Mdogo wangu wa kike amenitusi muda huu, ninatetemeka kwa hasira

Huyu mdogo wangu yupo kidato cha nne, ninampenda sana na nimekuwa kama mshauri wake hususani kwenye issues za kujikinga na mahusiano kwa ujumla. Humfundisha mbinu za kuepuka vishawishi vya wanaume, kumpa madhara ya mimba na kumsisitiza asome kwa bidii. Kifupi tunapendana.

Sasa leo nimekuja hapa home nimekuta wanamsema huyu mdogo wangu, kuhusu tabia za kihuni. Mimi kama kaka mwenye uchungu na kuharibikiwa kwake nikalazimika kuvunga ili baadaye nimuulize. Sasa hatimaye nikapata nafasi nikamuuliza shida nini, akasema wanamsingizia ameanza uhuni. Nikamshauri sana na kumuambia asome kwa bidii, ukizingatia nimemzidi miaka 6.

Akanijibu na kuniambia niache mambo ya kike, niwe kama mwanaume na nisimfuatilie fuatilie. Sikuamini kwa kauli hii, nusu nizimie kwa kweli. Mpaka muda huu bado siamini, kosa langu lipi?

Je, au ndio haitakiwi kumpenda na kuzoeana na mdogo wako wa kike? Kumsisitiza kusoma ni kosa? Nimeukumbuka uzi humu wa jamaa akisema hakuna kucheka cheka na mwanamke awe ndugu yako au mtu baki, nimeamini sasa. Mbaya zaidi haya matusi amesikia mpaka house girl, ambaye tulikuwa tunaheshimiana sana. Hivi nitamuangaliaje usoni? Kifupi sipo sawa, bora angekuwa mtoto ndiye amenitukana, ila huyu binti wa form four mwenye akili timamu mwenye miaka 20 hapana.

Bado sijaamini! Sijui cha kuomba ni nini, ushauri au... Nashindwa ku type sipo sawa.
Hama nyumbani kaka
 
Ilishawahi nitokea, mdogo wangu wa kike alikua na tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani, kurudi usiku ikawa ni kawaida kwake. Pamoja na kuonywa Sana,tabia iliendelea mpaka siku Moja niliyoamua kumtandika viboko na baada ya hapo kutokujihusisha na jambo lake lolote ikiwa ni pamoja na kutokupokea salamu zake. Alinichukia Sana na ulipita muda mrefu mpaka pale alipokuja kugundua ujinga aliokuwa ameufanya. Leo hii tunaheshimiana na ananishukuru Sana
 
Huyu mdogo wangu yupo kidato cha nne, ninampenda sana na nimekuwa kama mshauri wake hususani kwenye issues za kujikinga na mahusiano kwa ujumla. Humfundisha mbinu za kuepuka vishawishi vya wanaume, kumpa madhara ya mimba na kumsisitiza asome kwa bidii. Kifupi tunapendana.

Sasa leo nimekuja hapa home nimekuta wanamsema huyu mdogo wangu, kuhusu tabia za kihuni. Mimi kama kaka mwenye uchungu na kuharibikiwa kwake nikalazimika kuvunga ili baadaye nimuulize. Sasa hatimaye nikapata nafasi nikamuuliza shida nini, akasema wanamsingizia ameanza uhuni. Nikamshauri sana na kumuambia asome kwa bidii, ukizingatia nimemzidi miaka 6.

Akanijibu na kuniambia niache mambo ya kike, niwe kama mwanaume na nisimfuatilie fuatilie. Sikuamini kwa kauli hii, nusu nizimie kwa kweli. Mpaka muda huu bado siamini, kosa langu lipi?

Je, au ndio haitakiwi kumpenda na kuzoeana na mdogo wako wa kike? Kumsisitiza kusoma ni kosa? Nimeukumbuka uzi humu wa jamaa akisema hakuna kucheka cheka na mwanamke awe ndugu yako au mtu baki, nimeamini sasa. Mbaya zaidi haya matusi amesikia mpaka house girl, ambaye tulikuwa tunaheshimiana sana. Hivi nitamuangaliaje usoni? Kifupi sipo sawa, bora angekuwa mtoto ndiye amenitukana, ila huyu binti wa form four mwenye akili timamu mwenye miaka 20 hapana.

Bado sijaamini! Sijui cha kuomba ni nini, ushauri au... Nashindwa ku type sipo sawa.
Miaka 20 form four huyo kachelewa Sana kuanza shule aisee . Umri huo alistahili kuepo form six na pia miaka 20 huyo sio mtu wa kumuamuliia ishu nzima ya mahusiano kabisa
 
Sasa dogo amekua ashaonja rungu ndo unataka uendelee kumjaza sumu ambazo anaona ni uduwanzi😂😂😂😂
 
Mbona hayakutukana.Kakuambia kweli.Ungetukanwa ingekuaje?.Mwache kuku apewe mchele aliwe na wali.
Kwani kuku wako?
 
Tatzo limeanzia kwako Wew kaka mkubwa, Mpaka Leo unakaa kupishana na Dada zako Hapo kwenu alikusema vile mbele ya Dada wa kazi Ili uondoke ukapange kwako na kingne uache kufatilia mambo yawanawake .
 
Mkuu..kwel hilo la dogo tena wa kike kukutolea shiit sikubaliani nalo..mm madogo zangu wa kike hatutofautian ki umri ila wameniheshmu mpk wameolewa....yaan wao wakiwa form four mimi nipo chuo mwka wa kwanza nlikuwa nawapasua hadi wakawa wananiogopa.....bora uogopwe kulikon utolewe shiit na mtt wa kike
 
Miaka 26 bado upo kwa mama unasubiri chakula cha hausigeli. Huyu mdogo wako kakushauri vyema kuwa uwe kama mwanaume. Sasa wewe endelea kutetemeka hapo halafu kesho umwombe mama hela ya kunyolea ndevu na vyuzi lako
 
Baadae apate mimba zisizo eleweka, alete shida home & brother kupigwa vizinga vya dawa za mtoto (uncle)
Mabinti bhana
mtoto akililia wembe mpe
narudia tena mtoto wa kike hachungwi
 
Back
Top Bottom