Mchungaji Christopher Mkitila, akiongea na TUONGEE ASUBUHI kupitia Star Tv asubuh hii, amesema kuwa ni aibu sana IKULU kuifanya ICU ya Wagonjwa na mafisadi ambao wanataka kwenda kujifunzia pale, Lowassa ni mgonjwa hana uwezo wa kuwaongoza Watanzania kwa kuwa wapo watu wengi wenye Afya njema na hawana kashfa yoyote ya Ufisadi na maadili mabaya.
Akiendelea kuulizwa juu ya tathimini ya Uchaguzi kupitia Taasisi ya TWAWEZA amesema sio tatizo kwa maana tamwimu hazimlazimishi mtu kukipigia chama cha mapinduzi hivyo sio swala la msingi ila UKAWA sio sahihi kupewa Ridhaa ya kuwaongoza Watanzania.
Mchungaji ameendelea kusema kuwa Mficha maradhi kifo humuumbua, LOWASSA amekula pesa nyingi za Watanzania bila hofu hilo ndo tatizo lake sasa.