Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa ana imani na maadili ya Kiislamu, mafundisho ya Kiislamu na hata Mashehe wa Kiislamu. Pia, Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa hana imani pia na hata vijana wake wa Kikristo ndani ya KKKT na nje ya KKKT ambao siku zote yeye mwenyewe amekuwa akiwafundisha katika ibada, mikesha, semina, morning glory, bali ana imani kubwa na vijana wa Kiislamu ndio maana akawaajiri hao katika miradi yake.

Mtumishi ye yote (Mwinjilisti, Mchungaji/Padre au Askofu) kutoka katika madhehebu yetu ya Katholiko (RC, Moravian, Lutheran, Anglikana na Orthodox) akitoa kauli kama hizo, ni lazima aitwe na uongozi wake, ahojiwe na hata ikibidi achunguzwe. Hicho ndicho kilichotokea kwake Mch. Dkt. Kimaro kuitwa na uongozi wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, kuhojiwa na kuchunguzwa. Kauli zake alizotoa zimepingana na imani, mafundisho na maadili ya Kikristo! Kauli ya Mch. Dkt. Kimaro hayakushambulia Ulutheri tu, bali kwa kujua au hata kutokujua, kauli yake ilishambuliwa Ukristo wote kwa ujumla katika nchi hii.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu tunatoa wito kwa waumini wote wa Kikristo nchini kuwa watulivu wakati KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani inashughulikia jambo la Mch. Dkt. Kimaro. Sisi tumelazimika kuandika baada ya kuona kuwa jambo hili limeanza kusambaa mitandaoni na kubeba hisia zaidi kuliko uhalisia na pengine kubeba upotofu mwingi zaidi kuliko ukweli.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.

Wao Viongozi ndio wameyakuza, lakini watu walimuelewa pastor Kimaro vizuri tu maana ni alikuwa ana chagiza tu.

Wanatafuta visingizio tu !
 
bhasi ilikuwa ni biashara ya jamaa... anyway huyu jamaa itakuwa ana miradi mingi aliyowapa vijana wa kanisaa wakumdhurumuuu 😀 😀 😀 hasira yake imewakaa juu ya dini ya kikristo maana pesa kwanzaa akajisahau na yeye ni mkristo. Anyway hata hayo mambo ya kusema dini ya kweli ni katoliki sababu ukute kafatiliwa juu ya ubadhirifu wa pesa maana sharika kubwa zenye mapato huwa kuna wizi sana mwisho wa siku hakuna MCHUNGAJI ANAWEZA SHINDANA NA KANISA HATA MALASUSA MWENYEWE HAWEZI.
Inaezekana Mzee Rick kimasihara ila hata wao wana ya kwao why wachukulie hii issue siriaz hivi?
 
yeah Mchungaji Nkya ni GENTLEMAN!!!!!! Mshauri mzuri, myenyekevu, hana tamaa, anasikiliza, anajitoa bila kuangalia uwezo wa mtu kwa hali na mali, waislamu na watu wa madhebu mengine anaenda nao vizuri, muwazi sana especially kwa vijana na mengi kama hayo. vijana wengi tu pale wamenufaika na ushauri wake ukiwemo i hope,
Binasfi mie ni mkatoliki lakini amenisaidia sana kunipa mwongozo.
MUNGU AZIDI KUMUOMGOZA KATIKA KILA ATUA YA UTUMISHI WAKE
Mkuu umeongea ukweli kuhusu Nkya yaani hata harambee kuhusu kanisa na kuhusu mambo mengine mtu unatoa kiroho safi yaani tunamkumbuka sanaaa sanaaaa na tunampenda
 
kanisa ni moja tu: Katoliki la Mitume. uende ibadani usiende. uhudhurie jumuia usihudhurie. ukishakuwa Mkatoliki utaishi kwa amani sana.
Nani kakudanganya.

Wewe kama haushiriki shughuli za kanisa kama kulipa Zaka, kusali Jumuiya na kulipa michango mbalimbali tunakuona kama kibaka tu.
 
Mimi Nimezaliwa katika familia ya kiluteri na kupata hadi kipaimara ila mambo haya ya migogoro upande wa viongozi yalinikera ukifuatilia chanzo pesa halafu michango karibia mitano lol niliamua niwe tu nasali kwa ukawaida kwa mashahidi wa yehova watu walio na upendo wa hali ya juu wakiyaishi maisha ya viwango ya kikristo kwa matendo.

Kwanza KKKT inashangaza eti mtu anaweza akaacha kanisa lake la KKKT mtaani ila akawa anaenda kusali usharika wa Kimara eti kisa mchungaji wa Kimara ni maarufu anamvutia swali Je, akifa huyo mchungaji utaendelea kwenda huo usharika wa Kimara?
We Kuna jambo lilikupeleka huko Mashahidi ..Kwani hatujui
 
Back
Top Bottom