Mdude CHADEMA: Hii katiba haifai, Wazanzibari wanakuwa wakuu wa wilaya Tanzania bara huku Watanganyika hawaruhusiwi kuwa wakuu wa wilaya Zanzibar

Marekani kashampeleka mwenzenu kuzimu huko Somalia, mfadhili mkuu wa yale ma ISIS ma-ndugu yenu katika dini
Tumekusikia jibu swali

Nani alijitoa mhanga Zanzibar?
Mnatuletea vijikanisa vya mashoga Kama kule Mbeya mkizuiwa mnapiga kelele
 
Ukuu wa wilaya Tanganyika na chenyewe ni cheo cha muungano? hangaya anaihujumu Tanganyika waziwazi........tunahitaji katiba mpya haya mambo yakae sawa.
 
Huyo Mwinyi mdogo mwenyewe baba yake Mtanganyika. Utashangaa akimteua Mtanganyika, kama ulivyodai!?
 
Huyo Mhandisi Zena anatokea wapi na wizara aliyokuwa anaiongoza kama katibu mkuu ni ya muungano au siyo ya muungano? Pili alipoteuliwa na Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi je aliteuliwa kama mtu kutoka Bara au Zanzibar? Rudi darasani Kisha uje upost vitu vinavyoeleweka na pia achana na uccm au uchadema tunapoongelea mambo muhimu kama haya.
Kwa ujumla Shaka hafai kuwa mkuu wa wilaya huku bara kwani TAMISEMI siyo wizara ya muungano.
 
Aache roho mbaya, wote ni watanzani, kinachopaswa kufanywa ni kupeleka na wabara kwenye wilaya za Zanzibar. Tuache ubaguzi
Katiba haitoi haki hiyo ila rais katumia mamlaka yake yeye kinyume na katiba.Hakuna mtu wa Tanzania bara anayeweza kuwa Hata VEO Zanzibar.
 
Wajukuu hao si Wazanzibari kwa sheria za huko. Hata waliozaliwa Zanzibar ila hawaishi huko kwa zaidi ya miaka mitano si Wazanzibari.
Wanaweza kupata Uzanzibari kwa kwenda kuishi Zanzibar?
 
Ndio maana Katiba mpya ni muhimu ili irekekebishe mapungufu mengi yaliyojitokeza kwenye muungano na kwenye nyanja zinginezo ! Lakini utasikia wengine wanahoji eti kwani Katiba mpya itakuletea chakula mezani ? Jibu lao ni kwamba hapa duniani hatuishi ili tule bali tunakula ili tuishi tuweze kufanya mengine mengi yanayostahili kufanywa !!
 
Kiongozi atakae kuja kuifanya zanzibar kama mkoa.Tanzania ikawa moja atakua kalifanyia taifa hili jambo la kukumbukwa daima.

Tanganyika ilikufa baada ya kuzaliwa Tanzania, kwann zanzibar iwe hai [emoji2357].Tanzania ndo cha kuzingatiwa hakuna cha Tanzania zanzibar au Tanzania bara,hii inachochea huu ubaguzi.

Nyerere na karume walileta muungano si kosa kuboresha walichokifanya ,Rais awe na cheo cha President of Republic of Tanzania.

Kama ilivo kwa mtu wa mwanza kufany chochote arusha bas iwe ivo ivo kwa mtu wa kigoma kufanya chochote zanzibar kuanzia kumilik ardhi na mambo meng.

Nchi ndan ya nchi ni jibu la kwann mpka leo Ajenda za madara zinashika chart.

#MABORESHO
#KWENYE
#MUUNGANO
 
Ushawai ona mbara kaenda kuwa rais kule.. ila wa kule akhaaa.
 
Wanaweza kupata Uzanzibari kwa kwenda kuishi Zanzibar?
Mtanzania yeyote akiishi Zanzibar kwa miaka 5 mfululizo anakuwa Mzanzibari. Ila ni sheria za ajabu sana za kumpokonya uraia mtu kwa kuwa haishi huko. Kama Uzanzibari waweza kuitwa uraia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…