Mchungaji Msigwa akiri kumsingizia Kinana ujangili, amwangukia na kumwomba radhi

Siasa za bongo sio za kuziamin ,wanasisa ni kma mwanaume anae mtongoza mwanamke kwa maneno matamu ya uongo akipata mzigo tu anakimbia zake
 
OhoooΓ²

Wanamtaka agombee urais!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angeomba kwa siri! Kuomba hadharan ina athari kubwa sanaaa! Wengi wataanza kuamini tuhuma nyingi kwa viongozi was serikali ni za kupikwa
Kinana aliweka Masharti ya kesi hiyo alipofungua hayo mashtaka, na mojawapo ni kuwa aombe msamaha hadharani, la sivyo angehitajika kumlipa mabillion ya pesa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiona msigwa anavyotoa povu bungeni eti namba hazidanganyi, huku vijana wa ufipa wamekaa kwenye visturi na vi pop corn na soda ya fanta wanakenua πŸ˜… sasa leo amekubali mwenyewe kuwa hudanganya mbele ya watanzania. Sasa wale Bavicha mko wapi mje mtetee na hili?

Karma imeanza kuwasurubu mnakuja wenyewe hadhalani kusema yale mdhambi, nina uhakika hata waliompiga Lisu muda si muda watatokea, labda washindwe tu kwa sababu watakuwa na kesi,
 
Ingekuwa busara kama angesema na mengine ambayo aliwasingizia watu na kuwapa tuhuma za uongo akiwa Bungeni.

Tabia ya kuokota maneno na kwenda nayo Bungeni kuwachafua watu ni tabia ya hovyo. Wengi wa wabunge huwachafua watu wakitegemea kinga na haki za Bunge.

Msigwa kasema mengi na huenda 90% yalikuwa na nia ovu. Naona leo anaongea kwa unyenyekevu kwa kuwa kakamatwa sehemu za siri, wakati anatuhumu alijifanya mwamba kumbe hana umwamba wowote.

Chezea damages kutokana na defamation, angetema mzigo wote wa kiinua mgongo. Ameomba msamaha kuokoa kiinua mgongo chake.
 
Wanasiasa wanaongea uongo sana kutafuta umaarufu na kushangiliwa bila kujali wanachoongea kina ukweli kiasi gani, wakikutana na Mangangari ndio wanaishia kutia huruma.
 
Kwahiyo mmedanganya mangapi?

Kama mnakiri maovu yote, kirini na muorodheshe yote.

Huyu atakuwa kalazimishwa na mahakama AU kuna mtu anatuliza njaa yake.
 
Retired una maoni gani baada ya hili?
Sijapenda, ni kosa kubwa kwa mtu mwenye hadhi yake kusema uongo au kusikiliza mambo ya vijiweni ukayaleta katika seroius matter!

Nadhani alifany hivyo kwa vile Tanzania imetawaliwa na chuki za wanasiasa kama unavyoona Chadema wanaumizwa!
 
Sanji sijui Kiviele sijui Chivele sijui Kayemba sijui wanasemaga mkaza-mpwa Au wameoleana...wapo walionielewa...πŸ˜€

Everyday is Saturday........................... 😎
 
Dah!...wanasiasa si watu wa kuwaamini kabisa, wabaya sana hawa binadamu.
 
Ni swala la Muda tu, binafsi ningependa huko wanakoenda wakapambane kwenye kura za maoni kwa nguvu zao bila usaidizi.

Hata hivyo inauma sana kuona Upinzani hasa Chadema ukimomonyoka kama mkate kwenye chai wakati chama kimejengwa kwa jasho na damu.

Mkuu kwani cdm ikifa utashindwa kufanya siasa au kusimamia unachokiamini? Cdm tuliitumia tu kuwakilisha mitazamo yetu maana ndio platform rasmi ya kufanyia siasa. Lakini sitaki kuamini eti unachokiamini kitaondoka kisa cdm itakufa.

Ni nadra kwenye nchi zenye mitazamo ya kikomunisti vyama vya upinzani kuwa na nguvu, na vikiwa na nguvu zitatumika mbinu halali na chafu kuhakikisha kinapoteza nguvu.

Uzuri wa sasa hivi misimamo yetu iko wazi bila hata uwepo chama chochote cha siasa cha upinzani.
 
Sijapenda, ni kosa kubwa kwa mtu mwenye hadhi yake kusema uongo au kusikiliza mambo ya vijiweni ukayaleta katika seroius matter! Nadhani alifany hivyo kwa vile Tanzania imetawaliwa na chuki za wanasiasa kama unavyoona CDM wanaumizwa!
Hii inashusha hadhi yenu kama wapinzani wa CCM. Too sad my dear friends.

Kila siku nawaeleza strength ya upinzani katika nchi yeyote ni kutamka kitu ambacho kimefanyiwa utafiti ili watu wawaamini.

Poleni sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…