Zingatia kuna historia yenye ukakasi kumhusisha muumini huyu ambaye ni ofisa wa TAKUKURU (kama anavyojitambulisha mwenyewe).
Mchungaji kawekwa ndani na muumini wake.
Muumini huyu anakashfa nyingi zisizopendeza kanisani hapo. Muumini huyu ana misuguano na Mchungaji wake kanisani.
Bado haitoshi kuona mizania inalalia upande gani?
Ingekuwa heri, kabla ya kuandika bandiko lako ukajiridhisha na mambo mengi kidogo ya hayo uliyoyaandika:
1. Ni kweli mchungaji alilala mahabusu? Kama ni kweli, basi uko sawa na kama ni uongo! Kwa nini unaleta taarifa kuihadaa umma.
2. Je ni kweli mchungaji na huyu unayemwita muumini wake wanamsuguano? Kama ndivyo msuguano semwa unahusi nini hata mke wake ahusike kwa namna yoyote?
3. Je huyo afisa semwa, alikwenda peke yake au walikutana tu mtaani na yeye kumchukua mke wa mtumishi wa Mungu huyo? Fafanua vyema tupate taarifa kamili.
3. Shida ya daktari ilikuwa nini hata kukamatwa?
Imekuwa dhuluma hadi kwa watumushi wa Mungu. Raia wema wakimbilie wapi?
Katika hali ya kushangaza Mchungaji mmoja wa kanisa la wasabato wilayani Kahama na familia yake wamejikuta wakinyanyasika pasipokuwa na uhalali wowote kufikia kuswekwa ndani na kulala rumande.
Kadhia hii imemkuta mchunga kondoo huyu wa bwana wakati akimgombelezea mkewe mwenye kitoto kichanga ambaye ni mganga (Daktari) katika hospitali ya manispaa ya Kahama akijaribu kuepusha asikamatwe na TAKUKURU kimchongo mchongo.
Mganga huyo alikuwa amekumbwa na kadhia inayosemekana kuwa ni ya kubambikiziwa na kukamatwa na madawa ya binadamu kwenye pochi yake akiwa kazini.
Kwamba 1 March 2023 TAKUKURU walimzukia mama huyo, walipokuwa wamelazimisha kuwapekua wafanyakazi hospitalini hapo. Kwamba kwenye pochi yake walikuta madawa hayo. Jambo ambalo ni utata mtupu kwa wanaomfahamu.
Familia hiyo ya mume, mke na kichanga chao imejikuta ikisukumwa ndani na kulala selo kwa kinachosemekana ni kukamilisha majigambo ya baharia mmoja mchakata mbususu za waumini kanisani kwa mchungaji huyo.
Baharia huyo ambaye pia ni muumini katika kanisa la mchungaji huyo pia ni afisa wa TAKUKURU wilayani humo. Kutokana na tabia zake zisizokidhi vigezo amekuwa kero kubwa kanisani hapo huku akijigamba kuwa atawafunza adabu wote wenye kujaribu kumletea gozigozi.
Mchungaji alipoitwa na mkewe kuwa amepata tatizo, alikwenda kuishia kupewa kesi kuwa amewatolea lugha chafu vigogo hao (wa TAKUKURU) naye kuishia kusukumwa ndani.
Kweli kikulacho ki nguoni mwako.
Matukio ya waumini kanisani hapo kukumbwa na kadhia zenye kuishia watu kusukumwa ndani bila sababu za msingi yamekuwa mengi.
Kwa hakika afisa huyu mchakata mabinti weupe weupe kanisani hapo yaonekana amedhamiria kweli kweli.
Kauli yake mbiu ikiwa, hayupo wa kumfanya lolote.
Zingatia kuna historia yenye ukakasi kumhusisha muumini huyu ambaye ni ofisa wa TAKUKURU (kama anavyojitambulisha mwenyewe).
Mchungaji kawekwa ndani na muumini wake.
Muumini huyu anakashfa nyingi zisizopendeza kanisani hapo. Muumini huyu ana misuguano na Mchungaji wake kanisani.
Bado haitoshi kuona mizania inalalia upande gani?
Ingekuwa heri, kabla ya kuandika bandiko lako ungali jiridhisha na mambo mengi kidogo ya hayo uliyoyaandika:
1. Ni kweli mchungaji alilala mahabusu? Ni uongo! Kwa nini unaleta taarifa kuuhadaa umma.
2. Je ni kweli mchungaji na huyu unayemwita muumini wake wanamsuguano? Kama ndivyo msuguano semwa unahusi nini hata mke wake ahusike kwa namna yoyote na watu hawa wawili?
3. Je huyo afisa semwa, alikwenda peke yake au walikutana tu mtaani na yeye kumchukua mke wa mtumishi wa Mungu huyo? Na au walikwenda kama jopo kufanya kazi waliyokuwa wameagizwa na mkuu wao? Fafanua vyema tupate taarifa kamili.
3. Shida ya daktari ilikuwa nini hata kukamatwa? Je alikamatwa peke yake au na wengine, kama walikamatwa zaidi ya mmoja kwa nini mke wa mchungaji ndiye unayemsema na sio wote au wengine haifai kuwasemea?Mkuu, hebu toa taarifa kamili juu ya hili.