Pre GE2025 Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa: Nchimbi kaingia mitini, wengine wagoma kushiriki!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Fuatilia live Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM.​

Fuatilia mubashara Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM ambapo wanaotazamiwa kushiriki ni;

1. Dk. Emmanuel Nchimbi - CCM
2. Martha Chiomba - NNCR Mageuzi
3. Ado Shaibu ACT Wazalendo
4. Ahmad Masoud - CUF
5 John Mnyika - CHADEMA

Odemba akitangaza kwa masikitiko makubwa huku akilia amewaambiwa waliofika kwenye mdahalo huo kuwa Nchimbi mpaka muda huu hajatokea kwenye mdahalo, ambapo Mnyika amefika kwenye mhalo huo lakini kutokana na kuwa Nchimbi hayupo hivyo naye hatoshiriki kwenye mdahalo huo.

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shahibu amefika kwenye mdahalo huo, lakini kwakuwa wa CHADEMA na CCM hawashiriki naye pia amegoma kushirki, NCCR Mageuzi walituma mwakilishi, ila kwakuwa wengine hawashirki nao pia wamesema hawatashiriki.

Odemba amelaani vikali kilichotokea, lakini mjadala unaendelea hata baada ya changamoto hii kutokea ambapo yaliyopangwa kujadiliwa yatakuwa mjadala wa wazi kwa washiriki waliofika.

Mambo ambayo watu watashiriki kwenye mjadala huu ni nini kifanyike kuhusu watu kukamatwa ama kupotea kipindi cha uchaguzi, tufanye nini ili tuwe na uchaguzi wenye tija na kupata viongozi bora pamoja na nini maoni ya watanzania kuhusu makatibu wa vyama vya siasa nchini kukimbia midahalo?

Wahudhuriaji wengi walaani kitendo cha Nchimbi kuingia mitini kwenye mdahalo huu na kusema wanatoa mfano mbovu kwa vijana ambao wanawaangalia na kujifunza kutoka kwao

Baadhi ya wadau wasema watu hupotezwa kwa hofu ya CCM kushindwa uchaguzi

Ccm ni wahuni. Hawajali hata gharama zilizo tumika kuandaa hiki kipindi. Na mkome nyie star tv kuwa shobokea wahuni. Ccm wanacho jua kuua na kufuja mali za Watanzania. Wana kiburi cha kulindwa na dola.
 
Sijaona mantiki ya mdahalo kutofanyika simply katibu mkuu wa CCM kutokuwepo. Hao wengine waliofika si wageendelea na mdahalo?
Ila matamasha ya kukata viuno mngeenda

Ova
 
Ccm midahalo wapi na wapi
Kutwa kuingia mitini

Ova
 
Kanikumbusha watu walivokuaga wananikacha kwenye debate...hasa ile mada ya
Money is the source of all evil
au
A politician and a snake which is danjerazi ?
 
Sijaona mantiki ya mdahalo kutofanyika simply katibu mkuu wa CCM kutokuwepo. Hao wengine waliofika si wageendelea na mdahalo?
Watawaliwa wenyewe kw wnywe bila mtawala! Isingekua na tija. Uahirishwe mpk cku atakapoamua tayari, hana vikao huyo muoga
Sijaona mantiki ya mdahalo kutofanyika simply katibu mkuu wa CCM kutokuwepo. Hao wengine waliofika si wageendelea na mdahalo?
 
Fuatilia live Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM.​

Fuatilia mubashara Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM ambapo wanaotazamiwa kushiriki ni;

1. Dk. Emmanuel Nchimbi - CCM
2. Martha Chiomba - NNCR Mageuzi
3. Ado Shaibu ACT Wazalendo
4. Ahmad Masoud - CUF
5 John Mnyika - CHADEMA

Odemba akitangaza kwa masikitiko makubwa huku akilia amewaambiwa waliofika kwenye mdahalo huo kuwa Nchimbi mpaka muda huu hajatokea kwenye mdahalo, ambapo Mnyika amefika kwenye mhalo huo lakini kutokana na kuwa Nchimbi hayupo hivyo naye hatoshiriki kwenye mdahalo huo.

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shahibu amefika kwenye mdahalo huo, lakini kwakuwa wa CHADEMA na CCM hawashiriki naye pia amegoma kushirki, NCCR Mageuzi walituma mwakilishi, ila kwakuwa wengine hawashirki nao pia wamesema hawatashiriki.

Odemba amelaani vikali kilichotokea, lakini mjadala unaendelea hata baada ya changamoto hii kutokea ambapo yaliyopangwa kujadiliwa yatakuwa mjadala wa wazi kwa washiriki waliofika.

Mambo ambayo watu watashiriki kwenye mjadala huu ni nini kifanyike kuhusu watu kukamatwa ama kupotea kipindi cha uchaguzi, tufanye nini ili tuwe na uchaguzi wenye tija na kupata viongozi bora pamoja na nini maoni ya watanzania kuhusu makatibu wa vyama vya siasa nchini kukimbia midahalo?

Baadhi ya hoja zilizotolewa na wahudhuriaji

  • Wahudhuriaji wengi walaani kitendo cha Nchimbi kuingia mitini kwenye mdahalo huu na kusema wanatoa mfano mbovu kwa vijana ambao wanawaangalia na kujifunza kutoka kwao
  • Baadhi ya wadau wasema watu hupotezwa kwa hofu ya CCM kushindwa uchaguzi
  • Watanzania tuungane kupinga vitendo vya utekaji
  • CCM wanaenda kinyume na 4R za Rais Samia
  • CCM ni wazuri kungumza lakini vitendo ni 0
  • Vijana wa CCM wamechukua njaa tumboni wameihamisha kichwani, ofisi ya katibu mkuu ina watu watendaji wingi, Nchimbi angeweza kuacha watendaji wengine na akafika kwenye mdahalo
  • Uchaguzi wa mwaka huu (2024) CCM wamejipanga kufanya mabaya na ndio maana wamekimbia mdahalo sababu walijua wataulizwa kuhusu hayo
  • Jeshi la polisi ni kwaajili ya wananchi wote na siyo chama, hivyo wasijihusishe na masuala ya kisiasa na waache vyama vipambane
  • Vyombo vya Habari watoe habari za ukweli bila hofu, sababu kwa kuweka hofu wanakuwa wanalea mambo ya hovyo na wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa vyama vya upinzani

Mimi nafikiri ni wakati wa vyuo vilivyo wapa viongozi wa CCM PHD viwavuwa. Mtu unakuwaje na PHD halafu unakuwa sehemu ya wapumbavu kama ccm ? Yaani mimi nikiona mtu anava nguo za kijani popote pale mimi najuwa moja kwa moja kuwa ni tahila. Haiwezekani kwa maovu yote hayo ccm imewafanyia watanzania walio iamini kwa miaka zaidi ya 60 halafu bado awepo mtu mwenye akili timamu awe sehemu ya ccm. Imagine. Nchi yenye kila kitu ila watu wake hawana ajira za maana, hospital zake ni vituo vya kuhifadhi maiti, vyuo vinazalisha chawa na madreva wa bodaboda, bandari na bunga za wanyama wmegawa kwa warabu, madini wameuzia wazungu, miundo mbinu imekuwa miradii kichina. Biashara kubwa zimekuwa vichaka vya kuficha kodi zilizo ibwa serikalini. Wananchi wa kawaida wamegeuzwa watumwa ndani ya nchi yao. Mwalimu analipwa laki tano kwa mwezi. Mkuu wa mkowa kama bashite analipwa milioni Sita kwa siku. Dakitari alipwa mlioni moja kwa mwezi halafu mbunge wa darasa la saba analipwa milioni 20 kwa mwezi. ,makanisa ,bar na guest house ni vingi kuliko kuliko shule na vituo vya afya. .
 
Katibu Mkuu wetu Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi Yupo kwenye vikao vizito sana katika maandalizi ya kikao maalumu cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kitakachoketi Tarehe 2 septemba chini ya uwenyekiti wa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Hivyo hawezi kuacha vikao hivi halafu aende huko kwingine.Kumbuka macho na masikio yoote ya watanzania yameelekezwa kwenye vikao vya CCM na kusubiri kwa hamu na shauku kubwa na nzito Maazimio yake.View attachment 3083807
Hamna kitu
Ingekuwa tukio la zuchu
Wangeenda

Ova
 
Aliyeharibu mdahalo ni huyo mnyika aliyeanza kumshambulia Dr Nchimbi mitandaoni kabla ya wakati.

Kwa namna fulani ni kweli kabisa, alitakiwa aelewe wengine wanaweza kuwa na majukumu hata nnje ya mipaka yetu.
Sababu kuna majukumu ni mazito na ya kutekelezwa kuliko kuanzisha hoja zisizo na mashiko, watu wanaweza jisahaulisha au kutokutambu ya kwamba baadhi ya vyama vina mizizi na uzito kuliko tunavyo dhania na kazi zake zinatakiwa kuwa nzito na nyingi zaidi.
 
Unaweza kushangaa ata historia ya midahalo na chimbuko lake ulijui wewe umekariri Wazungu tu.
Hivi kwenye mitaala ya elimu yetu topic ya midahalo imeshaondolewa?
🗣️🗣️🗣️
 
Kwani akikosekana Mnyika wengine hawawezi kuendelea?
Brother Mshana Jr Niko nje ya mada ninashida naww ila siwez kukupata PM nakuomba kama hutojari nifungulie Kwa Muda nkushirikishe then utaendelea na taratibu zako kama kawaida. Natanguliza shukran🙏
 
Fuatilia live Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM.​

Fuatilia mubashara Mdahalo wa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa Maktaba ya UDSM ambapo wanaotazamiwa kushiriki ni;

1. Dk. Emmanuel Nchimbi - CCM
2. Martha Chiomba - NNCR Mageuzi
3. Ado Shaibu ACT Wazalendo
4. Ahmad Masoud - CUF
5 John Mnyika - CHADEMA

Odemba akitangaza kwa masikitiko makubwa huku akilia amewaambiwa waliofika kwenye mdahalo huo kuwa Nchimbi mpaka muda huu hajatokea kwenye mdahalo, ambapo Mnyika amefika kwenye mhalo huo lakini kutokana na kuwa Nchimbi hayupo hivyo naye hatoshiriki kwenye mdahalo huo.

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shahibu amefika kwenye mdahalo huo, lakini kwakuwa wa CHADEMA na CCM hawashiriki naye pia amegoma kushirki, NCCR Mageuzi walituma mwakilishi, ila kwakuwa wengine hawashirki nao pia wamesema hawatashiriki.

Odemba amelaani vikali kilichotokea, lakini mjadala unaendelea hata baada ya changamoto hii kutokea ambapo yaliyopangwa kujadiliwa yatakuwa mjadala wa wazi kwa washiriki waliofika.

Mambo ambayo watu watashiriki kwenye mjadala huu ni nini kifanyike kuhusu watu kukamatwa ama kupotea kipindi cha uchaguzi, tufanye nini ili tuwe na uchaguzi wenye tija na kupata viongozi bora pamoja na nini maoni ya watanzania kuhusu makatibu wa vyama vya siasa nchini kukimbia midahalo?

Baadhi ya hoja zilizotolewa na wahudhuriaji

  • Wahudhuriaji wengi walaani kitendo cha Nchimbi kuingia mitini kwenye mdahalo huu na kusema wanatoa mfano mbovu kwa vijana ambao wanawaangalia na kujifunza kutoka kwao
  • Baadhi ya wadau wasema watu hupotezwa kwa hofu ya CCM kushindwa uchaguzi
  • Watanzania tuungane kupinga vitendo vya utekaji
  • CCM wanaenda kinyume na 4R za Rais Samia
  • CCM ni wazuri kungumza lakini vitendo ni 0
  • Vijana wa CCM wamechukua njaa tumboni wameihamisha kichwani, ofisi ya katibu mkuu ina watu watendaji wingi, Nchimbi angeweza kuacha watendaji wengine na akafika kwenye mdahalo
  • Uchaguzi wa mwaka huu (2024) CCM wamejipanga kufanya mabaya na ndio maana wamekimbia mdahalo sababu walijua wataulizwa kuhusu hayo
  • Jeshi la polisi ni kwaajili ya wananchi wote na siyo chama, hivyo wasijihusishe na masuala ya kisiasa na waache vyama vipambane
  • Vyombo vya Habari watoe habari za ukweli bila hofu, sababu kwa kuweka hofu wanakuwa wanalea mambo ya hovyo na wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa vyama vya upinzani

Vyombo vya habari haviwezi kutoa habari muhimu na za kweli kwa kuhofia kuikosa rushwa ya ukuu wa wilaya na uongozi, kutokana na kukosa ya kutangaza vyombo vyote vimejikita kwenye uchambuzi wa Simba na Yanga kutwa nzima mwezi mzima mwaka mzima!
 
Sijaona mantiki ya mdahalo kutofanyika simply katibu mkuu wa CCM kutokuwepo. Hao wengine waliofika si wageendelea na mdahalo?
Mdahalo huandaliwa kwa kushindanisha pande mbili kubwa + na -, endapo upande mmoja utakosekana inamaana hakutakuwa na chaji hivyo hauna sababu ya kuwasha swichi, tujikumbushe Kikwete na CCM walipochomoa fyuzi baada ya kuboronga kwenye mdahalo na chama kikapiga marufuku ushiriki kwenye midahalo, nadhani marufuku ile bado haijaondolewa.
 
Katibu Mkuu wetu Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi Yupo kwenye vikao vizito sana katika maandalizi ya kikao maalumu cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kitakachoketi Tarehe 2 septemba chini ya uwenyekiti wa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Hivyo hawezi kuacha vikao hivi halafu aende huko kwingine.Kumbuka macho na masikio yoote ya watanzania yameelekezwa kwenye vikao vya CCM na kusubiri kwa hamu na shauku kubwa na nzito Maazimio yake.View attachment 3083807
majizi hayajawahi kosa sababu,tutawasubiri tu waache kukimbia
 
Back
Top Bottom