Maswali yanaendelea
Swali, unatarajia kutawala kwa miaka mitano tu je itawezekana?
Swali, nchi yetu imeumizwa sana na utaratibu wa wafanyabiashara kuwa wanasiasa. Aliyeko madarakani alisema angetenganisha ila ameshindwa je utafanyaje?
Swali, je utakapo apishwa, vipi kuhusiana na ongezeko la mishahara ya wafanyakazi?? Je wastaaafu wa Afrika mashariki wanaomwagiwa maji ya kuwasha utawasaidiaje?
Swali, Mipango yako kwenye ushindani wa East Afrika community, je utaiondoa Tz kwenye EAC.
Swali, mikutano inawafuasi wengi sana je hawa watanzania wote unawaandaaje kupokea furaha ukishinda, je pia unaandaje ikiwa utashindwa.
Swali, tunahitaji baraza la vijana je ukiingia madarakani utatusaidiaje kwa hilo
Swali, nasikia Tanzania ni nchi ya mwisho kwa umasini duniani, je kigezo ni nini, na utafanyaje kuondoa hilo, je ni kweli sisi ni masikini?
Swali, umezungumzia rasilmali za madini, je raslimali nyingine vipi???