Elections 2010 Mdahalo wa Dr Slaa Movenpick LIVE

Elections 2010 Mdahalo wa Dr Slaa Movenpick LIVE

Mdahalo ulikuwa umetulia na haukuchakuliwa. Jamaa kwa kweli anafaa kuwa rais sio Kikwete ambaye hata uwezo wa kujieleza hana.
 
Asante sana Bongo Radio na Mwanakijiji kwa kutuwezesha kumsikiliza Dr. Slaa, ambao hatukuweza kutazama matangazo hayo.
 
. Asante mkuu.

Prof. Azaveli anasema yeye ni mwanachama mfu wa CCM. Je ni wangapi wanachama wafu wengine ndani ya CCM ambao wako kimya?.

Wako wengi hata walio hai nao wengi wako kimya sana tuu.
 
Aisee nampa hongera Dada rose mwakitwange ameutawala mkutano vizuri na inaelekea kulikuwa na mamluki wengi ndani ya mdahalo.
 
Huyu jamaa ni genius leo kaburi ya Nyerere litakuwa limevibrate
 
kwa mara ya kwanza nimetoka machozi leo mara baada ya kusikiliza hii kitu
 
Rais Dr. Slaa hongera na pole sana kwa maswali na pilika za kampeni. Mwenyezi Mungu akibariki na kukulinda. Amina.

Asante wote walioshiriki kuleta matangazo haya.
 
Amejibu hoja kwa umakini na uelewa mkubwa. Tuwahamasishe wenzetu kupiga, na kulinda kura.Mungu ndiye muweza na kwa neema yake Dr. Slaa atashinda.
 
Slaa akichukua nchi narudi TZ, nimechoka kukaa kwenye nchi za watu
 
Shukrani mzee mwanakijiji na Bongo radio kwa kuweza kufanikisha matangazo ya leo, na kama ulivyoahidi itakuwa ni vizuri kama utaweka clips za mdahalo huo you tube
 
Anaongelea nyumba za Tembe na Majani, mtu ananyumba imekaribia kuanguka lakini ameweka picha ya chagua kikwete, anashangaa sana.
Dr. ana data ya pesa ambazo CCm wamelipia mabango na hayajalipiwa ushuru, anasema kama haya yanawezekana kutapanya mabango nchi nzima, je elimu ya mtoto wako haiwezekani,

Kama unaweza kwenda kunywa chain a obama, kwa nini useme elimu bure haiwezekani?
Dr. anasema yuko tayari kula mihogo ikulu ila elimu iwe bure.
Anasema pesa ziko zimesambaa kote kwenye idara za serikali, kinachotakiwa ni uwajibikaji. Anasema kila mahali kuna uchafu, miezi ya kwanza ni kurekebisha na kurejesha uwajibikaji. Kwenye swala hili ametoa mifano kibao alipokuwa somewhere mawilayani.

Anataarifiwa kuwa zimebaki dakika saba, anatoa points za mwisho mwisho

Anawashukuru sana watanzania
Anawaomba radhi majimbo ambayo ameshindwa kufika leo kwa sababu ya wimbi zito
Anasema katika siku 71 ni vigumu kufika majimbo yote hata kwa kutumia helikopta, ila anawaomba wote kura zao.
Anasema yeye hataki kuona damu ya mtanazania inamwagika
Anasema Tanzania itakuwepo hata baada ya uchaguzi
Anasema kwa siku nane zilizobaki, ukipigwa kofi basi geuza la pili maana hautakufa
Anasema, ukitaka kumuumiza aliyekupiga, wewe mpuuze, inauma zidi ya kulipiza kisasi
Anamwomba kikwete awe makini, anasema vurugu zitaletwa na serikali, na polisi na watendaji wengine, ametoa mifano ya mwanza, ambapo hakulindwa na polisi, vijana wakajitokeza kumlinda.
Mwisho, anawaomba watanzania wote wampatie kura, Chadema ni Tumaini jipya, makofi kibaoooo, anasema tuanze mabadiliko pamoja

Anasema hataki kuona watu wanalala kwenye nyasi, na tembe; kwa kuondoa kodi katika vifaa vya ujenzi.
Anasema Elimu ya bure inawezekana, atalisimamia swala hilo ili vijana wetu wapate matumaini mapya,

La mwisho kabisa, kuna maswala yanamgusa mtanzania wa kawaida ambayo hawajayazungumzia kwa kuwa hawajafanya utafiti, ila watashughulikia ili watanzania wawe na maisha bora ya kweli.

Kwamba, maendeleo yaitakiwi yawe ya vitu bali ya watu.

Mwisho, Asanteni sana na poleni kwa Spell error, ni kwa sababu speed ya kuongea na kuandika ni tofauti.

Tuko pamoja,

MC
 
Back
Top Bottom