Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Mchungaji Eliona Kimaro wa KKKT Kijitonyama apewa likizo ya siku 60 na kutakiwa kuripoti Makao Makuu

Niseme tu, hakuna marefu yasiyo na ncha.
Kilichokuwa kinatakiwa kufanyika ni kum demolish Kimaro tangu akiwa Usharika wa Kariakoo.

Kwa miaka mingi tumefanya mbinu na njama mbalimbali kumuondoa lakini hazikuwq na matokeo tuliyo yatarajia. Hivyo tukajaribu mbinu nyingine na nyingine tena, hatimaye leo mbuyu haujaanguka ila umemwagika.

Mara ya kwanza tulipofanya yetu akiwa pale Kariakoo alikimbia usharika na kwenda kujificha kwa Mapadre, na mapadre ndio waliofanya jitihada hadi akarudi tena usharikani, ila hii ya sasa harudi, na akirudi basi itakuwa zamu yetu kusalimu amri.

Kimaro alipokuwa Kariakoo, sio kwamba aliharibu taratibu za ibada hapana, hii ni cover tu, tunayoitumia.

Kimaro alipokuwa Kariakoo aliharibu biashara za wengi kwenye ulimwengu wa roho.

Watu walikuwa na madhabahu zao kubwa ambazo ziliprovide ulinzi wa pesa na mali, pia zikikuwa zikivuta mali kutoka kwa maboya wengine.

Alipofika Kimaro, wale ambao tulikuwa tukizivuta mali zao, wakaanza kumiminika kule kila alfajiri, ulinzi wa mali zao ukaanza kuongezeka, na zile biashara zao ambazo tulizifanya zisionekane na wateja zikaanza kuonekana, na taratibu taratibu wakaanza kukua na kutupora wateja wetu.

Kwa msio na ufahamu wa biashara, hamna biashara isiyo na madhabahu (iwe ya asili au hizo kama za Kimaro), hamna biashara isiye na kuhani, na wala hamna biashara isiyotolewa sadaka/kafara.

Watu wakaanza kufundishwa kutoa sadaka za maneneo na manuizi kwa ajili ya biashara zao, tukapata upinzani sana.

Kwa kushirikiana na wenzetu ndani ya kanisa, tukaanza figisu. Ibada hizo mpya zifutwe na ikiwezekana Kimaro ahamishwe Kariakoo.

Tukafanya Kimaro apitie magumu, tukakausha kabisa hali ya utoaji wa sadaka hadi kanisa likashindwa kulipia umeme na maji, tukahakikisha wanapitia kwenye hali ya ugumu kweli kweli.

Baadae Kimaro anajua alichokifanya, akapindua meza, hali ya uchumi wa kanisa ikaimarika sana, likawa pigo lingine kwetu.

Kipindi kile mkuu wa kanisa alikuwa yule jamaa wa Mbeya, tukafanya kila liwezekanalo ahamishwe. Ndipo akapelekwa Kijitonyama.

Zama zile Kijitonyama alikuwepo dogo mmoja anaitwa Kinyaha, hayo mambo ya ibada za asubuhi yalikuwa hayapo au yamekufa kabisa.

Ibada ilikuwa ikihudhuriwa na vizee vienne, wakizidi sana sita. Sasa alipokuja Kimaro sijajua alikuja na mguu upi, akaleta ibada za asubuhi na usiku.

Watu wakaanza kufurika, akaanza kununua nyumba za watu wetu na kuzifanya kuwa za kanisa. Kijitonyama yote ilikuwa ni ngome yetu.

Kata ya Kijitonyama ndio kata ina vijiji viwili mjini kati Dar es Salaam. Kijiji cha Mwenge na Kijiji cha Makumbusho. Jina na asili Kijitonyama sitaki kulielezea leo, lakini kaa ukijua kuwa ile ni ngome yetu na sehemu yetu ya kulia nyama na vitu vyetu vya kutuongezea nguvu. Kijitonyama ndiko kwenye madhabahu ya kuteketeza, ndio maana hata Wahindi miili yao huchomewa Kijitonyama.

Pale tulijaribu mbinu za kishushu, kuna kipindi tulitaka kumfitinisha na serikali kwa kupitia kijana aliyejinyonga kwa madeni aliyokuwa nayo, lakini alikwepa vihunzi kwa namna ya ajabu kabisa.

Kwetu sisi ni furaha, watu waharibifu aina ya KIMARO hawafai, wakakae huko vyuoni wafundishe. Na tutammaliza kwa njia hiyo.
 
Watu hawafati umaarufu bro umewaza kitoto sana watu wanafata mafundisho. Ukiangalia wote wanaotajwa ni watu wamafundisho ss ukiwa unapiga mondo mno lazima wakubwa wajisikie vibaya. Never outshine your master. Ss unafikir ni uongo vijana wengi wa kikristo sio waaminifu katika biashara. Nenda kariakoo 80% ya maduka utakuja na akina Amiii, Asha, Shabani so asichukuliwe vibaya alilosema ni kweli tubadilike tu.
Ukitoka Kariakoo pia ,uende Mahabusu na magereza ujue vijana waliopo kul3 ni kina nani!
 
Ukikaa na kufuatilia comments humu utawaonea huruma vijana na kanisa la sasa. Kanisa ni taasisi na mtu akifanya kitu nje ya taasisi inatakiwa kanisa kama taasisi limuweke sawa regardless na yeye alivyo. Ukisoma comments nyingi wazi wanaishambulia taasisi kuwa ina makosa na mchungaji yupo sahihi.

Mi natumika TAG na tunapomaliza vyuo vya Biblia na tunapowekewa mikono kwenye huduma tunaambiwa tuizitii mamlaka zilizopo juu yetu kwa TAG tuna kanisa la mahali pamoja, sehemu(section), Jimbo na Taifa. Pamoja na kwamba ni kweli tunaongozwa na Roho a Mungu ila kanisa kama taasisi ya kibinadamu inatakiwa iwe na utaratibu wake. Nifahamuvyo, hakuna kanisa linaloweza muonea Mchungaji wake kwani kuna vyombo vya maamuzi vilivyo jengwa na katiba ya kanisa. Sijui huko Lutheran ila kwetu iwapo kutatokea changamoto, utaratibu wa kuishughulikia huanzia sehemu (section) then jimbo na ilishindikana huko au mmoja hajaridhika na namna changamoto ilivyotatuliwa anaweza ifikisha Taifani.

Naamini Kimaro kuna sehemu hakuwa sawa hawezi onewa eti Kawa maarufu kuliko kanisa. Nifahamuvyo, huduma za kanisa limejengwa katika utaratibu na unyenyekevu na ukiangalia comments nyingi za humu zimejengwa kwenye ufuasi na ushabiki ambalo ni tatizo linalolila kanisa la vijana wa sasa. Ufahamu wa mambo ya kiroho kwa sasa kwa vijana ni mdogo sana na umejengwa kwenye ushabiki na ufuasi wa mtu binafsi na sio katika Kristo Yesu aliye Neno la Mungu. Mungu atusaidie sana kwa kweli.
 
Mimi nimezaliwa katika familia ya KKKT anakubatizawa , kupata kipaimara ndani ya KkKT, Kama kuna kitu huwa sikubaliani ni hili suala la kalenda, Mungu anatoa jumbe tofauti,kwa watu wake on his own will kupitia hao watumishi wake wachungaji ,naona kama ile kalenda ina limit that will of God kwa siku husika kwa watu wake ....
Calendar inasema wazungumziee na sadaka kila mahubirii sijui[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yani sadakaa inaongelewa mpaka unasema bhasii.
 
Mimi ni muislamu lakini nasema huyu Pastor Kimaro ni bonge la Pastor na waliomfanyia hizo figisu hawana roho wa Mungu ndani yao.

# Baba Kimaro kama unasoma UJUMBE huu please tunaomba tunaomba ufungue kanisa lako.

Siku 60 ni nyingi sana.

😭😭😭😭😭😭
😆😆😆!
Nimecheka sana waalah!
Muislam, hayo mambo ya ndani ya KKKT yanakuuma nini?
 
Calendar inasema wazungumziee na sadaka kila mahubirii sijui[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yani sadakaa inaongelewa mpaka unasema bhasii.
Nyie tu vijana wa sasa mna mtazamo hasi kuhusu kutoa. Sijawahi kuona mtu amefirisika kwa kutoa sadaka. Mbona kwa waganga wa kienyeji mnatoa sadaka? Relax bro.
 
Nyie tu vijana wa sasa mna mtazamo hasi kuhusu kutoa. Sijawahi kuona mtu amefirisika kwa kutoa sadaka. Mbona kwa waganga wa kienyeji mnatoa sadaka? Relax bro.
Elewa point kwano wasipozungumzia watu hatutoi?? Yani sadaka inakuwa kama ndo lengo la kwenda kanisanii.
 
Ungeelewa kwanza ulichokiandika ndipo uniambie nifafanue hoja yangu.

Kumpokea Yesu awe Bwana na Mwokozi siyo MAPOKEO bali ni kukiri Imani na ondoleo la dhambi.

Yesu hakuwa anarudia rudia mambo kwenye huduma yake. Angalia orodha ya vipofu aliowaponya utaona kila muujiza ulikuwa wa kipekee.

Aligeuza maji kuwa divai kwenye muujiza wake wa kwanza lakini kwenye karamu ya mwisho ilitengenezwa divai isiyotiwa chachu


Kumzoea Mungu ndo huko kwenda kanisani kufanya mambo ya kukariri yanayojirudia rudia.
Bado unajizungusha kwenye mstari ule ule ,kwamba kadri miaka inavyosonga basi utaratibu na namna ya kumuabudu Mungu lazima vibadilike na ndio uamini Mungu yupo?Mungu ni wa utaratibu na hata Yesu alifanya mambo kwa utaratibu,na kanisa limeweka utaratibu wa kuabudu kama huridhiki nazo,tafuta unapoona ni sawa
 
Ondoa kashfa zako!unaposema vijikanisa unamaanisha Nini?unajua taasisi ya pili kwa ukristo hap tz ni hii?Mungu ndiye mmiliki huwezi kumzidi
Una uhakika gani Mungu ndio ana umiliki wa kkkt?msimuingize Mungu kwenye mambo yenu ya ajabu ajabu
 
Shida ipo hapa naona KKKT haitakiw transformation Kuna moto wa injili unawachukua taratib wataukua wanaabudu kama walokole. Nilionaga padri mmoja akiomba mapepo yanalipuka ss chakushangaza alipigea chini. Itafika hatua KKKT itakua injili ya moto kwelikweli .
Hizo hoja ni za miaka na miaka,zilipelekea kuanzishwa kwa vipindi vya jioni maarufu kama fellowshop kwa ajili ya wanaopenda kusali katika modality ya Kilokole.
 
Kuna shida sana Kati ya lituludia na wake wanaoongozwa na roho mtakatifu!
Ibada zozote zinazoongozwa na roho hazina utaratibu maalumu! From no where mchungaji anaweza kujiskia kuingiza Jambo Fulani na hapo kiroho yuko sawa.
 
Thanks for this, very insightful and objective, please share hiyo ya tarehe 8.
P
Kiufupi ni kwamba kulikuwepo na mashtaka kwenye ofisi ya dayosisi kumhusu huyu kimaro, sasa kwenye dayoysisi hakuwepo katibu mkuu wakti huo kwa hiyo wakamtafuta katibu mkuu wa mda ambaye walimteua mchungaji wa kimara, sasa alivyoenda ofisini akakuta kuna mashtaka juu ya rafiki yake kimaro, ikabidi afatilie na kujua chanzo cha mashtaka
Baada ya kujua chanzo akavujisha siri na kumwambia pasta kimaro
Kwa sababy kimaro hana mambo ya kuficha ficha akaja kanisani na kuanza kuporomosha vijembe kwa viongozi wake lakini akajisahau akamtaja mpk aliyepeleka mashtaka kule kwa matamshi yake akisema ni huyo Anna. Na wakati anamsimanga huyo mchungaji alikuwepo mbele, aliyoongea hata mtoto mdogo akimsikiliza atajua kwamba anamsema yule mchungaji na viongozi wa dayosisi. Kimaro inabidi tu akubali kiburi kinamsumbua na kujiona yuko juu ya wengine sababu ya umaarufu alioupata baada ya kufika hapo kijitonyama.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] wacha nicheke japo mimi ni mkristo hasa wa kipaimara humu makanisani mna vituko vingi mbali na hizi ibada zetu za liturjia
Usicheke mkuu ni mambo ya kusikitisha yanayo fanywa na wachungaji
 
Mm ni mkatoliki ila niliwahi kwenda huko kwa maksai kimara uko sahihi uzuri ni kuwa Nje ya maji Mamba hana nguvu
Kabisa mkuu, mambo yako wazi kabisa yanaonekana ila tu ni kushupaza shingo kunawasumbua watu.
 
Kam
Kama ile kauli ya kibaguzi ndo kaitamka kwa kinywa chake kuhusu vijana wa kiislamu na ki kristo sina cha kumtetea due ni kama amespoil image za watu ambao aidha kazin na wanaosaka mkate wao wa kila siku
Hakuna mwenye akili timamu anayeweza kumtetea huyu jamaa zaidi ya hao makanjanja wake, yeye aondoke aone kama kkkt itayumba au kutoweka. Taasisi ina misingi yake ukienda kinyume na hiyo misingi ujue unajiweka kando.
 
Back
Top Bottom