Elections 2010 Mdahalo wa Dr Slaa Movenpick LIVE

Elections 2010 Mdahalo wa Dr Slaa Movenpick LIVE

Nimemsikia vizuri Dr. Slaa na namwombea apate urais ila siku anaingia Ikulu atakumbana na mambo mengi mno ambayo anaongea kama ni rahisi kumbe sio rahisi hivyo.

Haongelei serikali kuandaa mazingira ya wananchi kujiletea maendeleo yao bali serikali kuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa wananchi wake. Hayo mambo yalimshinda Nyerere pamoja na uaminifu wake wote.
 
kuna jamaa kauliza swali kwamba kwa nini wameteua Chadema mgombea mwenza darasa la 7, kuna Green card kwenye huu mdahalo!
 
dahhh recurrent expenditure...uwiiiiiiiiiiiiiiiiii wapi madaftali yangu ya book keeping..mshahara ni consumptive....dahhhh hivi vitu anasoma mahali au
Asome wapi! Kwani yeye ni Kikwete!!!!!
 
Kuhusu swala la Mafisadi. Anasema hana udugu hana urafiki kwenye rasilimali za taifa. Mgombea wa CCm anawakumbatia watuhumiwa wa ufisadi. Yeye ndio alizitoa bungeni. JK alisema kelele za Slaa hazimyimi usingizi. Kagoda wamepata Kigugumizi. JK aliiingizwa ikulu na Kagoda. Wanasema meremeta ni ya Jeshi. Bilioni 155 zilienda South africa lazima tuzijue. Hakuna Jiwe litaachwa kupinduliwa.
 
Swali la pili,

Bajeti tunategemea misaada kutoka nje, utafanyaje ili tujitegemee kibajeti
Swali la tatu
Swala la Meremeta atalishughulikiaje
Swali la Nne,
Sijalipata vizuri swali hili, wanakwenda faster faster sana, … just imagine typing while others are talking!!!
Swali la tano,
Kuhusu uhusiano wa kimataifa siku za nyuma tuliheshimika ila sasa hakuna heshima sana
Majibu.

Swala la utegemezi.
Ukitegemea mishahara yako ilipwe kwa njia na misaada umeua kila kitu, Upinzani bungeni ulitegeneza Budget mubadala, ila bunge na serikali wakapuuza. Walipata Trilioni zaidi ya mbili bila kumtegemea Muhisani, ila serikali ilipuuza.
Kuhusu meremeta, Sina undugu, sina urafiki na mtu yeyote anayehujumu rasilimali za nchi hii, anasema anazo data zote, kuanzia check number na mahali zilipo, anasema watu wote wazirejeshe kabla ya tarehe 31 october.
Anamshangaa Kikwete, watu wanatuhumiwa yeye anakwenda kusema huyu ndio mchapakazi, anasema hiyo inaondoa credibility ya serikali.
Amewashukuru vyombo vya habari kwa kuamsha watu juu ya mambo ya ufisadi.
Anakumbushia msemo wa kikwete huko nyuma kwamba kelele za Slaa hazimkoseshi usingizi. Anasema Kikwete na Serikali wamepata kigugumizi juu ya swala la Kagoda, kila document ipo.

Anasema Mkapa alifanya kikao na Rostam, ndio chanzo cha Kagoda, anasema kikwete lazima apate kigugumizi kwa kuwa documents zote zipo, pesa zilikwenda kampeni za CCM.
Swala la Meremeta anampiga madongo Pinda kwa jinsi alivyosema ni swala la Jeshi Bungeni, Anasema Bilioni 155 lazima tujue zilienda wapi kwa kuwa ni za umma, si za kikwete, si za serikali, na hakuna jiwe litaachwa bila kupinduliwa,
 
Mazee. Dr. Slaa kwa kweli anaongea kwa confidence na intellect ya hali ya juu. Mkuu GQ ahsante bongoradio juu......

Kuna mtu anayeangalia TV anaweza kuconfirm kama dr. Slaa anasoma mahali au anaongea kutoka kichwani?? Kazi kweli kweli
 
mhhhh ..kapangua swali la mgombea ni darasa la 7 ...katiba inaruhusu...duuuuh hiki ni kifaaaa aiseee
 
kuna jamaa kauliza swali kwamba kwa nini wameteua Chadema mgombea mwenza darasa la 7, kuna Green card kwenye huu mdahalo!
Anajibu.....wametumia katiba ya leo ambayo haimzuii inasema maadam ujue kusoma na kuandika kiswahili na kiingereza. Katiba inamruhusu na ana uzoefu! Sifa ya uongozi sio elimu pekee, ni uaminifu na uadilifu wake.
 
Jinsi Chadema inavyodhamilia kurejesha sura ya tanzania kimataifa,
Tunachafuliwa sasa na ufisadi, tunahitaji viongozi wasafi, viongozi wale wanaangalia maslahi ya taifa.
 
Anajibu.....wametumia katiba ya leo ambayo haimzuii inasema maadam ujue kusoma na kuandika kiswahili na kiingereza. Katiba inamruhusu na ana uzoefu! Sifa ya uongozi sio elimu pekee, ni uaminifu na uadilifu wake.


daaaah huyu mzee ni balaa
 
Back
Top Bottom