John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Je, umeshawahi kuishi nchini Urusi au umewahi kuishi pamoja na Warusi? Au kuwahi kuishi kwenye moja ya nchi ambazo ni washirika wa karibu na Urusi? Hayo ni mambo ya kawaida kabisa kufanyika huko kwenye hizo nchi, hususani kwa Watu maarufu wenye ushawishi mkubwa kwenye jamii wamekuwa wahanga wakubwa Sana wa kufanyiwa matukio kama hayo.Kwani kumharibia mtu ni rahisi kiasi hicho?
Mawakala wa Ujasusi wa KGB/FSB wamekuwa hodari sana wa kupanga na kuratibu matukio ya namna hii nchini Urusi na kwenye nchi zingine ambazo ni washirika wake. Ili uweze kuishi kwa usalama na amani ni lazima ukiwa kwenye nchi hizo upate 'intelligence briefing' ya kutosha na ya kina kabisa ili uweze kujihami dhidi ya 'mashambulizi ya namna hii.' Kumbuka; hata Mabalozi wa nchi mbali mbali za kigeni pamoja na Wanadiplomasia wa kigeni waliopo kwenye nchi hizo pia nao wamekuwa wakiwindwa au kufanyiwa matukio ya namna hii. Aidha, hata 'wavaa kaunda suti' wengi zaidi waliopo hapa Tanzania nao pia wamechukulia Mafunzo yao ya 'umahiri' huko huko nchini Urusi, so take care!