Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Mdogo wa Gwajima amtetea Makonda, asema Josephat apuuzwe vita ya madawa ya kulevya

Huyu nae anatafuta kiki aonekane kwenye media. Anaongea ujinga kwa nini sasa asitumie fursa hiyo kumwambia Makonda aonyeshe vyeti. Badala ya kusema eti yeye anatetea uzalendo wa Daudi Bashite.
 
Sawa! Hakuna anayepinga vita dhidi ya madawa ya kulevya; tena tunaiunga mkono sana Tume ya Kamishna Siang'a kwa jukumu zito na muhimu. Hata hivyo, vita dhidi ya madawa haihalalishi forgery za aina yoyote. Vyeti viwekwe mezani acheni blah blah.
Viwekwe meza ipi?
 
Kwa ufupi

Mdogo wake na mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la ufufuo na uzima, amesema mchungaji huyo anatakiwa aache kutumika na kuhoji kuna nani nyuma yake. Amedai mchungaji hawezi kujiingiza kwenye malumbano na mipasho ya kidunia.

Ameendelea kusema vyeti vya Makonda viachiwe mamlaka husika kuchunguza kwani kumuandama sana inaweza kusababisha watu wengine siku zijazo kuogopa kujihusisha kupambana na madawa ya kulevya.

Amesema serikali imemlea sana Gwajima na waziri wa mambo ya ndani anatakiwa amuangalie na ana tuhuma nyingi ikiwemo kadai angemfufua baba wa watoto yatima ilhali yeye anajua hajawahi kufufua hata panya.

Amedai tabia ya kubeza shughuli za maendeleo zinazofanywa na serikali sio tabia njema na haiisadii nchi. Amesema anajua vita ya madawa ya kulevya ni ngumu na hugharimu maisha, atoa wito kwa watanzania wote kuunga mkoni juhudi za kutokomeza madawa ya kulevya hasa Dar es Salaam.

Amesema anafahamu yeyote atakayejitokeza kuunga mkono juhudi za kupambana na madawa ya kulevya ataandamwa tu na hivyo kwa namna ya pekee anamshukuru mkuu wa mkoa wa Dar Paulo Makonda na atakumbukwa na vizazi vyote kwa kujitoa Muhanga kusimamia vita ya madawa ya kulevya Dar es Salaam na kila mmoja amefahamu athari za madawa ya kulevya hadi kwa watoto wadogo ndio maana anaandamwa kila kona na kuhoji walikuwa wapi kuyasema yote kabla ya vita ya madawa ya kulevya.

Huyu atakua mwanasheria wa serikali ambaye amekula mlungula.
Mjinga kabisa.

Kati ya Bashite na kamishna alieteuliwa na na Rais Rogers Siang'a nani amesomea kuthibiti Madawa ya kulevya.?
 
Mtaongea lugha zote na kumtetea huyo kihiyo lkn ili Gwajima aoekane muongo wekeni vyeti,lkn hata mseme nini Daudi anahitajika ashitakiwe mahakani kwa kutumia cheti cha MTU mwingine ni kosa kisheria.
Ni sahihi lkn atapelekwa mahakamani bila ushahidi?
 
Kama umeandika zaidi ya Maneno 5000 bila kumtaja huyo Mdogo wake Gwajima kwa Majina yake wewe ndio utakuwa ni kilaza zaidi ya Bashite.

TUNATAKA VYETIIIIIIIIIII
Mvipeleke wapi? Vyanini?
 
katika vitabu vyote vya kikristo ambavyo vimeandika kuwa unapotoa majini kwa mgonjwa sharti uyatume kwa binadamu mwenzako hakuna hicho kitu
Hakuna hata sehemu moja ya maandiko yanayosema hivyo nadhani huyu anajua anatumia nguvu za namna gani nadhani amezitoa kule Nigeria

Hata Yesu Kristo alipokuwa anayatoa majini aliyaamuru kwenda kuwaingilia nguruwe na sio binadamu wengine
Tumeona alichofanya Gwajima nikiwa kama mkatoriki safi nampinga hadharani kwa alichofanya

Hakuna ukristo unaofundisha huo upumbavu nina imani pia hata katika uislamu hakuna mafundisho ya namna hii
Hakuna nabii wa namna hii na hawa ndio wale manabii ambao Yesu Kristo alisema watakuja
Na nabii wa mwisho kuja hapa duniani ni Yesu Kristo hawa wengine wote ni waganga njaa tu wameamua kugeuza dini kuwa biashara

Niliwahi kuhoji uko nyuma kuwa hivi Mungu wa Gwajima ni yupi? Ni huyu huyu Mungu wa Isaka na Yakobo? Ndio huyu huyu tunaemuomba sisi kila siku?
Nadhani sasa watu wamejua rangi halisi ya huyu anayejiita askofu
Hakuna askofu wa namna hii ambaye anaamuru majini yaende kwa mtu mwingine kisa tu wana ugomvi wao binafsi
Huyu si askofu huyu ni Mganga wa Kienyeji na kumuita Gwajima askofu ni kuwatukana maaskofu wote

Ni wakati sasa wa serikali kuyachunguza haya makanisa
Wengine wana vibali vya kutoa huduma lakini ni waganga wa kienyeji, Huyu Gwajima ni mganga wa kienyeji au ni mchawi
Nikiwa kama mkristo safi nalaani kitendo alichofanya huyu askofu feki

Ndimi

RAPHAEL LUKINDO
0765499321
 
Mimi najiuliza sana kuhusu kutajwa kwa mchungaji gwajima katika sakata la madawa ya kulevya, sijui sana lkn naamini gwajima hahusiki na madawa ya kulevya walijaribu kumtaja tu ni kwasababu ya mali anazo miliki, lkn kulikuwa na sababu gani ya gwajima kuanza kumchamba paul makonda kiasi kile wakati yeye hahusiki, kama yeye ni mchungaji anawafundisha nn waumini wake wanapopitia changamoto kama hizo, yesu kristo ambaye wao wanamwakilisha alikuwa na upendo na unyenyekevu sana ambapo wachungaji, mapadri nanatufundisha tuwe na upendo kama ule, tena biblia inatwambia akupigaye shavu la kushoto mpe na lakulia sasa kwanini yeye ana jazba vile, juzi nimeona scine moja inatembea anamtoa mtu majini afu anayaambia toka kwa jina la yesu nenda kwa mtu anaesumbua hapa daresalam akimaanisha liende kwa makonda, lile jini likamjibu kule hapaingiliki, akawa analilazimisha eti lisipoenda atalichoma moto. Jaman nakumbuka yesu alitoa mapepo aliyaamuru yaende kwa nguruwe kwani hakukua na watu walio muudhi? Napata wasiwasi kuhusu utumishi wa huyu mtu kama kweli anamwabudu mungu wa kweli , nakumbuka hayo mambo ya jino kwa jino yako kwa waislam so angekuwa muislam wala nisinge uliza, kweli gwajima kachanganyikiwa, mwaka juzi alimtukana sana pengo lkn kwasababu lilekanisa limejaa misukule sheria ilipotaka kuchukua mkondo wake ilemisukule ilikuwa inalia eti inasema muacheni baba yetu kwani amewakosea nini ,nilishangaa sana nikasema ivi kanisa lile lote hakuna mtu mwenye smart phone ambaye ameona jinsi ambayo gwamaji kamtukana askofuu mkuu kadinali pengo jaman , ile kesi sikumbuki iliishaje lkn gwajima anatakiwa kupimwa akili, mimi naamin ni mtumishi wa mungu ila ufahamu wake unashida. Matokeo yake watu wamebaki kushadadia vyeti vya paul makonda na kusahau kabisa issue ya madawa ya kulevya, kiasi kizazi kinaangamia nguvukazi ya taifa inaangamia watu wanaona sawa tu kwakweli nimeumia kweli . Yangu ni hayo
 
Hamtutoi kwenye mstari na hao mnaowanunua. Leo mnaona issue ya vyeti ni upuuzi, madhara ya vyeti feki unayajua vizuri na ni makubwa kuliko unavyojaribu kudanganya watu kisa unamtetea mtoto wa mfalme. Hatuipuuzi vita ya madawa ya kulevya, lakini nayo haiwezi kutuondoa kwenye vita ya elimu feki.
Kufoji chochote ni kosa la jinai na hukumu yake ni miaka 7 mpk 15. Kwanini asijitokeze mtu akafungua kesi dhidi yake akiwa na ushahidi unaosemekana upo kwa gwajima? Wengi wanatarajia atoe vyeti hadharani je kama kweli amefoji atakubali kutoa vyeti aumbuke? Na je asipotoa kabisa itakuwaje?
 
Mimi najiuliza sana kuhusu kutajwa kwa mchungaji gwajima katika sakata la madawa ya kulevya, sijui sana lkn naamini gwajima hahusiki na madawa ya kulevya walijaribu kumtaja tu ni kwasababu ya mali anazo miliki, lkn kulikuwa na sababu gani ya gwajima kuanza kumchamba paul makonda kiasi kile wakati yeye hahusiki, kama yeye ni mchungaji anawafundisha nn waumini wake wanapopitia changamoto kama hizo, yesu kristo ambaye wao wanamwakilisha alikuwa na upendo na unyenyekevu sana ambapo wachungaji, mapadri nanatufundisha tuwe na upendo kama ule, tena biblia inatwambia akupigaye shavu la kushoto mpe na lakulia sasa kwanini yeye ana jazba vile, juzi nimeona scine moja inatembea anamtoa mtu majini afu anayaambia toka kwa jina la yesu nenda kwa mtu anaesumbua hapa daresalam akimaanisha liende kwa makonda, lile jini likamjibu kule hapaingiliki, akawa analilazimisha eti lisipoenda atalichoma moto. Jaman nakumbuka yesu alitoa mapepo aliyaamuru yaende kwa nguruwe kwani hakukua na watu walio muudhi? Napata wasiwasi kuhusu utumishi wa huyu mtu kama kweli anamwabudu mungu wa kweli , nakumbuka hayo mambo ya jino kwa jino yako kwa waislam so angekuwa muislam wala nisinge uliza, kweli gwajima kachanganyikiwa, mwaka juzi alimtukana sana pengo lkn kwasababu lilekanisa limejaa misukule sheria ilipotaka kuchukua mkondo wake ilemisukule ilikuwa inalia eti inasema muacheni baba yetu kwani amewakosea nini ,nilishangaa sana nikasema ivi kanisa lile lote hakuna mtu mwenye smart phone ambaye ameona jinsi ambayo gwamaji kamtukana askofuu mkuu kadinali pengo jaman , ile kesi sikumbuki iliishaje lkn gwajima anatakiwa kupimwa akili, mimi naamin ni mtumishi wa mungu ila ufahamu wake unashida. Matokeo yake watu wamebaki kushadadia vyeti vya paul makonda na kusahau kabisa issue ya madawa ya kulevya, kiasi kizazi kinaangamia nguvukazi ya taifa inaangamia watu wanaona sawa tu kwakweli nimeumia kweli . Yangu ni hayo
Hata uvumilivu nao una kiasi , nakisi hicho kikitosha busara huondoka, gwajima ana waumini na kutokqna na heshima ya kazi anayo fanywa hakupaswa kutangazwa kama kibaka wa kuku, nadhani usiwe na upendeleo kwa kudhani mooja hapaswi na mwingine anapaswa , hata maandika yana andika kiasi kilekile ulimpimia nduguyo ndicho hichi hicho nawe utapimiwa.hivyo waache wapimiane.
 
Back
Top Bottom