LESIRIAMU
JF-Expert Member
- Feb 12, 2008
- 9,006
- 14,536
Fuatilia live Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM.
Fuatilia mubashara Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM ambapo wanaotazamiwa kushiriki ni;
1. Dk. Emmanuel Nchimbi - CCM
2. Martha Chiomba - NNCR Mageuzi
3. Ado Shaibu ACT Wazalendo
4. Ahmad Masoud - CUF
5 John Mnyika - CHADEMA
Odemba akitangaza kwa masikitiko makubwa huku akilia amewaambiwa waliofika kwenye mdahalo huo kuwa Nchimbi mpaka muda huu hajatokea kwenye mdahalo, ambapo Mnyika amefika kwenye mhalo huo lakini kutokana na kuwa Nchimbi hayupo hivyo naye hatoshiriki kwenye mdahalo huo.
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shahibu amefika kwenye mdahalo huo, lakini kwakuwa wa CHADEMA na CCM hawashiriki naye pia amegoma kushirki, NCCR Mageuzi walituma mwakilishi, ila kwakuwa wengine hawashirki nao pia wamesema hawatashiriki.
Odemba amelaani vikali kilichotokea, lakini mjadala unaendelea hata baada ya changamoto hii kutokea ambapo yaliyopangwa kujadiliwa yatakuwa mjadala wa wazi kwa washiriki waliofika.
Mambo ambayo watu watashiriki kwenye mjadala huu ni nini kifanyike kuhusu watu kukamatwa ama kupotea kipindi cha uchaguzi, tufanye nini ili tuwe na uchaguzi wenye tija na kupata viongozi bora pamoja na nini maoni ya watanzania kuhusu makatibu wa vyama vya siasa nchini kukimbia midahalo?
Wahudhuriaji wengi walaani kitendo cha Nchimbi kuingia mitini kwenye mdahalo huu na kusema wanatoa mfano mbovu kwa vijana ambao wanawaangalia na kujifunza kutoka kwao
Baadhi ya wadau wasema watu hupotezwa kwa hofu ya CCM kushindwa uchaguzi
Ccm ni wahuni. Hawajali hata gharama zilizo tumika kuandaa hiki kipindi. Na mkome nyie star tv kuwa shobokea wahuni. Ccm wanacho jua kuua na kufuja mali za Watanzania. Wana kiburi cha kulindwa na dola.