Swali la pili,
Bajeti tunategemea misaada kutoka nje, utafanyaje ili tujitegemee kibajeti
Swali la tatu
Swala la Meremeta atalishughulikiaje
Swali la Nne,
Sijalipata vizuri swali hili, wanakwenda faster faster sana,
just imagine typing while others are talking!!!
Swali la tano,
Kuhusu uhusiano wa kimataifa siku za nyuma tuliheshimika ila sasa hakuna heshima sana
Majibu.
Swala la utegemezi.
Ukitegemea mishahara yako ilipwe kwa njia na misaada umeua kila kitu, Upinzani bungeni ulitegeneza Budget mubadala, ila bunge na serikali wakapuuza. Walipata Trilioni zaidi ya mbili bila kumtegemea Muhisani, ila serikali ilipuuza.
Kuhusu meremeta, Sina undugu, sina urafiki na mtu yeyote anayehujumu rasilimali za nchi hii, anasema anazo data zote, kuanzia check number na mahali zilipo, anasema watu wote wazirejeshe kabla ya tarehe 31 october.
Anamshangaa Kikwete, watu wanatuhumiwa yeye anakwenda kusema huyu ndio mchapakazi, anasema hiyo inaondoa credibility ya serikali.
Amewashukuru vyombo vya habari kwa kuamsha watu juu ya mambo ya ufisadi.
Anakumbushia msemo wa kikwete huko nyuma kwamba kelele za Slaa hazimkoseshi usingizi. Anasema Kikwete na Serikali wamepata kigugumizi juu ya swala la Kagoda, kila document ipo.
Anasema Mkapa alifanya kikao na Rostam, ndio chanzo cha Kagoda, anasema kikwete lazima apate kigugumizi kwa kuwa documents zote zipo, pesa zilikwenda kampeni za CCM.
Swala la Meremeta anampiga madongo Pinda kwa jinsi alivyosema ni swala la Jeshi Bungeni, Anasema Bilioni 155 lazima tujue zilienda wapi kwa kuwa ni za umma, si za kikwete, si za serikali, na hakuna jiwe litaachwa bila kupinduliwa,