Mchungaji Kimaro: Afrika itakuwa ya kwanza kupona Corona itafuatiwa na Asia na wa mwisho watakuwa Israel (Wazungu)

Mchungaji Kimaro: Afrika itakuwa ya kwanza kupona Corona itafuatiwa na Asia na wa mwisho watakuwa Israel (Wazungu)

Mchungaji wa KKKT Kijitonyama Dr Kimaro amesema kwa mujibu wa maandiko ya Biblia Mungu alishaitangazia uponyaji wa kwanza Afrika yanapotokea maradhi ya kiulimwengu kama Corona.

Hivyo kwa mujibu wa Biblia Afrika itapona ya kwanza, itafuatiwa na Asia na mwisho watakuwa Israel kwa maana ya waxungu wa Ulaya na Marekani amesema mchungaji.

Mchungaji Kimaro amefanya maombi maalumu ya kuliepusha taifa kutoka janga la Corona na ameahidi Tanzania itakuwa kimbilio la dunia nzima kwani hata sayansi inaitambua Tanzania kama ni nchi na ardhi aliyoishi binadamu wa kwanza katika uso wa dunia.

Source Upendo tv

Nawatakia Dominica yenye baraka!
Hayo maneno ya Afrika kuwa wa kwanza kuponywa Corona yameandikwa kwenye Biblia yameandikwa kitabu gani?
 
Kuishi kwa kuamini miujiza wakati sayansi ipo pia ni jambo jema!!

Mimi naona hakuna haja ya kufundisha watoto wetu sayansi...
Badala yake tujenge makanisa ili watoto wawe na imani kwamba hakuna linaloshindikana kwa Mungu muumba mbingu na nchi.
 
Adam aliishi kwenye bustani ya Eden, ambayo iko Iraq!! Ndiko iliko mito iliyokuwa inaimwagilia bustani.
Unaijua vizuri ramani ya Tanzania? Unajua mito mikubwa ndani yake ilivyokaa? Unajua majina ya hiyo mito ya Iraq yalibadilishwa mwaka gani ili kuendana na majina ya mito ya Eden yaliyoandikwa kwenye Bible?
 
Adam aliishi wapi?
Aliishi kwenye bustani ya Eden, kwenye makutano ya mito miwili, Tigris na Euphrates. Hii mito ipo Iraq (Mesopotamia). Mto Tigris bado upo. Mto Euphrates ulikauka lakini channel bado ipo.
 
Aliishi kwenye bustani ya Eden, kwenye makutano ya mito miwili, Tigris na Euphrates. Hii mito ipo Iraq (Mesopotamia). Mto Tigris bado upo. Mto Euphrates ulikauka lakini channel bado ipo.
Hizo ni conspiracy theory tu. Unajua ni lini hiyo mito ilibadilishwa majina ili iendane na majina ya kibiblia? Palipokuwa na Eden mito yake haiwezi kukauka.
 
Tanzania kama ni nchi na ardhi aliyoishi binadamu wa kwanza katika uso wa dunia
Hakuna Mchungaji hapa; Kwa statement hii tu inaonyesha jamaa hana uelewa na Neno, Nafundishaje?
Ndio maana huwa nasema Huyu na Mgogo ni Motivational Speakers na si Waalimu/Wahubiri wa neno la Mungu kama wanavyojitanabaisha.
 
Hizo ni conspiracy theory tu. Unajua ni lini hiyo mito ilibadilishwa majina ili iendane na majina ya kibiblia? Palipokuwa na Eden mito yake haiwezi kukauka.
Eden haikuwahi kuwepo,,
Adamu hakuwahi kuwepo bali kuna mtawala mmoja wa Asyria aliitwa Adam,,
Story ya Adam imevuviwa na huyo jamaa Adam the asyrian
 
Kimaro amepata umaarufu sasa anaanza kuwa kama mzee wa upako. Soon ana kwenda kuaibishwa na Mungu. Aache siasa ahudumu kama mtumishi.
nasikia ana mpango wa kuhama kkkt na kuanzisha kanisa lake baada ya viongozi wa kanisa kuanza kutilia shaka ukwasi anaomiliki.
 
Back
Top Bottom