Mdhamini: Tundu Lissu ameshapona, anashindwa kurejea nchini akihofia usalama wake

Mdhamini: Tundu Lissu ameshapona, anashindwa kurejea nchini akihofia usalama wake

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imeelezwa kuwa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ameshapona ila anashindwa kurudi nchini kwa kile alichokidai ni kuhofia usalama wake.

Hayo yameelezwa leo Novemba 21,2019 na Mdhamini wa Lissu, Ibrahim Ahmed, alipokuwa akiieleza mahakama hiyo juu ya afya ya Mwanasheria huyo wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Ahmed ameieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati wa kesi ya uchochezi inayomkabili mshtakiwa huyo na wenzake watatu ilipoitwa.

41028383_303.jpg

Pia soma



 
Lissu jikalie tu ulaya achana na siasa uchara za kununuana za wapumbavu wanaofikiria watanzania wote ni mafala kama wao kuna siku utarudi waache wapumbavu wafanye wanayoyafanya maana ukija watasema unawakwamisha tulia kula bata achana na upumbavu.
 
Kama alikua anaamini anachokiongea anaogopea nini kurudi? arudi tu apambane Mahakama si zipo

ifike wakati hawa wana siasa wakumbukege kuna "kesho"
Mahakama zipi mkuu? Baba levo alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kule kigoma leo mahakama hiyo hiyo imetengua hukumu na kusema haikuwa ya haki, unadhani Lisu jinsi alivyotaka kuuwawa hizi mahakama zikimuhukumu kwa hila kuna hakimu atatengua hukumu hiyo?
 
Lissu jikalie tu ulaya achana na siasa uchara za kununuana za wapumbavu wanaofikiria watanzania wote ni mafala kama wao kuna siku utarudi waache wapumbavu wafanye wanayoyafanya maana ukija watasema unawakwamisha tulia kula bata achana na upumbavu.
Hili ndilo la msingi haswa
 
Kama alikua anaamini anachokiongea anaogopea nini kurudi? arudi tu apambane Mahakama si zipo

ifike wakati hawa wana siasa wakumbukege kuna "kesho"
Mahakama za nchi ipi?

Hizi hizi zinazofuata maelekezo kutoka "juu"?


Baada ya Kushindwa Kumuua Kwa Risasi nafsi zenu zinaweweseka Sana, sasa mnatamani arudi ili mbadilishe Mbinu?
 
Anaogopa nini. mbona nyie makamanda mnamuogopa jiwee..

Ila mi sinashida hata angekufa nisingeumia kwani hajawahi kutetea watu wanaonewa mfano Shekhe ponda alipopigwa risasi mbona alikuwa kimyaa? Af leo et nisikitike walaa akitaka ahamie hukoo. Wanasiasa wote wapigwe risasi tuu wafe nasisi watuue tufe
 
Back
Top Bottom