Fuatilia live Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM.
Fuatilia mubashara Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM ambapo wanaotazamiwa kushiriki ni;
1. Dk. Emmanuel Nchimbi - CCM
2. Martha Chiomba - NNCR Mageuzi
3. Ado Shaibu ACT Wazalendo
4. Ahmad Masoud - CUF
5 John Mnyika - CHADEMA
Odemba akitangaza kwa masikitiko makubwa huku akilia amewaambiwa waliofika kwenye mdahalo huo kuwa Nchimbi mpaka muda huu hajatokea kwenye mdahalo, ambapo Mnyika amefika kwenye mhalo huo lakini kutokana na kuwa Nchimbi hayupo hivyo naye hatoshiriki kwenye mdahalo huo.
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shahibu amefika kwenye mdahalo huo, lakini kwakuwa wa CHADEMA na CCM hawashiriki naye pia amegoma kushirki, NCCR Mageuzi walituma mwakilishi, ila kwakuwa wengine hawashirki nao pia wamesema hawatashiriki.
Odemba amelaani vikali kilichotokea, lakini mjadala unaendelea hata baada ya changamoto hii kutokea ambapo yaliyopangwa kujadiliwa yatakuwa mjadala wa wazi kwa washiriki waliofika.