Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
Biblia inasema Mungu akasema " na tufanye mtu kwa mfano wetu"
Tufanye mtu kwa mfano wetu na sio tuumbe Adam awe mtu wa kwanza.
Adam ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kufanywa mfano wa Mungu, yaani yeye ndiye aliyefanywa na Mungu kuwa wa kwanza kuonyesha njia za Mungu kwa watu wengine katika zama zake, ndiyo maana ya kufanya, tofautisha kati ya kufanya/kufanywa na kuumba/kuumbwa.
Kwa kiarabu ni rahisi, fanya ni (ja'la) na kuumba ni (khalaqa).
Hivyo kauli hiyo ya Biblia ni sahihi kabisa na inafanana katika maana na kauli ya Qur'an inayotaka watu tujipake rangi ya Mwenyezi mungu, yaani tuwe na tudhihirishe sifa za Mungu katika maisha yetu hapa duniani hiyo ndiyo maana ya kufanywa kuwa mfano wa Mungu na si vinginevyo.