Mchungaji Mashimo ahukumiwa kwenda jela miaka 2 na miezi 6

Mchungaji Mashimo ahukumiwa kwenda jela miaka 2 na miezi 6

ni muda sasa amba rutty aoneshe fadhila aende akamuokoe huyu jamaa maana huyu ndo alimuokoa yeye kipindi kile. ila sasa wanawake walivyo🤔
 
Mashimo.jpg
Mchungaji Daud Nkuba, maarufu Komando Mashimo, amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia katika makosa mawili, kuingia kijinai katika ardhi isiyo yake na kuharibu mali.

Katika hukumu hiyo Komando Mashimo pia ameamriwa kulipa fidia ya Sh5 milioni.

Mashimo amehukumiwa kutumikia adhabu hiyo na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, leo Jumanne, Machi 18, 2025, kutokana na kesi ya jinai iliyokuwa ikimkabili mahakamani hapo.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalira, aliyesikiliza kesi hiyo, baada ya kuridhika na ushahidi wa upande wa mashitaka umethibitisha mashitaka hayo bila kuacha mashaka yoyote.
Mashimo 1.jpg

================

Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imemhukumu kifungo cha miaka miwili jela Mchungaji Daud Nkuba, maarufu kama Komando Mashimo au Nabii Mikaya, baada ya kupatikana na hatia ya kuharibu ujenzi wa nyumba mali ya Frola Mwashaa katika eneo la Mbezi Luis, Dar es Salaam.


Aidha, Mahakama imemtia hatiani kwa kuingia kwa jinai katika ardhi ya Frola Mwashaa, lakini imemuachia huru katika shtaka la kutishia kwa vurugu, kwa kuwa upande wa mashtaka haukuweza kuthibitisha shtaka hilo bila shaka yoyote.

Hukumu hiyo imesomwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalira, ambaye amesema upande wa mashtaka umethibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa kupitia mashahidi watano na vielelezo mbalimbali.

"Kwa shtaka la kuingia kwa jinai, mshtakiwa atatumikia kifungo cha miezi sita, na kwa kosa la kuharibu mali, atatumikia kifungo cha miaka miwili gerezani," alisema Hakimu Rugemalira.
Hata hivyo, Mahakama imeamua vifungo hivyo viende kwa pamoja, hivyo Komando Mashimo atatumikia kifungo cha miaka miwili pekee.

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Rhoda Kamungu, aliiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa jamii kwa ujumla.

Kwa upande wake, Komando Mashimo aliiomba Mahakama kumpunguzia adhabu, akidai ana familia inayomtegemea.

Komando Mashimo alishtakiwa kwa makosa matatu:

  1. Kuingia kwa jinai katika ardhi ya Frola Mwashaa mnamo Novemba 22, 2023, eneo la Mbezi Luis, Wilaya ya Ubungo.
  2. Kuharibu ujenzi wa nyumba ya Frola Mwashaa kinyume cha sheria.
  3. Kutishia kwa vurugu dhidi ya Ramson Vicent – shtaka hili lilikosa ushahidi wa kutosha, hivyo Mahakama ikamuachia huru.
 
Mchungaji Mashimo huwa ananifurahisha sana kwa jinsi anavyoongea na kusisitiza anachokiamini....

Binafsi nimepata huruma kubwa juu yake....

All and all atayashinda na yatapita kwani ndio dunia....

#Do Not Do Harm!
 

Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni chini ya Hakimu Rugemalila imemhukumu Daudi Mashimo kifungo cha miaka miwili na miezi sita jela baada ya kumkuta na hatia katika mashtaka mawili kati ya matatu yaliyokuwa yakimkabili.

Mashimo alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya kuvamia na kuishi kwenye eneo la mlalamikaji, Flora Jonasi, kuharibu mali kwa makusudi, na kufanya vurugu dhidi ya Ramsoni. Mahakama ilimkuta na hatia katika mashtaka ya mawili, huku ikimuondolea shtaka la moja ambalo wamekuta hana hatia.

Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mtuhumiwa ameshauri ndugu,jamaa na marafiki kukata rufaa ikiwa hawajaridhika na uamuzi huo.
Kwani Ubungo hakuna Mahakama??
Kosa kafanya Ubungo na kukamatiwa huko then analetwa Kino
 
Kuna wajinga wanaenda kupiga magoti kwa huyu mtu ili awaombee wasamehewe dhambi na wanampa sadaka wanasema wametoa kwa mungu.
 
Back
Top Bottom