Mdada unaolewa huwezi kupika wala kufua kiafrika, hii imekaaje?

Mdada unaolewa huwezi kupika wala kufua kiafrika, hii imekaaje?

Unampeleka binti kwenu , mtihani wakwanza mama anamwambia ampikie chakula fulani Tena ni chakawaida kabisa. Binti jashi Lina mtoka. Anahangaika huko anakuja kuja kuleta mezani chakula chaajabu hapo yupo mama baba na dada ZAKO. Aibu ya mwaka!!
Huu mtihani wengi hua wanafeli na kinachowafelisha wengine sio kwamba hawajui ila wanakua na kitete chakula ambacho hakipaswi kua over cooked ana over cook mpaka anaunguza

bi mkubwa anaangalia anasema wewe unaenda kumlisha mikaa mwanangu shenzi hujui kupika
 
Kuna michezo ya kitoto ilikuwa ni msingi wa kuja kuwa imara ukiwa mkubwa na unawajibika vema na familia yako uliyoianzisha. Watoto walicheza kinyumbanyumba, kujipilikisha udongo/mchanga na baadaye chakula cha halisi. Huko kinyumbanyumba kuna mama na baba, mengine waliyoyafanya ni zoezi tosha ukubwani na usitake nikuambie siri za michezo ya utotoni. Sasa kama mtoto hajapitia mambo ya umama mama na ubaba baba si ukubwani akiingia ndoani ataonekana kituko? Mambo mengi muhimu ndani ya unyumba alitakiwa ayajue na kuyafahamu tangu akiwa mtoto, si vibaya na si dhambi, asili ndivyo ilivyo
 
Mimi mwanamke wangu akipika, apike kwa kujisikia mwenyewe Akisema leo sitaki kupika, sawa tu, anunue chakula nje kwa hela yake, sina noma kabisa. Ila kama vitu vya kula vipo ndani halafu unaamua kununua nje kwa hela yangu, hapo tutakaa chini tuongee 😂😂.
 
Kuna mmoja alitia aibu uchagani, hajui kupika ndizi, alipika zile ndizi kubwa mkojozi, wenzake wakamcheka wakamuambia hizo ndizi hazipikwi, wakamfundisha aina za ndizi za kupikwa
 
Mgonile wadau,
Mdada anakuja kwako kukusalimia ,umeandaa vyazi nyama na mazagazaga kibao unajua Leo umempata mtu WA kupika chakula kizuri. Anakuambua agiza chakula yeye hawezi pika anatoa visingizio kibao kumbe hawezi kupika
Unampeleka binti kwenu , mtihani wakwanza mama anamwambia ampikie chakula fulani Tena ni chakawaida kabisa. Binti jashi Lina mtoka. Anahangaika huko anakuja kuja kuleta mezani chakula chaajabu hapo yupo mama baba na dada ZAKO. Aibu ya mwaka!!
Shida hapa nini , malezi au uzungu mwingi.
Sifa kubwa ya mwanamke WA kiafrika ni kusimamia nyumba yake. Yaani familia wale washibe Tena chakula kilichopikwa vizuri. Hapo ndugu jamaa na marafiki watakusifia Kwa kuoa mke bora
Gentleman,
ikiwa wewe unajua kupika,
nadhani unaweza kuchukua muda wa chini ya wiki tu, kumtrain huyo binti kupika chakula ukipendacho na mambo mengine ya ziada yakasonga as family.

Hata kama wew ni mfanyibiashara na yeye hajui biashara, unaweza kumpa training ya muda fulani na akawa na experience ya biashara na kisha as family mkawa mnasaidia majukumu na kazi hizo za kifamilia 🐒
 
Shule, tuition, homework, chuo, and labda baadaye kazi/sjira/biashara.

Unatarajia ajifunze muda gani wakati nyumbani kuna house girl anayetakiwa kuhakikisha kila wakitoka kwenye mizunguko hiyo wakute chakula tayari?
Kwa kukusaidia ni kwamba, ukiamua kuoa bint wa aina hiyo lazima sehemu ya mfumo wa maisha aliyokuwa akiishi kwao ui adopt pia kwake ili aendelee kuwa Mwanamke yule uliyempenda na kuvutiwa naye, ndiyo maana tunapohamisha mmea uliiota ili kwenda kuupandikiza kwingine huwa tunahamisha mmea na sehemu ya udongo wa hapo ulipokuwepo huo mmea.

Kimgine ni je, unaoa mwanamke wa kisasa au umeenda kuoa miaka ya 80?
Akaolewe huko chuo na assignment
 
Mtego mkubwa na muhimu kwa mwanamume aliye kwenda JANDO ni tumbo kwanza halafu ndio sex.
Kama atashindwa kukupikia basi omega showgal aka showroom
 
jimama kubwa halijui kupika ulipeleke VETA kwa nini? VETA mbali, afundishwe na majirani au we mwenyewe mwanaume mfundishe kupika
Majirani sio jukumu lao kumfundisha na wala hawana athari ya moja kwa moja na kutokujua kupika kwake.

Jamaa kitendo cha kuja jukwaani ni ishara tosha hafahamu kupika, vitu ambavyo anatarajia kupikiwa.

Hivyo veta inabaki kua chaguo sahihi kabisa, au sehemu yeyote ile inayotoa mafunzo ya kupika mahoteli na kadhalika, yani hapa binti alipiwe hizo gharama akirudi hata wana jf tunaweza alikwa kuwakilisha kula misosi ya kigeni
 
Mtego mkubwa na muhimu kwa mwanamume aliye kwenda JANDO ni tumbo kwanza halafu ndio sex.
Kama atashindwa kukupikia basi omega showgal aka showroom
na ndio maana wanawake wa ndoani walizingatia sana lishe kwa waume zao. Walijua waumd zao wakipata lishe watapeleka moto kisawasawa
 
Back
Top Bottom