Mdogo wangu wa kike kapotea tokea siku ya ijumaa

Mdogo wangu wa kike kapotea tokea siku ya ijumaa

Hawa watoto wa kike wanaweza kufanya wazazi watembee njiani huku wanaongea peke yao.

Utateseka sana, mwache atarudi tu, ila ndo hivyo tena.
 
Wakuu,,,kichwa kinauma sana,..malezi ya watoto wa kike ni magumu sana.

Dogo mara ya mwisho aliga anaenda kujaza fomu shule,...yaani ndio hawa madogo wamemaliza mitihani juzi ya necta. Sasa kutokea ijumaa alivoondoka ndio hadi sasa hajaonekana.

Nilivofikishiwa na bi mkubwa hizi taarifa imenibidi nisafiri ndio nimeeingia saivi Dar maana nilikuwa Dodoma.

Yani dogo katumia uzaifu wa wazee kaona anawamudu kwa hiyo katokomea alipotokomea nimefatilia RB,...nimepeleleza kwa rafiki yake akadai kuna boda ndio huwa anaonekana nae....

Sasa shida inakuja namna ya kumtaiti huyu boda maana naingia gharama ambazo ni nyingi za usafiri na ufatiliaji. Hivi kitu kama hiki kama kilishatokea mlifanyaje wakuu...kichwa ni kinauma sana wakuu ....

Jua kali mno kumtafuta mtu aliyejificha.
================
Nilichopanga Kufanya
================

Kesho nimejipanga nianzie shuleni alikokuwa akisoma,..kisha niwaelezee walimu wake situation nzima...baada ya hapo nitamuomba rafiki yake ...na binti ...anipe ushirikiano wa kunionesha huyu boda aliyemchukua mdogo wangu...sitaki nimuingize huyo rafiki wa binti kwenye majanga ...kisha nikishamjua nitamkodi hadi gogoni kituo cha polisi nikifika pale ...nitamwambia aingie tu hmna wasiwasi ...

Nitawaeleza polisi kila kitu kisha tutamnasa kirahisi sana...

Mods onganisheni huu uzi na ule niliouweka awali...
Mtangaze kwenye radio na kwenye mitandao.
 
mkuu hujapitia hayo yakutafuna watoto za watu....acha na wenzako wajilipe...kawaida sana lazima wana waisraeli waipitishe jangwani kabla hajaingia inchi ya ahadi....enzi zangu binti alichungwa nikaenda ipigia kwenye chumba chake mdngi akanifuma.....demu akavunja mlango aniserve...kwa mimi siangaiki kabisa na hawa wadogo zangu.... kuna siku niliiingia chumbachao nilikuta azuma kama box 800.....utapambana na vijana wa watu kumbe kenyewe ni kaajenti ka kiwanda cha azuma kusambaza gono...
 
Umenikumbusha mbali kisa cha rafiki yangu. Binti kabaki peke yake na Mama yake kwa sababu Kaka zake wote wako mbali kikazi.

Akaanza usumbufu kama huo, Mama kila wakati anampigia rafiki yangu juu ya tabia za mdogo wake. Rafiki alimwambia sasa ushauri wa mwisho achana naye kabisa. Sisi kama Watoto wsko tunataka ufurahie maisha yako ya Uzee.

Binti baada ya miezi sita karudi kwao na mimba. Mhusika kakimbia, kawa mpole.

Sasa hivi Binti kanyooka na ni msaada mkubwa pale kwao hasa kumsaidia Bi Mkubwa na masuala pia ya logistics.
 
Back
Top Bottom