Anaongelea nyumba za Tembe na Majani, mtu ananyumba imekaribia kuanguka lakini ameweka picha ya chagua kikwete, anashangaa sana.
Dr. ana data ya pesa ambazo CCm wamelipia mabango na hayajalipiwa ushuru, anasema kama haya yanawezekana kutapanya mabango nchi nzima, je elimu ya mtoto wako haiwezekani,
Kama unaweza kwenda kunywa chain a obama, kwa nini useme elimu bure haiwezekani?
Dr. anasema yuko tayari kula mihogo ikulu ila elimu iwe bure.
Anasema pesa ziko zimesambaa kote kwenye idara za serikali, kinachotakiwa ni uwajibikaji. Anasema kila mahali kuna uchafu, miezi ya kwanza ni kurekebisha na kurejesha uwajibikaji. Kwenye swala hili ametoa mifano kibao alipokuwa somewhere mawilayani.
Anataarifiwa kuwa zimebaki dakika saba, anatoa points za mwisho mwisho
Anawashukuru sana watanzania
Anawaomba radhi majimbo ambayo ameshindwa kufika leo kwa sababu ya wimbi zito
Anasema katika siku 71 ni vigumu kufika majimbo yote hata kwa kutumia helikopta, ila anawaomba wote kura zao.
Anasema yeye hataki kuona damu ya mtanazania inamwagika
Anasema Tanzania itakuwepo hata baada ya uchaguzi
Anasema kwa siku nane zilizobaki, ukipigwa kofi basi geuza la pili maana hautakufa
Anasema, ukitaka kumuumiza aliyekupiga, wewe mpuuze, inauma zidi ya kulipiza kisasi
Anamwomba kikwete awe makini, anasema vurugu zitaletwa na serikali, na polisi na watendaji wengine, ametoa mifano ya mwanza, ambapo hakulindwa na polisi, vijana wakajitokeza kumlinda.
Mwisho, anawaomba watanzania wote wampatie kura, Chadema ni Tumaini jipya, makofi kibaoooo, anasema tuanze mabadiliko pamoja
Anasema hataki kuona watu wanalala kwenye nyasi, na tembe; kwa kuondoa kodi katika vifaa vya ujenzi.
Anasema Elimu ya bure inawezekana, atalisimamia swala hilo ili vijana wetu wapate matumaini mapya,
La mwisho kabisa, kuna maswala yanamgusa mtanzania wa kawaida ambayo hawajayazungumzia kwa kuwa hawajafanya utafiti, ila watashughulikia ili watanzania wawe na maisha bora ya kweli.
Kwamba, maendeleo yaitakiwi yawe ya vitu bali ya watu.
Mwisho, Asanteni sana na poleni kwa Spell error, ni kwa sababu speed ya kuongea na kuandika ni tofauti.
Tuko pamoja,
MC