Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

ASKOFU MWAMAKULA AZUNGUMZIA SUALA LA KUSIMAMISHWA KWA MCH. DKT. KIMARO

Taarifa za kupewa likizo na kusimamishwa kwa muda kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Kijitonyama Mch. Dkt. Eliona Kimaro zimeanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kuzua hisia nzito miongoni mwa waumini na wasio waumini wa KKKT. Kimaro ni miongoni mwa watu maarufu, hivyo suala hili haliwezi kuchukuliwa wepesi.

Hapa tumeweka tazamo wetu wa kitheologia ili kutoa mchango wetu katika hoja hii. Ni dhahiri kuwa misimamo binafsi ya Mch. Dkt. Kimaro imemtia katika misuguano mingi na uongozi wa KKKT kwa kipindi kirefu. Lakini, misimamo hiyo iliweza kuvumiliwa ndani ya KKKT na ndio maana alipewa kuongoza Usharika mkubwa katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

Tumefuatilia kutoka kwa baadhi ya viongozi ndani ya Dayosisi ya Mashariki na kuelezwa kuwa matamshi ya Mch. Dkt. Kimaro aliyoyatoa hivi karibuni baada ya kutoka Marekani ndiyo yaliyopelekea uongozi wa Dayosisi kumuita na kumpa likizo ambayo imeibua hisia na mjadala mzito baada ya yeye Mch. Dkt. Kimaro kutoa hadharani jambo ambalo lilikuwa ni karipio la Kichungaji.

Kwa mujibu wa video iliyosambaa, Mch. Dkt. Kimaro amesikika akisema kuwa vijana wa Kikristo sio waaminifu bali vijana wa Kiislamu ndio waaminifu kuliko vijana wa Kikristo. Mch. Dkt. Kimaro amesikika pia akisema kuwa watu wote wanaosimama madhabahuni [Wainjilisti, Wachungaji na Maaskofu] ni matapeli na watu wote waliokaa kwenye viti [vya ibadani - Wazee wa Kanisa na waumini] ni matapeli pia. Mch. Dkt. Kimaro amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa takwimu [hajataja ni takwimu gani na taasisi iliyotoa takwimu hizo] zinaeleza hayo aliyosema.

Kitheologia tunapata tafsiri kuwa Mch. Dkt. Kimaro hana imani na maadili ya Kikristo, hana imani na mafundisho ya Kikristo na pia hana imani hata na watumishi wenzake wote wa Kikristo kutoka madhehebu yote nchini Tanzania. Tafsiri hapa ni kuwa Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa ana imani na maadili ya Kiislamu, mafundisho ya Kiislamu na hata Mashehe wa Kiislamu. Pia, Mch. Dkt. Kimaro anaonesha kuwa hana imani pia na hata vijana wake wa Kikristo ndani ya KKKT na nje ya KKKT ambao siku zote yeye mwenyewe amekuwa akiwafundisha katika ibada, mikesha, semina, morning glory, bali ana imani kubwa na vijana wa Kiislamu ndio maana akawaajiri hao katika miradi yake.

Mtumishi ye yote (Mwinjilisti, Mchungaji/Padre au Askofu) kutoka katika madhehebu yetu ya Katholiko (RC, Moravian, Lutheran, Anglikana na Orthodox) akitoa kauli kama hizo, ni lazima aitwe na uongozi wake, ahojiwe na hata ikibidi achunguzwe. Hicho ndicho kilichotokea kwake Mch. Dkt. Kimaro kuitwa na uongozi wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, kuhojiwa na kuchunguzwa. Kauli zake alizotoa zimepingana na imani, mafundisho na maadili ya Kikristo! Kauli ya Mch. Dkt. Kimaro hayakushambulia Ulutheri tu, bali kwa kujua au hata kutokujua, kauli yake ilishambuliwa Ukristo wote kwa ujumla katika nchi hii.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu tunatoa wito kwa waumini wote wa Kikristo nchini kuwa watulivu wakati KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani inashughulikia jambo la Mch. Dkt. Kimaro. Sisi tumelazimika kuandika baada ya kuona kuwa jambo hili limeanza kusambaa mitandaoni na kubeba hisia zaidi kuliko uhalisia na pengine kubeba upotofu mwingi zaidi kuliko ukweli.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula
Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
Word

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Nimeshangaa sana reasoning capacity ya Mwamakula kumbe ni bure kabisa.
Maneno hayo ukisema mtu kama wew ni poa tuu just assume aseme leo Samia??? So nani kasema na kasemea wapi ndo jambo kubwa inaweza kuwa neno dogo sana lakini likatela mpasuko na shida kubwa sanaa.
 
Nilijua ipo siku KKKT watamfyatua out aidha kwa figisufigisu ili akimbie mwenyewe.

KKKT haipendagi mtu alinyooka ktk ukweli, sasa jamaa huwa yupo straight forward huwa hapindipindi hata kidogo, so kwa Lutheran hiyo ni kasoro, pia kuna ngoma nyingine Askofu Bagonza huyu nae ni kisiki hawana cha kumfanya make huyu nae ni kichwa kingine ambacho kimenyooka na hakuna mtu mwenye uwezo nacho ndani ya KKKT.
Dahh ..huyuu baba mpk kitabu chake nilikua nacho but why?
Waache wivu Mimi muislam lakini nampenda mnoo
 
Maneno hayo ukisema mtu kama wew ni poa tuu just assume aseme leo Samia??? So nani kasema na kasemea wapi ndo jambo kubwa inaweza kuwa neno dogo sana lakini likatela mpasuko na shida kubwa sanaa.
Maonyo na mahubiri huwa hayapigwi ngumu.
Yohana aliwaita wasikilizaji ni kizazi cha nyoka.
Hamyajui maandiko mnaleta aiasa uchwarwa

Imeandikwa kuwa neno la Mungu ni upanga ukatao kuwili. Kanisa lijitafakari kama umefika wakati wanapinga kuonywa
 
1673973986835.png
Vilio na mjadala vimeibuka mara baada ya kusambaa kwa video ikimuonyesha Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kijitonyama Eliona Kimaro akiwaaga waumini wake akieleza kuwa amepewa likizo ya siku 60 na uongozi.

Usiku wa jana, Januari 16, 2023 video ikimuonyesha mchungaji huyo akiwaeleza waumini wake kuwa amepewa likizo ya siku 60 baada ya kuitwa katika ofisi ya msaidizi wa askofu na kufanya kikao na mkuu wa jimbo, ilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

"Semina yetu ni ya wiki mbili (Semina ya neno la Mungu), lakini leo niliitwa ofisi ya msaidizi wa askofu, tulikuwa na kikao na Mkuu wa Jimbo la Kaskazini Mchungaji Mwangomola. Nimepewa barua ya likizo ya siku 60 kesho asubuhi atahubiri Mchungaji Anna na ataendelea kuwa Mchungaji wenu,"

“Kwa mujibu wa barua nitarudi Machi 17 (2023) na sitakuja hapa barua inanilekeza kuripoti Makao Makuu ya Dayosisi kwa hiyo mimi ni mchungaji wa Lutheran kwa hiyo nina heshimu kiapo changu cha kichungaji na kuishi katika kiapo na maadili…

“Pia kwa neema ya Mungu kwa sababu hiyo imenilazimu kutii na kwenda kwenye hiyo likizo na baadaye kuripoti kwenye ofisi ya askofu kama nilivyoelekezwa,” anasema Mchungaji Kimaro katika video hiyo.

Mbali ya video hiyo, ipo nyingine iliyosambaa ikiwaonyesha baadhi ya waumini wa usharika huo wakiangua vilio, wakati mchungaji huyo akifanya maombi ndani ya kanisa hilo wakati akiaga.

Mwananchi imefika kanisani hapo na kuwakuta baadhi ya waumini ambao wameeleza kuwa baadaye jioni watakuwa na jambo lao, ambalo walidokeza kuwa ni kutaka arudi kazini.

Akizungumzia suala hilo, mmoja wa waumini katika usharika huo, Friday John's ambaye ni muumini wa kanisa hilo amesema… “hatujajua watu watapokeaje hili. Mafundisho yake yametutoa mbali, watu wengi wamekuwa wakifuatilia na kupokea mafundisho yake.

“Tunataka mchungaji wetu arudi mafundisho yake yametusaidia ukiacha uchungaji amekuwa na roho ya kipekee ya kusaidia watu.”

Muumini mwingine, Enea Mwantika amesema mchungaji huyo ndio kwanza alikuwa ameanza semina ya wiki mbili na kwamba barua hiyo ya likizo imewaumiza.

“Kilio chetu kwa Dayosisi tunamtaka Mchungaji Kimaro arudi Kijitonyama kuna mtu amehusika. Sisi ndio tunayemfahamu mafundisho yake wapi yanatupeleka na ni nini tunachokipata,” amesema Mwantika.

Alipoulizwa na Mwananchi kuhusu suala hilo, Katibu Mkuu wa KKKT, Robert Kitundu alisema lipo chini ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani.

“Kanisa la Kiinjili la Kilutheri lina dayosisi nyingi. Kunapokuwa na dayosisi maana yake kunakuwa na Askofu ambaye anamiliki lile eneo. Mimi kama katibu mkuu wa Kanisa labda nimeambiwe au vinginevyo kwa sasa wazungumzaji ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambaye ni (Alex) Malasusa au Katibu wake,” alisema.

Mwananchi lilifika katika ofisi kuu za jimbo hilo, Azania Front ambako lilielezwa kuwa Askofu Malasusa yupo nje ya nchi kikazi.

Katibu wa dayosisi hiyo, Goodluck Nkini pia alikataa kuzungumzia suala hilo akieleza kuwa hayo ni mambo ya kichungaji taaluma ambayo alisema hana.

Mwananchi lilimtafuta msaidizi wa Askofu Chediel Lwiza ambaye anaidaiwa kuwa ndiye aliyefanya kikao na Mchungaji Kimaro na mara baada ya mwandishi wa Mwananchi kujitambulisha, alikata simu.

Alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu utaratibu wa kuhamishwa kwa wachungaji katika Kanisa hilo, Askofu mmoja wa KKKT ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe amesema, “Kila dayosisi ina utaratibu wake. Hapo Dar es Salaam nasikia hata wakuu wa majimbo wanahamishwa.”

MWANANCHI
 
Na nyie msilifanye hilo jambo kuwa kuuuubwa. Kama mmeshindwa kugawana vizuri swadaqa za waumini mpige kimya.

Aliondoka martn luther huko rumi na hakuna kilicho haribika
 
Nguvu ya mamba kumayi,nje ya kkkt hana nguvu hata yeye analijua, kuanzisha kanisa sio kazi rahisi kihivyo
Usijidanganye wewe, hakuna kitu rahisi kuanzisha kama kanisa, tena kwa mtu kama Mch Kimaro akiamua akakohoa tu kho, Kanisa tiyar.
Huo ugumu unaosema sijui unamaanisha ni ugumu wa kuliandikisha au wa waumini??!!!
 
Mimi Nimezaliwa katika familia ya kiluteri na kupata hadi kipaimara ila mambo haya ya migogoro upande wa viongozi yalinikera ukifuatilia chanzo pesa halafu michango karibia mitano lol niliamua niwe tu nasali kwa ukawaida kwa mashahidi wa yehova watu walio na upendo wa hali ya juu wakiyaishi maisha ya viwango ya kikristo kwa matendo.

Kwanza KKKT inashangaza eti mtu anaweza akaacha kanisa lake la KKKT mtaani ila akawa anaenda kusali usharika wa Kimara eti kisa mchungaji wa Kimara ni maarufu anamvutia swali Je, akifa huyo mchungaji utaendelea kwenda huo usharika wa Kimara?
Paragraph ya pili wakulaumiwa ni muumini mwenyewe na sio KKKT.
 
Back
Top Bottom