Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Ss najaribu kutafakari km Mchungaji Gwajima ni last born hyo kada Wa chama katokea wapi
 
Tunajua Gwajima tapeli wala hakuna anaemamini, tunarudi kwa Daudi vyeti tunataka mbona rahisi tu
 
sijui wengi wetu tuna akili za kushikiwa!, ndugu wa makonda kajitokeza mmewaamini waloyasema ila ndugu wa gwajima kujitokeza hamumuamini kazi kumponda!, haya ndo kashasema hajawahi fufua hata panya rubbish!..
 
Ngoja tusubiri j2 gwajima mkubwa atakapomjibu gwajima mdogo
 
Huyu naye atakuwa ameshahongwa mwambieni Daudi Bashite aonyeshe vyeti vyake hadharani kama hajanunua aache usanii kwenye jumba la sanaa.
 
Huyo sio mdogo wake kwakweli...yani ndugu yako wa dam kabisa anatuhumiwa kuuza unga anadakwa na kulala central ...badala ya kumsaidia unasema ujinga kama huo..ety serikali inamlea sana Gwajima....ety anatuhumiwa vingi sana...hajamfufua baba wa watoto yatima ....huyu ni mjinga....kwaiyo anaisapport serikali imkandamize kaka yake...imfunge...imtuhumu kwa kuuza unga...huyu dogo anabidi akapimwe akili...Na sidhani kama ni mdogo wake wa kweli
Amsaidiaje kuyauza? kuyaficha? kuficha ukweli? anatuhumiwa kweli ndugu anajua jamaa hawez fufua kitu wewe unamuita mjinga kama nan? aachwe mtaani azidi kutuharibu kama anauza anyongwe!.
 
Sisi watz tumechoka na ujinga wenu hoja ya msingi hapa ni.madawa ya kulevya ni siyo ujinga wenu .
Lete vyeti sio kelele hapa
089b2f7a6cdc755d6465d0e12c85f5cf.jpg
 
Huwa nasema kila siku upinzani hawajitambui!

Yani mwanafamilia kaja kuthibisha kwamba Gwajima ni tapeli, wewe msukule unaemuona kupitia tv unakuja hapa na porojo zako!
 
Nilimsikiliza kwa makini sana nikajua sasa busara inatawala, lakini alichokosea huyo ndugu ni kusema tu.. Yeye ni kada wa ccm. Kauli zake zote zitachukuliwa kisiasa pia..

Nasubiri majibu ya akomeeee kutoka kwa Gwajima maana ukiingiza siasa tu Gwajima hakuachi.
 
Alichozungumza ni sahihi kabisa na mimi namsifu kwa ujasiri alionao, ishu ya vyeti ni suala la yeye na mwajiri wake na kwakuwa nafasi aliyopewa sio ya kupigiwa kura sidhani kama kunahajaya watu kushikia bango kiasi hicho ati aonyeshe vyeti ili kiwe nini? na kwavyovyote vile ingekuwa ya ni nafasi ya kushindaniwa yawezekana asingetia mguu. Hatahivyo shida kubwa watu wameamua kujitoa ufaham kwenye jambo la msingi la madawa ya kulevya kwa sarakasi za gwajima. Yaani watu na elimu zao kila siku wamekalia vyetivyeti mdaini vyeti akigombea ubunge au udiwani hii aliyoteuliwa na Rais atajuana na bosi wake. Tuwe serious jamana watanzania please for the seck of our country

Dawa za Kulevya kakabidhiwa Siang'a ambaye anafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na husikii watu wakilalamika kuonewa.Baraza la Mitihani linahamasisha watanzania kuwafichua wote wenye vyeti feki na wanaotumia vyeti ambavyo sio vya kwao.Adhabu yake ni kifungo cha Miaka Saba Gerezani.Watanzania wamemfichua Bashite kutekeleza Maombi ya Baraza la Mitihani na kuisaidia Serikali katika zoezi uhakiki wa vyeti feki.
Kumbuka Nchi ni ya Watanzania na watanzania ndio hawataki kiongozi mwenye vyeti feki.
 
Kwa ufupi

Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake. Amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.

Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.

Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.

Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.

Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.


wee dogo Gwajima... embu usituondoe kwenye uwepo wa kusubiri vyeti hapa!
 
Back
Top Bottom