Baadaye utajua hujui!
Kwani umetumwa na nani?
Aliyekutuma ndio kakupa hiyo taarifa?
Unaandika bila kuchunguza mambo, na kuonyesha udhaifu na ufinyu wa upembuzi wa taarifa uliyopokea!
Acha kulichafua kanisa na waumini wake kwa sababu za kuhisi!
Halafu hilo jina mbona halifanani na wewe! WEWE ULIPASWA KUJIITA "MLAUDEKIA"
Mie ni binadamu so naweza kuwa yeyote na wala sio lazima niwe kwenye hiyo orodha yako!
Leta ushahidi wa hao weupe, weka na picha zao tuuone huo weupe walio nao, labda naweza pata jiko la pili hapo!
Vyeupe mwilini kwangu ni macho ukiondoa mboni za zake. Hata hivyo, weupe ni moja kati ya rangi zisizo na thamani kwani wanaozitaka huzinunua kwa mafuta ya kupaka na wengine kwa vidonge... weusi wangu ndio rangi halisi kwangu.
Akili nyingi haihitaji nguvu nyingi kuelewa.
Naona umekuja na kufungua akaunti mpya kwa ajili ya uzi huu sijui utaendelea 🙄?
FAFANUA VYEMA NA MIMI NIPATE TAARIFA KAMILI kulingana na nilichokuuliza hapo awali, ACHA KUFUNIKA MASHIMO KWENYE BARABARA YA LAMI KWA KUTUMIA MCHANGA!🚮🚮
Post zako mbili namba 51 na namba 57 hazikanushi kuwapo kwa tatizo ambalo ndilo lililo la msingi.
Bila shaka nilichoandika namba 53 na namba 61 kinajieleza.
Nikukumbushe haikuwa rahisi kuufikisha ujumbe huu ndani ya vigezo vyote vilivyoelezwa.
Kwa kweli ukuu wa Mungu dhidi ya uovu umejidhihirisha.
Inafahamika tambo zote za aliyetaka kumtia adabu mchungaji zimeyeyuka na mlipo mnahaha kulizima soo hili kwa namna yoyote. Mwovu hakuwa ameyakadiria maji sawa sawa. Hakujua JF, ikibidi watu huongea kwa uwazi.
Inafahamika kuna mkutano wa usuluhishi umefanyika. Inafahamika kufuatia uzi huu kuna jitihada za yule mwovu nyuma ya pazia kutafuta kanusho la hadaa toka kwa wahusika kwa ahadi kadhaa wa kadhaa.
Mungu mkubwa ngoja tuone.
Nirudi kwenye post yako hii mpya:
Post hii inafanana na mbili zako za awali kwenye kuwa zimeandikwa zikibeba hasira kali na maneno matupu.
Post hii inatofautiana na mbili zile kwenye kuwa juu yake kuna vitisho, aya zake zimenyumbulishwa na haina makosa makosa ya kiuandishi.
Haimchukui mtu muda kufahamu mbili zile na moja hii zimeandikwa na watu wawili tofauti walioguswa kisawa sawa ...
Ashukuriwe kwa yote baba wa mbinguni bwana wa majeshi.