KULAWITI.
Bashir Yakub, WAKILI
+255 714 047 241.
1. ADHABU YAKE.
Kifungu cha 154 Kanuni za Adhabu, Sura ya 16, Adhabu ya kulawiti ni Kifungo cha Maisha jela, au miaka isiyopungua 30 jela.
Kujaribu(attempt) kulawiti adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka 20.
2. USHAHIDI WAKE.
MOSI
Mahakama ya Rufaa katika kesi SELEMANI MAKUMBA vs JAMHURI, (2006) TRL 379 inasema kuwa ;-
"Ushahidi mzuri unaohusu Makosa ya Kujamiiana(sexual offences) ni ule unaotoka kwa mtendewa/muathirika mwenyewe(victim)."
Maana yake kile anachokisema muathirika ndio ushahidi mkuu na wa maana zaidi mbele ya Mahakama kabla ushahidi wa mtu au kitu kingine chochote.
PILI.
Kifungu cha 127(7) cha Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6 kinasema kuwa ;-
Ushahidi wa muathirika/mtendewa wa makosa ya kujamiina, kama utatolewa vizuri, na shahidi akawa ni wa kuaminika(credible witness), basi unatosha peke yake bila kuhitaji ushahidi mwingine wowote( collaboration) kumtia mtuhumiwa hatiani na kuadhibiwa na mahakama.
Muathirika akitoa ushahidi mzuri imeisha.
3. VIPI KUHUSU USHAHIDI WA DAkTARI.
Katika kesi ya C.D. DE SOUZA vs B.R.SHARMA(1953)EACA 41 na maamuzi mengine meengi ya Mahakama ya rufaa, Ushahidi wa daktari ni MAONI tu(opinion).
Watu hujua ushahidi wa daktari ndio kila kitu,hapana. Ushahidi wake ni maoni tu.
Kwakuwa ni maoni, basi Mahakama inaweza kuukubali au kuukataa.
Na hata ushahidi wa daktari uwe sahihi vipi hauwezi kusimama peke yake kuthibitisha ulawiti, mpaka usaidiwe na ushahidi mwingine hasa wa mtendewa.
Mwisho, kuna vijana wa mjini wanajua kumuingilia mwanamke girlfriend wako au mke wako kinyume na maumbile sio kosa. Wanajua kosa ni mpaka iwe mwanaume kwa mwanaume.
Acheni ujinga mtaenda jela, hilo ni kosa. Na ni kosa hata kama ameridhia. Akiridhia nyote mpo kwenye makosa na mnakabiliwa na kifungo cha miaka 30 au maisha.
Msiseme sikuwaambia.