Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Mtaongea lugha zote na kumtetea huyo kihiyo lkn ili Gwajima aoekane muongo wekeni vyeti,lkn hata mseme nini Daudi anahitajika ashitakiwe mahakani kwa kutumia cheti cha MTU mwingine ni kosa kisheria.

Nendeni mkashitaki
 
Mwelekeze am shauri huyo dogo kuwa na adabu na awe tayari kutubu pale anapoambiwa anakosea eg ubungo plaza scam
 
Mbowe hatumii vyeti vya mwingine Hata kama ana div 0. Ameridhika na zero yake ndo maana hakuthubutu kutumia cha mwingine
 
SIJAWAI KUPATA KUMUELEWA MCHUNGAJI GWAJIMA HATA SIKU MOJA, NA SITOKAA NA KUMPONGEZA MAKONDA KIUONGOZI HABADANI.
 
Huyu dogo vipi?Gwajima ni mchungaji lakini pia ni mtanzania aliyetuhumiwa kuuza madawa ya kulevya.Kwa hiyo anahaki ya kujibu tuhuma pia kuhoji uhalali wa vyeti vya Makonda.Mlikuwa wapi kuongelea hili wakati Gwajima anatuhumiwa?
 
Kazi ndogo tu hapa weka vyeti tuachane na Gwajima hapa jina la mchezo ni Bashite sio mdogo wake Gwajima huyo naye atakuwa anafanya biashara ya mihogo atulie kwanza vyeti viwekwe mezani.
 
Si Gwajima anadanganya watu kuwa Kabisa lake linafufua wafu? Hiyo ndio tuhuma ya udanganyifu kwa umma!
 
hahaha watu wengine 'HAKILI' HAMNA
 
Kwani mkuu wa mkoa kuambiwa aonyeshe vyeti vya form four ni kumzuia kupambana na madawa ya kulevya?
 
Maneno matupu bila vyeti ni Unaa.. Nilijua Kaleta vyeti. JINGALAO mkubwa.
 
Huyo katumwa, ina maana mchungaji alivyochafuliwa hadharani hakuona, hata alivyolala selo hukuona?,
Mbali ya hayo yote, kwani mkuu wa mkoa akionyesha vyeti vyake atapungukiwa vipi nguvu ya kupambana na madawa ya kulevya? Kama ana kosa la kutumia cheti cha mtu mwingine, hana budi kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria. Kupambana na madawa ya kulevya isiwe kichaka cha wavunja sheria
 
Ndugu wa Ngwajima anasema Ngwaji hajawai hata kufufua panya ndio aweze binadamu hahaha sasa misukule ina amini atafufua binadamu...
 
Huyu ni mhuni Fulani kajitengenezea kimkutano cha ubabaishaji.Kwanza hajajitambulisha yeye ni nani! Na sisi tusiokuwa wa familia ya Gwajima tutajidhihirisha vipi kuwa kweli ni mdogo wake? Any way jumapili nitafika kanisani kwa Gwajima najua majibu ya hiki kilichopo hapa kitazungumzwa na Gwajima na Familia yake pale Ubungo.
 
Dah! huyu ndiye ndugu yake anayemfahamu in and out " hajawaki kufufua hata panya" ila waliokutana naye bongo ndio wanajifanya kumuamini. Kamrarua ile mbaya
"MDOGO WAKE"
Hana jina?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…